NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Nane – Tarehe 13 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu Tatu, leo ni Kikao cha Nane. Katibu NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI SPIKA: Hati za kuwasilisha Mezani, Mheshimiwa Waziri Mkuu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA): Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2021/2022. MHE. JOSEPH K. MHAGAMA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, baadaye tutakapokuwa tunaisoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni muhimu vilevile kupitia Hotuba za Kamati, zinasaidia kutoa picha pana zaidi kuhusiana na Ofisi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa nimuite Mwenyekiti wa Kudumu ya Bajeti na wale Wenyeviti wengine wasogee karibu karibu. Mheshimiwa Shally J. Raymond, karibu sana. MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana, hiyo ndiyo Kamati ya Bajeti. Sasa twende Kamati ya Masuala ya UKIMWI. Waheshimiwa Wabunge wengine mnaiita Kamati ya UKIMWI hapana, ni Kamati ya Masuala ya UKIMWI. Endelea Mheshimiwa. MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya na Tume ya Uratibu na Kudhibiti UKIMWI kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. HUMPHREY H. POLEPOLE - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Uchambuzi wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Humphrey Polepole, Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, uliza swali lako. Na. 60 Kuruhusu Wananchi Kandokando ya Barabara Kufanya Biashara kwa Saa Ishirini na Nne MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Je, Serikali ipo tayari kuruhusu wananchi wanaoishi kwenye Miji ambayo ipo kando ya barabara kuu kama Mji wa Mafinga kufanya biashara kwa saa ishirini na nne? SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Mheshimiwa David E. Silinde, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kubuni mikakati mbalimbali katika kuwaendeleza wafanyabiashara wadogo ikiwa ni pamoja na kuwatengea maeneo kwa ajili ya kuendesha biashara zao na kuwatambua kwa kuwapatia vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo na watoa huduma. Kutokana na uhaba wa maeneo ya kufanyia biashara kwenye baadhi ya Miji, yameanzishwa masoko ya usiku ambayo yanaendeshwa kwa kufunga baadhi ya Mitaa nyakati za jioni hadi usiku kwa ajili ya kupisha wafanyabiashara wadogo kuendesha biashara zao. Baadhi ya Halmashauri hizo ni Jiji la Dodoma, Jiji la Dar-es-Salaam na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji. Mheshimiwa Spika, uendeshaji wa biashara nyakati za usiku umeonekana kuwa na changamoto nyingi za ulinzi na usalama wa wafanyabiashara, wateja pamoja na bidhaa zao. Uzoefu unaonesha kuwa maeneo zinakofanyika biashara kwa saa 24 kuna miundombinu yote muhimu ikiwemo taa, kamera, vyoo na maeneo ya kuhifadhia bidhaa za wafanyabiashara. Aidha, ili kuwa na usalama wa uhakika katika masoko, kunahitajika ulinzi wa Polisi au Askari wa akiba kwa maana ya Mgambo, hususan nyakati za usiku. Serikali kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama itaendelea kutafuta namna bora ya kuwezesha wafanyabiashara waishio kwenye Miji kando ya barabara Kuu ikiwemo Mafinga kufanya biashara zao kwa saa 24 ikiwa ni pamoja na kuweka miundombinu ya msingi. SPIKA: Mheshimiwa Cosato Chumi, swali la nyongeza. MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Leo tutajadili hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na sehemu ya hotuba hiyo tutajadili suala la ajira hususan kwa vijana. Nina maswali mawili ya nyongeza kwa Serikali. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, tunaishukuru Serikali iliruhusu tusafirishe mazao ya misitu kwa saa 24 na hivyo kusisimua na kuchechemua uchumi sio wa Mafinga tu na maeneo mengine. Je, Serikali iko tayari kufanya upendeleo maalum kwa Mji wa Mafinga kutokana na nature yake ya kibiashara kuruhusu baadhi ya maeneo watu kufanya biashara saa 24 na yenyewe ikabaki na suala la ulinzi ambayo ni kazi kuu ya Serikali? Mheshimiwa Spika, swali pili, katika jibu la msingi Serikali imesema kuna changamoto ya miundombinu muhimu kama vile taa, kamera na kadhalika. Sisi kama Halmashauri tuko tayari kujenga baadhi ya miundombinu lakini je, Serikali iko tayari kutusaidia japo taa za barabara katika maeneo muhimu katika njia panda za Itimbo, Madibila, Mufindi na Sokoni ili kuwawezesha wananchi hawa kuendelea kujiajiri na kujipatia kipato na hivyo kuwa na mchango katika Serikali na mifuko yao? SPIKA: Maswali mazuri sana haya, majibu Naibu Waziri, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu maswali madogo ya nyongeza ya Mheshimiwa Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Mheshimiwa Mbunge alikuwa anataka upendeleo maalum kwa Mji wa Mafinga ili uweze kufunguliwa. Katika jibu langu msingi nilieleza kabisa moja ya jukumu kubwa la Serikali ambalo tunalifanya sasa ni kuhakikisha tunajenga miundombinu na usalama unakuwepo. Baada ya kutathmini ndipo tunaweza kuruhusu Mji wa Mafinga ili uweze kufanya biashara kwa saa 24. Mheshimiwa Spika, swali la pili ambalo ni la msingi kabisa Mheshimiwa Mbunge ameainisha commitment ya Halmashauri yake kwamba wao kama Mafinga Mji wako 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) tayari kujenga baadhi ya miundombinu muhimu na sisi kama Serikali tuweze kusaidia katika kuweka hizo taa za barabarani. Nafikiri wazo hilo ni jema na mimi niungane kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kusema kwamba tunaomba Halmashauri ya Mji Mafinga waanze hiyo hatua ya kutengeneza hiyo miundombinu muhimu na sisi tutatuma wataalam wetu waende kufanya tathmini, ili tuweze kuwaruhusu waweze kufanya hiyo biashara yao kwa saa 24 na sisi tutawasaidia katika hiyo sehemu itakayobakia. SPIKA: Tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na swali linalofuata, bado tuko TAMISEMI, swali linaulizwa na Mheshimiwa Tunza Issa Malapo. Na. 61 Tatizo la Kujaa Maji baadhi ya Maeneo ya Mtwara Mikindani MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya kujaa maji mara tu mvua zinaponyesha katika baadhi ya maeneo ya Kata za Magomeni, Shangani, Ufukoni, Reli na Likombe katika Manispaa ya Mtwara Mikindani? SPIKA: Bado tuko TAMISEMI, Mheshimia David Silinde, majibu ya swali hilo, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya kujaa maji mvua zinaponyesha katika baadhi ya maeneo ya Kata za Magomeni, Shangani, Ufukoni, Reli na Likombe katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Katika mwaka wa 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) fedha 2017/2018, Serikali kupitia Mradi wa Uendelezaji Miji (Tanzania Strategic Cities Projects) imejenga mifereji ya kutoa maji kwa maana ya stand-alone drains yenye urefu wa kilomita 10 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.82 katika Kata za Shangani, Reli, Likombe na Vigaeni Manispaa ya Mtwara Mikindani. Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kukamilisha Mpango Kabambe wa kuyaondoa maji ya mvua katika makazi na kuyaelekeza baharini katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Serikali itatafuta fedha ili kutekeleza kikamilifu Mpango Kabambe wa kuondoa maji ya mvua kwenye makazi na kuyaelekeza baharini katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. SPIKA: Mheshimiwa Tunza Malapo, nimekuona. MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali imejenga mifereji katika baadhi ya maeneo, lakini mfereji wa kutoa maji kutoka Kata ya
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages276 Page
-
File Size-