Tarehe 11 Septemba, 2018

Tarehe 11 Septemba, 2018

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Sita– Tarehe 11 Septemba, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU – KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha mezani HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa shughuli za Serikali kwa mwaka wa fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa mwaka 2018 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018]. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. MASHIMBA M. NDAKI – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI: Maoni ya Kamati ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018]. MHE. HALIMA J. MDEE – MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani juu ya Wizara ya Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018] MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. RUTH MAKUNGU– KATIBU MEZANI: Maswali MASWALI NA MAJIBU Na. 68 Baadhi ya Raia Kushiriki Uchaguzi Tanzania na Msumbiji MHE. ABDALLAH A. MTOLEA (K.n.y. MHE. HAMIDU H. BOBALI) aliuliza:- Kumekuwa na raia wengi kutoka Msumbiji katika Jimbo la Mchinga hasa Vijiji vya Kilangala B, Butamba, Mvuleni, Kitolambwani na Kikonde ambao wamekuwa wakishiriki uchaguzi katika nchi zote mbili Tanzania na Msumbiji. (a) Je, raia hao ni Watanzania au wa Msumbiji? (b) Je, Serikali imepitisha utaratibu wa uraia pacha na kuwapa watu maalum? 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamidu Hassan Bobali, Mbunge wa Mchinga lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Ibara ya 5(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi unaofanywa Tanzania. Aidha, Ibara ya 5(2) ya Katiba hairuhusu mtu mwenye uraia wa nchi nyingine (raia pacha) kushiriki katika shughuli za uchaguzi ikiwemo kupiga kura. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ili mtu aweze kupiga kura lazima awe ameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura lililoanzishwa chini ya ibara ya 5(3)(a) ya Katiba. Uandikishaji wa wapiga kura unapokamilika, daftari la awali huwekwa wazi kwa mujibu wa kifungu cha 24 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya 343 ili kukaguliwa na wananchi. Kifungu cha 24(1) cha sheria hiyo kinatoa fursa kwa mtu aliyejiandikisha kuweka pingamizi dhidi ya mtu mwingine aliyendikishwa kwenye daftari ikiwa imebainika kuwa hana sifa ya kuandikishwa kwa kutokuwa raia wa Tanzania. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hali hii, sheria zetu hazijaruhusu uraia pacha na hakuna watu maalum waliopewa uraia wa aina hiyo. MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Mtolea. MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, majibu ya Serikali yanaonesha kwamba kumbe Tume ya Uchaguzi haiandikishi watu kwa kufuata vigezo bali inaandikisha yeyote atakatejitokeza na mzigo wa kuangalia nani ana vigezo na nani hana unabaki kwa wananchi kwamba waweke pingamizi, jambo hili siyo zuri. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba Tume ya Uchaguzi inapoandikisha wapiga kura ifuate vigezo vilivyoainishwa kisheria? Hilo moja. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kutokana na harakati za kiuchumi sasa hivi zilivyo duniani Watanzania wanaishi katika mataifa mbalimbali na wangependa kuendelea ku- enjoy ule Utanzania (utaifa) wao. Serikali ina mpango gani wa kuruhusu uraia pacha ili Watanzania walio nje na wenyewe waweze kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kama watanzania wanaoishi Tanzania? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante, majibu kwa maswali hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mavunde. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, KWA swali la kwanza, si kweli kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi ikiwa inawaandikisha Watanzania kushiriki kwenye uchaguzi haifuati vigezo vilivyowekwa. Kwa mujibu wa Katiba yetu na Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vigezo vimewekwa vya nani anapaswa kuandikishwa kwenye daftari la kupiga kura na ndiyo maana kifungu cha 24 cha sheria hiyo kimetoa mwanya kwa mtu yeyote ambaye ana pingamizi kwa mtu aliyeandikishwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, tafsiri yake si kwamba tume sasa inamchukua kila mmoja tu lakini kwa mujibu wa kifungu hicho imetoa nafasi hiyo ili yeyote mwenye pingamizi awasilishe pingamizi hilo kwa Tume lifanyiwe kazi na kama mtu hana sifa ataondolewa. Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la uraia pacha limezungumzwa mara zote, suala hili ni la Kikatiba muda utakapofika na itakapoonekana inafaa basi ninaamini sisi sote kama Wabunge na nchi kwa ujumla tutaenda katika mwelekeo huo, lakini kwa hivi sasa Katiba na sheria zetu haziruhusu uraia pacha. (Makofi) 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Mheshimiwa Maige. MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na mimi kuniruhusu niulize swali la nyongeza katika suala hili. Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kuhusu raia wageni kushiriki mambo ya ndani ya nchi yetu katika Jimbo la Mchinga inafanana sana na hali ilivyo katika kambi za wageni katika Mikoa ya Kigoma na Tabora hasa Ulyankulu na Katumba. Katika maeneo hayo wageni wamekuwa wengi wanafanya maamuzi kwa ajili ya Watanzania waliopo pale. Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaangalia wakimbizi wale wasifanye maamuzi yanayohusu Watanzania? (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante, majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Anthony Mavunde, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE): Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria za nchi yetu zimeweka wazi namna ambavyo wageni wataingia nchini na shughuli zao zote zinaratibiwa kwa mujibu wa sheria. Inapotokea kuna wageni wowote wameingia nchini wanafanya mambo kinyume na sheria tafsiri yake ni kwamba wanavunja sheria za nchi yetu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu limeletwa hapa Bungeni, tunalipokea na tutalifanyia kazi kuhakikisha kwamba wageni wote waliopo huko wafuate sheria za nchi yetu na pia tunawaagiza maafisa wetu wa Serikali kuhakikisha kwamba wanalifuatilia jambo hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. MWENYEKITI: Ahsante, tunaendelea Waheshimiwa Wabunge. Swali linalofuata linaulizwa na Mheshimiwa Godbless Jonathan Lema, Mbunge wa Arusha Mjini, bado linaelekezwa kwa Ofisi ya Waziri Mkuu. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 69 Umuhimu wa Serikali Kuzisimamia Taasisi Binafsi Kulipa Mishahara Stahili MHE. SUSAN A. J. LYIMO (K.n.y. MHE. GODBLESS J. LEMA) aliuliza:- Mishahara ya taasisi za umma hupangwa na Serikali. Utaratibu huo wa Serikali kupanga mishahara ya watumishi wake huathiri pia upangaji na ukadiriaji mishahara katika taasisi binafsi. Je, Serikali haioni haja ya kuboresha mishahara yake na kuzielekeza taasisi binafsi kulipa mishahara inayoendana na hali ya maisha? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA (MHE. ANTONY P. MAVUNDE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Godbless Jonathan Lema, Mbunge wa Arusha Mjini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha mishahara ya watumishi wake wa kada mbalimbali kila mwaka kwa kutoa nyongeza kulingana na kanuni za kiutumishi ikiwa ni pamoja na muda wa kukitumikia cheo au kupandishwa cheo mtumishi. Sambamba na utaratibu huu Serikali imeunda Bodi ya Kima cha Chini cha Mshahara ambayo hufanya utafiti kwa kuzingatia hali halisi ya maisha na uwezo wa kibajeti wa Serikali na kumshauri waziri mwenye dhamana na masuala ya utumishi wa umma kupanga kima cha chini cha mshahara. Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Taasisi za Kazi Na. 7 ya mwaka 2004 kama ilivyoboreshwa mwaka 2015 imeanzisha Bodi ya Mishahara ya Sekta Binafsi ambayo ina jukumu la kufanya utafiti kwa kuzingatia hali halisi ya gharama za maisha na masuala mengine ya kiuchumi na 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kupendekea kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa sekta binafsi. Serikali hivi sasa ipo katika hatua za kuiwezesha bodi hiyo kufanya utafiti ili kuhakikisha utafiti huo unakidhi matakwa ya sheria, kanuni na taratibu zinazokubalika hapa nchini na viwango vya kimataifa. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi na ukuzaji wa tija na uzalishaji sehemu za kazi unaboreshwa kila mwaka, Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na. 6 ya mwaka 2004 kama ilivyorekebishwa mwaka 2015, imeweka utaratibu kwa waajiri na wafanyakazi katika sekta binafsi kujadiliana na kufunga mikataba ya hali bora mahali pa kazi kwa lengo la kuboresha maslahi yao ikiwemo mshahara na stahiki nyingine. Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia utaratibu huu wa kisheria waajiri katika sekta binafsi wanaruhusiwa kuwalipa viwango vya mishahara hata zaidi ya kiwango kinachowekwa kama kima cha chini cha mshahara pale ambapo wanaona kwa

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    208 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us