NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 8 Mei, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Moja leo ni Kikao cha Ishirini na Nne. Katibu. NDG. ASIA MINJA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 197 Hitaji la Watumishi na Vifaa Tiba – Hospitali ya Wilaya ya Newala MHE. JAMES F. MBATIA (K.n.y MHE. RASHID A. AKBAR) aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuipatia Hospitali ya Wilaya ya Newala watumishi pamoja na vifaa tiba? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA(MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Ajali Akbar, Mbunge wa Newala Vijijini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi kwa kuhakikisha vituo vinakuwa na vifaa tiba vinavyohitajika. Hospitali zinapatiwa rasilimali watu na fedha kwa ajili ya kununua dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi. Katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi 198,671,475mpaka sasa shilingi 120,510,860 zimepokelewa kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa. Katika mwaka wa fedha 2018/19 Serikali imetenga shilingi 244,066,959.92 kwa ajili ya vifaa tiba na dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Newala. Mheshimiwa Spika, uhaba wa watumishi ni changamoto inayovikabili vituo vingi vya kutolea huduma za afya nchini. Hata hivyo Serikali inaendelea kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya kadri vibali vya ajira vinavyopatikana. Mwezi Novemba, 2017 Halmashauri ya Mji wa Newala ilipata watumishi 12 wa kada mbalimbali za afya na katika mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri imeomba kibali cha kuajiri watumishi 60 wa kada mbalimbali za afya. Serikali itaendelea kupeleka watumishi wa afya, vifaa tiba na vitendanishi ili kuboresha huduma za afya katika Wilaya ya Newala. SPIKA: Mheshimiwa Mbatia nilikuona, swali la nyongeza. MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Vifaa tiba ni tatizo kubwa kwenye hospitali nyingi nchini na utajiri mkubwa tulionao kuliko wote ni afya za mwanadamu. Mheshimiwa Spika, swali, Wizara hii ina upungufu wa zaidi ya sekta ya afya zaidi ya asilimia 50 ya watumishi. Serikali inaji-commit nini kuhusu kuhakikisha watumishi wa kutosha wa Hospitali ya Newala wanapatikana kwa wakati ili waweze kutoa huduma zinazostahiki? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, swali la pili, Hospitali ya Kilema iliyoko Vunjo au ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ina tatizo la vifaa tiba na watumishi wake kwa wakati huu nesi mmoja anahudumia zaidi ya watu 30 wodini. Serikali inatoa kauli gani hapa ili hospitali hii nayo ipate watumishi wa kutosha pamoja na vifaa tiba kwa ajili ya afya za binadamu? SPIKA: Majibu ya maswali hayo. Mheshimiwa Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Josephat Kandege. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, kuhusiana na commitment ya Serikali ili kuhakikisha kwamba watumishi wa afya wanapelekwa wa kutosha Newala ni kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi. Maombi yao ni kupatiwa watumishi 60 na hii naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbatia kwa niaba ya Mheshimiwa Ajali Akbar kwamba ni commitment ya Serikali kuhakikisha pindi fursa za ajira zitakapokuwa zimetolewa hatutaisahau Newala. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Hospitali yake ya Kilema ambayo anasema wastani Nesi mmoja anahudumu wagonjwa 30 ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba tunaweka vifaa vya kutosha lakini pia na watumishi wa kutosha. Ndio maana wakati Mheshimiwa Waziri wa dhamana ya ajira alivyokuwa anahitimisha alisema ndani ya Bunge hili tunategemea kuajiri watumishi wa kutosha. Katika watumishi 59,000 watakaoajiriwa sehemu kubwa ni upande wa elimu na afya, naomba nimuhakikishie ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba tunapunguza mzigo mkubwa kwa wahudumu kwa maana ya manesi ili na wao wawe na fursa ya kuweza kuhudumia wagonjwa kwa uzuri zaidi. Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie na Hospitali ya Kilema tutaikumbuka. SPIKA: Nilikuona Mheshimiwa Nape Nnauye, swali la nyongeza tafadhali. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza. Katika sekta iliyoathirika sana wakati wa zoezi la uhakiki wa vyeti, suala zima la vyeti fake ni sekta ya afya. Jimboni Mtama baadhi ya zahanati tumelazimika kuzifunga kabisa kwa sababu watu wameondolewa. Mheshimiwa Spika, sasa kwa nini Serikali isichukue hatua za dharura kwenye haya maeneo ambayo zahanati zimefungwa badala ya kusubiri process hii ya kuajiri watumishi wapya wa afya? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Spika, katika maeneo ambayo nilifanikiwa kupita na kuona kazi nzuri ambayo imefanyika katika suala zima la ujenzi wa vituo vya afya ni pamoja na Jimbo lake la Mtama, kwanza naomba nimpongeze. Mheshimiwa Spika, tukiwa hapa ndani bungeni Mheshimiwa Mkuchika alitoa taarifa kwamba kama yuko Mbunge yeyote, wa eneo lolote ambalo tumelazimika kufunga zahanati au kituo cha afya kwa sababu ya ukosefu wa watoa huduma aandike barua ampelekee ili tatizo hili lisiweze kutokea. Mheshimiwa Spika, naomba kama Mheshimiwa Mbunge hakuwepo siku hiyo atumie fursa na bahati nzuri yeye yuko jirani sana na Mheshimiwa Mkuchika ili hicho anachokisema kisiweze kutokea. SPIKA: Tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na swali linaulizwa na Mheshimiwa Alex Raphael Gashaza, Mbunge wa Ngara. Mheshimiwa Gashaza tafadhali. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na.198 Hali ya Usalama katika Jimbo la Ngara MHE. ALEX R. GASHAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu kumekuwepo na tatizo kubwa la hali ya usalama katika Jimbo la Ngara tangu mwaka 1993 kutokana na kuwa mpakani mwa nchi za Rwanda na Burundi ambapo kuna mwingiliano mkubwa wa wageni/wahamiaji haramu kutoka nchi hizo. (a) Je, ni lini Serikali itaanzisha Kanda Maalum ya Kipolisi katika Wilaya ya Ngara ili kudhibiti hali ya usalama? (b) Je, ni lini Serikali itajenga vituo vya polisi katika Kata ya Mabawe, Muganza, Kirushya, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa? (c) Kwa kuwa Jeshi la Polisi Wilayani Ngara lina gari moja tu zima na lingine bovu bovu, je, ni lini Serikali itatupatia angalau magari mawili, moja kwa ajili ya Tarafa ya Rulenge na la pili kwa ajili ya Tarafa ya Murusagamba? NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Alex Gashaza, Mbunge wa Ngara lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, hali ya usalama katika Jimbo la Ngara kwa sasa imeimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita. Wilaya ya Ngara imepakana na nchi jirani za Rwanda na Burundi. Serikali imeweka mikataba ya ujirani mwema na nchi za Rwanda ambapo Jeshi la Polisi hufanya doria za pamoja mipakani. Mheshimiwa Spika, kuna changamoto katika mipaka yetu na nchi ya Burundi inayotokana na kukosekana kwa 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) amani katika nchi hiyo na kupelekea watu kuvuka mipaka. Aidha, Jeshi la Polisi nchini limeanzisha vituo vya ulinzi shirikishi ili kujenga uhusiano wa pamoja na wananchi ili kuimarisha hali ya usalama katika eneo hilo. Kwa sasa hali ya usalama katika eneo hilo imeimarika na hakuna haja ya Serikali kuanzisha Kanda Maalum ya Kipolisi. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua tatizo la uhaba wa vituo vya Polisi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Ngara na katika Kata za Mabawe, Muganza, Kirushya, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa. Aidha, katika Kata ya Muganza kitajengwa Kituo cha Polisi eneo la Mkalinzi kwa nguvu za wananchi ambapo katika Kata za Mabawe, Mtobeye, Mbuba na Nyakisasa Polisi hutoa huduma kupitia Vituo Maalum vya Operesheni vya maeneo ya Murugyagira, Rulenge, Kabanga na Bugaramo. Hata hivyo, Serikali itajenga vituo vya polisi katika maeneo hayo kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tusikilizane, hii ni sauti ya zege, kwa hiyo msiwe na wasiwasi. (Kicheko) Mheshimiwa Gashaza swali la nyongeza. MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nitaomba kuuliza maswali ya nyongeza kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ngara kimejengwa tangu enzi za ukoloni na majengo yake yamechakaa pamoja na nyumba za watumishi kwa maana nyumba za askari wetu. Sasa ni lini Serikali itaweza kukarabati kituo hiki cha polisi na nyumba za askari wetu? Mheshimiwa Spika, swali la pili, wananchi wa Jimbo la Ngara wameathirika kwa kiasi kikubwa sana na operesheni zinazoendelea hususani za Uhamiaji. Maeneo mengi Dar es Salaam, Kahama, Arusha, Ngara kwenyewe wananchi hawa wanapokamatwa kwa kuhisiwa na kueleza kwamba wanatokea Ngara moja kwa moja wanachukuliwa kwamba 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ni wahamiaji haramu. Wamekuwa wakipigwa na kuumizwa na baadaye baada ya kujiridhisha inaonekana kwamba ni Watanzania halisi. (Makofi) Sasa je, Serikali iko tayari pale inapobainika kwamba wananchi hawa wamehisiwa, wakadhalilishwa, wakapigwa wako tayari kulipa fidia kwa hawa wananchi wanaokuwa wamedhalilishwa na kupigwa? SPIKA: Majibu ya maswali hayo Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Mheshimiwa Engineer Masauni tafadhali. NAIBU WAZIRI
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages184 Page
-
File Size-