Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NAMBILI Kikao cha Ishirini na Saba - Tarehe 18 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: - NAIBU WAZIRI WA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAZI: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Shirika la Nyumba la Taifa kwa Mwaka 2000/2001 (The Annual Report and Accounts of the National Housing Corporation for the year 2000/2001) Hotuba ya Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MHE. KIDAWA HAMID SALEH (k.n.y. MHE. ELIACHIM J. SIMPASA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO NA ARDHI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo na Ardhi kuhusu Utekelezaji wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi katika Mwaka uliopita, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 259 Ubinafsishaji MHE. MARIA D. WATONDOHA aliuliza: - Kwa kuwa baadhi ya malengo ya ubinafsishaji wa Mashirika ya Umma ni kuongeza ajira, soko la wakulima wa Tanzania na kuongeza Pato la Taifa: - (a) Je, tangu ubinafsishaji huo uanze kutekelezwa, ajira ya Watanzania imeongezeka kwa kiasi gani? (b) Je, ni mazao gani ya wakulima wa Tanzania yameweza kununuliwa kwa wingi na kuwaongezea kipato kutokana na ubinafsishaji huo? (c) Je, ni kiasi gani cha fedha kimepatikana kutoka kwa kila Shirika tangu mwaka 1998 - 2002? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI alijibu: - 1 Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maria Watondoha, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifauatavyo: - (a) Mheshimiwa Spika, tangu ubinafsishaji uanze kutekelezwa, ajira ya Watanzania kuongezeka ni wazi na imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Mashirika mengi yaliyobinafsishwa sasa yamefufuliwa na yameanza kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi na hivyo kuongeza ajira hususan nje ya Mashirika yenyewe. Mheshimiwa Spika, bidhaa nyingi zinazalishwa na kusambazwa kwa walaji wa hapa nchini na hata nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji mali na utoaji wa huduma mbalimbali katika Mashirika yaliyobinafsishwa, yote hii ikimaanisha ongezeko la ajira nje ya Mashirika yenyewe. Mheshimiwa Spika, aidha, ongezeko la ajira ya Watanzania kwa Mashirika yaliyobinafsishwa kama vile Kiwanda cha Bia, Kampuni ya Sigara, Viwanda vya Sementi linajionyesha kupitia kazi zinazofanywa na Sekta Binafsi mfano uwakala, ujenzi, matengenezo, usambazaji na kadhalika. Kiwanda cha Sukari cha Kagera kimeajiri wafanyakazi 1,050 hivi sasa wakati kilikuwa na wafanyakazi 120. Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa kimeajiri wafanyakazi 1,800 na ukichanganya wale wa muda wanafikia wafanyakazi 3,000. Mheshimiwa Spika, Mashirika yapatayo 70 yalikuwa yamefungwa hata kabla ya ubinafsishaji kuanza na hivyo wafanyakazi wote walipoteza ajira zao. Mengi ya Mashirika hayo sasa yamefufuliwa baada ya kupata wawekezaji wapya na hivyo yamejiajiri upya wafanyakazi. Hapa mfano ni Kiwanda cha Mablanketi, Kiwanda cha Kukausha Tumbaku (Morogoro), Kiwanda cha Viatu na kadhalika. Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inalifanyia tathmini ya kina zoezi zima la ubinafsishaji ili kujua matatizo yaliyojitokeza na mafanikio yaliyopatikana. Tathmini hiyo pia itaangalia suala la ajira mpya zilizopatikana katika uchumi kutokana na mafanikio yaliyopatikana utekelezaji wa zoezi la ubinafsishaji. (b) Mheshimiwa Spika, baadhi ya mazao ya wakulima Watanzania yaliyoweza kununuliwa kwa wingi kutokana na ubinafsishaji ni Chai (Rungwe na Lushoto baada ya viwanda husika kufufuliwa), Tumbaku (baada ya Kiwanda cha Kukaushia Tumbaku cha Morogoro kukarabatiwa na kuanza uzalishaji upya), Pareto (baada ya Kiwanda cha Mafinga kupata mwekezaji), Miwa ya wakulima wadogo wadogo (baada ya Viwanda vya Sukari vya Kilombero na Mtibwa kukarabatiwa na kuongeza uzalishaji). (c) Mheshimiwa Spika, thamani ya Mikataba ya ubinafsishaji kati ya mwaka 1998 hadi 2002 ni takriban shilingi bilioni 68.7 na takriban Dola za Kimarekani milioni 204.0. Kati ya fedha hizo, jumla ya shilingi bilioni 43.02 na Dola za Kimarekani 64.6 zimekwishalipwa. MHE. MARIA D. WATONDOHA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. (a) Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, je, atakubaliana nami kwamba ubinafsishaji haujaleta mafanikio makubwa sana hasa kwa ajira, kwa mfano, tukiona mgogoro uliopo sasa NBC na wengine wengi ambao wameachishwa katika Mashirika mbalimbali? (Makofi) (b) Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri amesema kuna mazao ambayo yameweza kununuliwa kwa wingi kama vile chai na tumbaku. Mikoa ya Lindi na Mtwara ni wazalishaji wakubwa wa korosho; je, Viwanda vya Korosho vya Mtwara na Lindi vingebinafsishwa si kwamba zao la korosho nalo lingepata soko kubwa na Wananchi wa kule kuajiriwa? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, ni dhahiri kabisa zoezi la ubinafsishaji limeongeza ajira, kwa sababu kabla ya zoezi lenyewe kufanyika zaidi ya viwanda 70 vilikuwa vimeshafungwa au vimefilisika na hivyo kupoteza ajira ya wafanyakazi hao. Baada ya viwanda hivi kufufuliwa ajira zilianza upya na kama nilivyotoa mifano katika maeneo mengi, watu wengi wameweza kuajiriwa. 2 Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la migogoro kama hiyo inayotokea NBC, ni lazima tuangalie mahusiano kati ya Menejimenti na Utawala kwa sababu hata katika maeneo ambayo viwanda vimeendelea, migomo kama hii inatokea kutokana na migogoro kadhaa ambayo inajitokeza kati ya menejimenti na wafanyakazi. (b) Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Maria Watondoha, kwamba ikiwa Viwanda vya Korosho vitabinafsishwa au tutapata wawekezaji vitasaidia sana kuongeza kwanza si tu thamani ya zao la korosho, lakini vile vile, upatikanaji wa ajira katika maeneo hayo. Sasa hivi Serikali kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho tunafanya jitihada ya kupata wawekezaji wa kuweza kuwekeza katika viwanda vile vya korosho. Mheshimiwa Spika, tatizo tunalolipata ni kwamba, viwanda vingi teknolojia yake ni ya zamani. Kwa hiyo, wakati wa uwekezaji huo ni lazima kufikiria taratibu ambazo zitafanya wale wawekezaji waweze kumiliki viwanda hivyo na kupata teknolojia mpya ya kisasa ili kuweza kufanya kazi kwa tija na ufanisi. (Makofi) MHE. DR. ZAINAB A. GAMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii, nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa baadhi ya viwanda vya korosho vilivyokodishwa kwa watu binafsi vilisababisha kero kubwa. Kwa mfano, katika Kiwanda cha Korosho cha Kibaha, wafanyakazi wake mpaka sasa hivi hawajalipwa pesa na matokeo yake wahusika wamekimbia. Je, Mheshimiwa Waziri anasema nini kwa wafanyakazi hao? (Makofi) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, wawekezaji waliowekeza na waliokodisha Kiwanda cha Korosho cha Kibaha, kwanza ni wawekezaji wa Tanzania. Taarifa nilizonazo ni kwamba, wawekezaji hawa wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za kuweza kupata fedha ili kulipa mishahara ya wafanyakazi husika. Sasa hivi kinachojitokeza ni kiwanda hiki kupeleka order ya korosho wapate fedha ili waweze kuwalipa wafanyakazi hao. Mheshimiwa Spika, ninachosema ni kwamba, siyo kwamba inaleta kero, lakini ukosekanaji wa mitaji na mbinu ya kutafuta mitaji hiyo ndiyo inayofanya ucheleweshaji utokee katika baadhi ya maeneo kama Kiwanda cha Korosho cha Kibaha, lakini kitaendelea vizuri. Na. 260 Kuhusu Utafiti wa Mkondo wa Biashara ya Korosho MHE. ABDULA S. LUTAVI aliuliza: - Kwa kuwa inasemekana kwamba Tume ya Kurekebisha Mashirika ya Umma imekamilisha utafiti juu ya mkondo wa biashara ya Korosho kwa nia ya kubaini manufaa ya kiuchumi ya kuuza korosho ghafi na zile zilizobanguliwa: (a) Je, utafiti huo umechukua muda gani na matokeo yake ni nini? (b) Baada ya matokeo ya utafiti huo; je, sera ya nchi yetu kuhusu uwekezaji kwenye Viwanda vya Kubangua Korosho itachukua mwelekeo gani? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UBINAFSISHAJI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdula Lutavi, Mbunge wa Tandahimba, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo: - (a) Mheshimiwa Spika, utafiti juu ya mkondo wa biashara ya korosho ulichukua kiezi sita na matokeo yake yamebainisha yafuatayo:- 3 (i) Tani 4.5 za korosho ghafi hutoa tani 1 ya korosho zilizobanguliwa. Bei ya mauzo ya tani 4.5 za korosho ghafi ni Dola za Kimarekani 3,375, ambapo tani ya korosho iliyobanguliwa ni Dola za Kimarekani 5,000. Kwa kuuza korosho iliyobanguliwa nchi inapata mapato zaidi. (ii) Kuwepo viwanda vya ubanguaji kunawezesha kupatikana by products kama vile Cashew Nuts Shell Liquid (CNSL) na maganda ya korosho ambayo hutumika katika kutengeneza chakula cha mifugo by products hizi pia huingiza mapato. (iii) Kuwepo viwanda vya ubanguaji kunaongeza ajira kwa Wananchi na pia soko la chakula kwa wakulima wa zao la korosho. Utafiti umebainisha kuwa viwanda vyenye uwezo wa kuzalisha tani 10,000 vinaweza kuajiri kati ya wafanyakazi 700 hadi 1,000. (iv) Ajira zaidi zitapatikana kwenye Kampuni zinazohusiana na Viwanda vya Korosho kama vile karakana za kukarabati na kutengeneza vipuri vya Viwanda vya Korosho. Mheshimiwa Spika, ikumbukwe pia, hivi sasa soko la korosho zetu ni soko tegemezi ikiwa korosho ghafi zinauzwa India ambapo baada ya muda si mrefu India itakuwa imejitosheleza katika uzalishaji wa korosho ghafi na hivyo kutoagiza korosho toka nje. Hivyo, utafiti huo ni changamoto kwa Taifa katika kuwezesha kuinua zao la korosho nchini kabla hali haijawa mbaya. (b) Mheshimiwa Spika, baada ya matokeo
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages93 Page
-
File Size-