Majadiliano Ya Bunge ___Mkutano Wa Kumi Na Sita

Majadiliano Ya Bunge ___Mkutano Wa Kumi Na Sita

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Thelathini na Nane - Tarehe 2 Agosti, 2004 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha kwa Mwaka 2002/2003 (The Annual Report and Audited Accounts of the Arusha International Conference Centre for the Year, 2002/2003). WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2004/2005. MHE. JOHN S. MALECELA - MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha Uliopita, Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2004/2005. 1 MASWALI NA MAJIBU Na. 355 Benki ya Dunia Kufadhili Utengenezaji wa Barabara za Manispaa MHE. LEONARD N. DEREFA aliuliza:- Kwa kuwa Manispaa karibu zote nchini zinafadhiliwa na Benki ya Dunia katika utengenezaji wa barabara za lami na mitaro katika barabara za Manispaa hizo lakini Manispaa ya Shinyanga haimo katika miradi hiyo tangu ianze mwaka 2000 hadi sasa. Je, ni lini sasa Manispaa hiyo ya Shinyanga itawekwa katika miradi hiyo ili barabara zake ziweze kutengenzwa na kuboreshwa na kuifanya Manispaa hiyo iwe kwenye hadhi inayofanana na Manispaa nyingine nchini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leonard Derefa, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mradi wa Huduma Mijini (Urban Sector Rehabilitation Project), pamoja na shughuli nyingine, ulihusika kutengeneza barabara na mifereji ya maji ya mvua kwa baadhi ya Manispaa. Mradi huu ulianza mwaka 1997 na ulitekelezwa katika Manispaa za Arusha, Moshi, Tanga, Morogoro, Iringa, Mbeya, Dodoma na Majiji ya Mwanza na Dar es Salaam. Wakati huo Mji wa Shinyanga ulikuwa bado haujapewa hadhi ya Manispaa. Mradi huu umegharamiwa kwa kiasi kikubwa na mkopo toka Benki ya Dunia na unatarajiwa kufungwa rasmi ifikapo Desemba, 2004. Kwa hiyo, fedha zote zimekwishatumika. Chini ya Mradi huo, jumla ya Kilometa 104 za barabara za lami kati ya Kilometa 210 za barabara za lami zilizomo katika Manispaa hizo ndizo zimeweza kukarabatiwa. Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya Mpango wa Kuzisaidia Serikali za Mitaa uitwao Local Government Support Programme, utakaowezesha kupatikana kwa fedha zaidi kwa ajili ya Bajeti za Maendeleo za Halmashauri katika maeneo ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu, ujenzi wa miundombinu katika maeneo yenye makazi duni ya Manispaa za Jiji la Dar es Salaam na kujenga uwezo wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri, wa kusimamia utekelezaji wa mpango huo. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mpango huu unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 121.7 na utaanza rasmi mwezi Januari, 2005 baada ya Serikali kuingia Mkataba na Benki ya Dunia mwezi Desemba, 2004. Ni matarajio ya Serikali kuwa, Halmashauri zitatumia vizuri fedha zitakazopatikana chini ya mpango huu ili kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu zikiwemo barabara na mifereji 2 ya maji machafu ya Manispaa ya Shinyanga. Napenda kumwomba Mheshimiwa Mbunge, avute subira na kuihamasisha Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, kuboresha utendaji wake ili ifikie viwango vitakavyoiwezesha kushirikishwa katika Mpango huu. Na. 356 Orodha ya Wafanyabiashara MHE. MOHAMED ABDULLY ALLY (k.n.y. MHE. MOSSY SULEIMAN MUSSA) aliuliza:- Kwa kuwa nchi zote duniani hutegemea kuongeza Pato la Taifa kupitia walipa kodi na hasa wafanyabiashara wakubwa:- (a) Je, Serikali imeorodhesha wafanyabiashara wangapi katika taratibu hizo za ukusanyaji mapato? (b) Je, ni wafanyabiashara wangapi wanaolipa sahihi katika taratibu hizo? (c) Je, ni wafanyabiashara wangapi sugu wanaokwepa taratibu hizo? NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. DR. FESTUS B. LIMBU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleiman Mussa, Mbunge wa Mfenesini, naomba kutoa maelezo mafupi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kimsingi kodi haiongezi Pato la Taifa bali ni namna ya kukusanya rasilimali zilizopo kwa lengo la kuzitumia kwa njia inayotoa manufaa makubwa zaidi kwa jamii nzima. Pato la Taifa hutokana na ongezeko katika uzalishaji bidhaa na huduma na si vinginevyo. Kwa upande mwingine, ukusanyaji mzuri wa kodi huiongezea Serikali uwezo wa kutoa huduma za kiuchumi na kijamii. Matumizi ya aina hiyo yanaweza kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kwa kadri yanavyoboresha mazingira ya uzalishaji wa bidhaa na huduma katika uchumi husika. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleiman Mussa, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2004, jumla ya walipakodi 236,392 walikuwa wameorodheshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Hii ni kwa mujibu wa Namba za Utambulisho za Walipakodi (TIN). Aidha, waajiriwa wasiopungua 795,809 wanalipa kodi chini ya utaratibu wa Pay As You Earn. (b) Mheshimiwa Spika, sio rahisi kusema ni walipa kodi wangapi wanalipa kodi zao kwa usahihi kwa kuwa ni mlipakodi mwenyewe anajua kwa uhakika usahihi wa kodi anayolipa. Hata hivyo, kumbukumbu za Mamlaka ya Mapato Tanzania zinaonyesha ongezeko katika uwajibikaji, yaani compliance kwa walipa kodi. Kati ya mwaka 1998/99 3 na 2002/2003, idadi ya walipa kodi ya mapato iliongezeka kutoka asilimia 80 hadi asilimia 82 na walipa kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka asilimia 80 hadi asilimia 94 katika mwaka 1998/99 na 2000/2001. (c) Mheshimiwa Spika, kutokana na uchunguzi uliofanywa na Kitengo cha Upelelezi wa Kodi (Tax Investigation), cha Mamlaka ya Mapato Tanzania, kwa kipindi cha miaka mitatu 2000/2001 hadi 2002/2003, takwimu zinaonyesha kwamba, idadi ya makosa imekuwa ikipingua, toka makosa 474 mwaka 2000/2001 hadi makosa 247 mwaka 2002/2003, japo thamani ya makosa hayo imeongezeka kwa karibu mara mbili katika kipindi hicho. MHE. MOHAMED ABDULLY ALLY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri, ametujibu kwamba hana hakika ya takwimu sahihi kwa wale ambao hawalipi kodi. Je, kutokuwa na takwimu hizo hahisi kwamba fedha za Serikali za Wananchi zinapotea? Pili, je, hawa wanaokataa kulipa, yaani wakwepaji kodi sugu, je, Serikali ina mkakati gani ili kuwezeshwa kukusanya fedha hizo? NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. DR. FESTUS B. LIMBU): Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, mlipa kodi mwenyewe ndio anajua kama analipa kodi sahihi ama halipi kodi sahihi. Lakini kwa wale wanaogundulika kwamba wamekwepa kodi, sheria zipo ambazo ni aidha kufilisiwa ama mali kukamatwa au kupelekwa Mahakamani. Tunasema kwamba, kama ikigundulika umekwepa kodi, inabidi ulipe asilimia 30 ya kodi ambayo unadaiwa halafu kama unakwenda Mahakamani au unakwenda kudai haki yako, basi umelipa hiyo asilimia. Mamlaka ya Mapato Tanzania pamoja na Wizara ya Fedha, imejitahidi sana kuelimisha walipa kodi na ninapenda nitumie nafasi hii kuwapongeza walipa kodi wanaolipa kodi kwa uaminifu, wamelisaidia sana Taifa hili kuongeza malipo ya kodi kutoka shilingi milioni 25 mpaka shilingi milioni 130 hivi sasa. Nawapongeza sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu wakwepaji kodi sugu, Serikali inapambana nao na Mamlaka ya Mapato imefanya mabadiliko makubwa katika vitengo mbalimbali na kuwa na One Stop Centre kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, inatoa huduma nzuri na zenye ufanisi zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Kuna baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakifahamika kwamba, yana wakwepaji kodi sugu. Maeneo hayo ni pamoja na Idara ya Mafuta ya Petroli, ambayo juzi Serikali imechukua hatua na toka imechukua hatua toka Bajeti iliyopita, makusanyo kwenye Sekta ya Petroli yameongezeka sana. Juzi tumefunga flow metre na hatua nyingine za kiutendaji. Pili, eneo lingine ambalo lilikuwa na matatizo ni Kodi ya Mapato. Sheria ya Kodi ya Mapato iliyopitishwa imeziba mianya mingi sana ambayo wakwepaji kodi walikuwa wanaitumia kutokana na Sheria hii ya Kodi ya Mapato kupitwa na wakati. Mheshimiwa Spika, napenda nitoe taarifa kwamba, Serikali imejizatiti vilivyo katika kuongeza mapato ya Serikali na napenda niwaombe wafanyabiashara wasiwe 4 wanakwepa kodi kwa sababu fedha zinazokusanywa na Serikali maendeleo yake yanaonekana. MHE. DR. THADEUS M. LUOGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Wananchi wengi katika nchi hii hawalipi kodi kwa sababu hawajawezeshwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwawezesha wakulima wadogo wadogo, wavuvi, wafanyabiashara wadogo wadogo ili wawe na uwezo wa kuchangia mapato ya Serikali yao kwa lengo la kuongeza mapato ya Serikali? (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Waziri mwenyewe, labda unajua namna ya kuwawezesha. Hebu jibu. (Kicheko) WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, hakuna Serikali yoyote duniani inayowezesha raia wake kulipa kodi. Hakuna! Raia wanajiwezesha wenyewe. Sisi tunamfuata yule ambaye amekwisha jiwezesha, ana ziada na anatakiwa alipe kodi, ndio huyo tunayemtoza. Lakini hiyo ni kwa kodi ya mapato. Lakini kwa kodi ya thamani, VAT ni mtu wa kawaida anapokwenda kununua mali dukani ndio anayelipa kodi hiyo. Kwa sababu kila mtu kila wakati ananunua kitu, basi

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    136 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us