Tarehe 4 Mei, 2021

Tarehe 4 Mei, 2021

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 4 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Ishirini na mbili. Katibu! NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO - K.n.y. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI A KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Husna Sekiboko kwa niaba ya Kamati. Katibu! NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali letu la kwanza leo tunaanza na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali hilo litaulizwa na Mheshimiwa Hassan Selemani Mtenga Mbunge wa Mtwara Mjini. Mheshimiwa Mtenga tafadhali uliza swali lako. Na. 179 Kujenga Barabara za Lami-Kata za Manispaa ya Mtwara Mikindani MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara za lami katika Kata za Ufukoni, Magomeni na shangani Manispaa ya Mtwara Mikindani. SPIKA: Majibu ya swali lako, Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde tafadhali majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais–TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Selemani Mtenga Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kama ifuatavyo: 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kujenga mundombinu ya barabara nakufanya matengenezo katika Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani ambapo katika mwaka wa fedha 2017/2018 kupitia Miradi ya Uendelezaji Miji yaani Tanzania Strategic Cities Projects Serikali ili jenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 4.53 katika Kata ya Shangani Manispaa Mtwara Mikindani kwa gharama ya shilingi bilioni 7.09. Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/ 2020 kupitiafedha za Mfuko wa Barabara Serikali imejenga barabara za lami zenye urefu wa kilomita 0.85 katika Kata ya Shangani kwa gharama ya shilingi milioni 232.98. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali imetenga shilingi milioni 117.38 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilomita 0.55 kwa kiwango cha lami katika mtaa wa Maduka Makubwa ambapo mkandarasi anaendelea na ujenzi. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21 barabara zenye urefu wa kilomita 22.37 zimefanyiwa matengenezo na kilomita 1.3 zinaendelea na matengenezo kwa gharama ya shilingi milioni 74.19 katika Kata za Ufukoni na Magomeni. Serikali inatambua ukuaji wa haraka wa Mji wa Mtwara naitaendelea kuupa kipaumbele cha barabara za lami na mifereji ya maji ya mvua kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. SPIKA: Mheshimiwa Mbunge wa Mtwara Mjini, nimekuona swali la nyongeza. MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, kwanza nitoe shukurani kwa majibu, lakini nataka niseme kwa mradi ambao unazungumzwa wa TACTIC mradi huu nadhani ulishapangiwa fedha, lakini mpaka sasa hivi jinsi ninavyozungumza kuhusu Kata ya Magomeni na Ufukoni bado hali ni mbaya. Je, Serikali ni lini ujenzi wa barabara hizi utakua tayari? Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili ni lini miundombinu ya mifereji ambayo tulikua tunaizungumza toka mwanzo Serikali itakua tayari kuweza kuboresha mifereji 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ambayo sasa hivi mara kwa mara kunapatikana mafuriko makubwa na wananchi inatokea hali sinto fahamu kwenye majumba ya watu na wengine kupoteza maisha. (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri TAMISEMI tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge ametaka kufahamu ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ambazo ameziainisha zilizopo katika mradi wa TACTIC kwa kifupi ni kwamba mradi wa TACTIC bado katika hatua za mwisho za makubaliano na mahafikiano na Serikali ili zianze kutekezwa. Kwa hiyo, Mbunge nikuhakikishie kabisa kwamba mara baada ya huu mradi kuwa umekamilika na Serikali kumaliza hatua zote, barabara hizo ambazo umeziainisha zitaanza kujengwa kwa sababu ziko katika mradi wa TACTIC. Mheshimiwa Spika, vile vile, katika sehumu ya ule mradi wa TACTIC miongoni mwa component ambazo ziko ndani yake ni pamoja na ujenzi wa mifereji kwa hiyo, mradi huu utakapokua umefikia hatua za mwisho na ninaamini Serikali ipo katika mazungumzo na ninahuhakika kabisa mara itakavyokamilia basi barabara zako pamoja na mifereji ya wananchi wa Mtwara Mjini itajengwa kama ambavyo imeainishwa katika huo mradi ahsante sana. SPIKA: Mheshimiwa Aida Khenani nimekuona uliza swali la nyongeza. MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru changamoto iliyopo Mtwara ya barabara inafanana sana na changamoto Nkasi. Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano alituahidi wana Nkasi kipande cha barabara kutoka Chala mpaka Mpalamawe, ningependa kupata commitment ya Serikali kwa kuwa ahadi zote zinakua recorded ni lini ahadi hiyo itatekelezwa. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ni lini ahadi hiyo itatekelezwa Mheshimiwa Naibu Waziri, David Silinde majibu tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ametaka kujua tu ni lini ahadi ya Mheshimiwa Hayati Rais ama niseme ahadi zote za viongozi ni kwamba sasa hivi Ofisi ya Rais, TAMISEMI ipo katika hatua ya mwisho tunakusanya na kuandaa mpango wa namna ya kutekeleza ahadi zote za viongozi na nikuhakikishie tu kwamba kuanzia mwaka wa fedha ujao tutaanza kutenga pole pole fedha kwa ajili ya kuhakikisha zile ahadi zote ambazo viongozi wakuu walikua wamezitoa zinaanza kutekelezeka. Mheshimiwa Spika, na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita ni Serikali makini na imeshazungumza hadharani kwamba kazi inaendelea yale yote yaliyozungumzwa tutayaendeleza kuhakikisha kwamba tunawahudumia wananchi wetu vizuri. Kwa hiyo, waambie wananchi wa Nkasi Kaskazini kwamba zile ahadi zilizoaidiwa Serikali itazitekeleza kwa vitendo ahsante. SPIKA: Tunaendelea na Wizara ya Utumishi na Utawala Bora, swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mheshimiwa Shangazi uliza swali lako tafadhali. Na. 180 Rushwa katika Mchezo wa Soka MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:- Vitendo vya rushwa vimekithiri sana katika mchezo wa soka hapa nchini. Je, ni kwa kiasi gani Serikali inakabiliana na kudhibiti hali hiyo? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika sekta ya michezo hususan mchezo wa soka hali inayoathiri maendeleo ya mchezo huu kwa ujumla, lakini pia kuikosesha Serikali mapato. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TAKUKURU imekuwa ikikabiliana na vitendo vya rushwa kwenye mchezo wa soka kwa kufanya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya viingilio katika mechi za mpira wa miguu. Matokeo ya uchambuzi huo yaliwezesha kubaini kwamba kuna mianya ya rushwa kwenye eneo hili ambapo baada ya kubana mianya hiyo mapato yaliongezeka hadi kufikia shilingi milioni 206 kwa watu 50,233 waliokata tiketi katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa mwezi Machi, 2019 ukilinganisha na mapato ya shilingi milioni 122 kwa watu 47,499 waliokata tiketi kwa mechi iliyochezwa Januari, 2019 kwenye uwanja huo. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa sekta ya michezo nchini, mwaka 2016 TAKUKURU iliunda Timu Maalum ya Uchunguzi kufuatilia na kuchunguza vitendo vya rushwa katika michezo ambapo kesi tatu zimefunguliwa mahakamani na tuhuma saba zinaendelea kuchunguzwa. Aidha, semina zimetolewa kwa makundi mbalimbali ikiwemo Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu (TAFCA), Waamuzi na Makamisaa wanaotumika katika michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza pamoja na kufanya vikao na viongozi 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wa Chama cha Mpira wa Miguu (TFF) kuhusu kuweka mikakati ya pamoja kuelimisha umma kupitia soka. Mheshimiwa Spika, nichukue fursa hii kuwataka TFF, wasimamizi wa soka na viwanja vya michezo waruhusu na kushirikiana na TAKUKURU kuweka matangazo ya kukemea rushwa kwenye soka na michezo kwa ujumla. SPIKA: Mheshimiwa Shangazi, swali la nyongeza. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali ambayo yanaonesha mwanga wa kupambana na rushwa katika michezo, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, je, ni hatua gani zimechukuliwa kwa watu ambao wamebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika michezo? Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni mkakati gani Serikali itatumia kuboresha mifumo ya uuzaji tiketi na kukusanya mapato, lakini pia kuziba mianya ili kuongeza mapato zaidi katika sekta hii ya michezo? SPIKA: Majibu ya maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri,

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    315 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us