JAMHURI YA MUUNGANO WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

IDARA YA MAMBO YA KALE

MAFANIKIO YA IDARA KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 - 2019

1 2 3 4

C C

Aprili 2019

1 2 Picha ya kwenye jalada inaonesha bonde la Olduvai (Olduvai Gorge) ni moja ya bonde ambalo ni maarufu Duniani kwa masalia mbalimbali ya Zamadamu yanayoonesha chimbuko la binadamu. Kutokana na tafiti zilizofanyika katika bonde hili zimegundua zamadamu walioishi miaka 1.75 hadi miaka milioni 2 iliyopita kama ifuatavyo (1 hadi 4 kwenye picha ya jalada): Australopithecus boisei(1) au Zinjanthropus boisie lililogunduliwa na Dkt. Mary Leakey na mumewe Dkt. Louis Leakey mwaka 1959; Homo habilis(2) aligunduliwa Mei 1960 Olduvai na Jonathan leakey mtoto wake leakey, ambaye inasadikika kuwa alitengeneza zana za Mawe Olduvai ziitwazo “Oldowan”; Homo erectus(3) aligunduliwa Olduvai Disemba 1960 na Dkt. Mary Leakey. Vilevile Dkt. Mary Leakey ndiye aliyegundua Homo sapiens (4) Olduvai. Aidha katika bonde hilo ziligunduliwa zana za mawe kama zinavyoonekana kwenye picha (c).

Haki zote za kunakili zimehifadhiwa © 2019 Wizara ya Maliasili na Utalii ISBN 978-9976-93594-9 Kimechapishwa na IPRINT LIMITED

i ii YALIYOMO DIBAJI...... v MUHTASARI...... vii SHUKRANI...... viii SURA YA KWANZA 1.0 Uhifadhi wa Malikale Tanzania Bara...... 1 1.1 Utangulizi...... 1 1.2 Historia ya Idara Mambo ya Kale...... 1 1.3 Sera, Sheria na Miongozo inayotumika kwenye Uhifadhi wa Malikale...... 2 1.4 Aina, Ubora na Umuhimu wa Malikale, Tanzania...... 3

SURA YA PILI 2.0 Majukumu, Muundo na Watumishi...... 8 2.1 Utangulizi...... 8 2.2 Majukumu ya Idara...... 8 2.3 Muundo wa Idara ya Mambo ya Kale...... 8 2.4 Watumishi wa Idara ya Mambo ya Kale na Viongozi...... 11

SURA YA TATU 3.0 Ushiriki wa Serikali na Sekta Binafsi katika Uhifadhi wa Malikale...... 14 3.1 Utangulizi...... 14 3.2 Umuhimu wa ushirikano wa Serikali na Binafsi katika Uhifadhi wa Malikale...... 14 3.3 Ushiriki wa Taasisi za serikali...... 14 3.4 Ushiriki wa Taasisi binafsi...... 19

SURA YA NNE 4.0 Mafanikio ya Idara katika Serikali ya Awamu ya Tano...... 21 4.1 Utangulizi...... 21 4.2 Uhifadhi na Uendelezaji wa Malikale...... 21 4.3 Makumbusho Mpya katika Kituo cha Bonde la Olduvai...... 21 4.4 Uendelezaji wa Kituo cha Kimondo cha Mbozi, Mkoa wa Songwe...... 23 4.5 Mfumo wa Kukusanya Maduhuli...... 29 4.6 Uendelezaji wa Vituo vya Mambo ya Kale Mkoa wa Iringa...... 29 4.7 Ukarabati wa BOMA la Iringa ...... 29 4.8 Uhifadhi na uendelezaji wa Makumbusho ya Chifu Mkwawa Kalenga...... 33 4.9 Mapango ya Amboni...... 39

iii 4.10 Uhifadhi wa Mji Mkongwe wa Mikindani Mtwara...... 41 4.11 Uhifadhi wa Michoro ya Miambani, Tanzania...... 47 4.12 Mafanikio ya Idara kwa Upande wa Taasisi Binafsi...... 49

SURA YA TANO 5.0 Kuendeleza Vituo vya Mambo ya Kale na Makumbusho...... 52 5.1 Utangulizi...... 52 5.2 Kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi...... 53 5.3 Taarifa ya Awamu ya Pili ya utekelezaji wa Maagizo...... 54 5.4 Kuendeleza Kituo cha kumbukizi ya Mwalim Nyerere Magomeni...... 58 5.5 Idara ya Mambo ya Kale kuhamisha majukumu kwenda Makumbusho ya Taifa...... 61

SURA YA SITA 6.0 Utangazaji na Uhamasishaji wa Vivutio vya Malikale...... 66 6.1 Utangulizi...... 66 6.2 Historia ya Utangazaji na uhamasishaji...... 66 6.3 Ushiriki wa Idara katika utangazaji na uhamasishaji...... 66 6.4 Maboresho kwenye Makumbusho za vituo vya Mambo ya Kale na Makumbusho...67 6.5 Maonyesho ambayo Idara ilishiriki 2018/2019...... 68 6.6 Tamasha la Urithi ...... 69 6.7 Kilele cha Tamasha lilifanyika Arusha...... 70 6.8 Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji...... 71

SURA YA SABA 7.0 Mikataba ya Kitaifa na Kimataifa na kutoa ushauri wa kitaalam...... 79 7.1 Utangulizi...... 79 7.2 Umuhimu wa Mikataba ya Kimataifa...... 79 7.3 Kufanya tathmini ya Majengo ya kihistoria yenye asili ya Kijerumani ...... 80 7.4 Mradi wa Kuhifadhi Magofu ya Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani...... 80 7.5 Mkataba kati ya Idara ya Mambo ya Kale na NCAA ...... 80

SURA YA NANE 8.0 Maoni, Ushauri na Hitimisho...... 81 8.1 Maoni au ushauri kuhusu Malikale...... 81 8.2 Hitimisho ...... 82 Kiambatisho Na. 1: Orodha ya Vituo vya Mambo ya Kale:...... 83 Kiambatisho Na. 2 Faharasa...... 86

iv DIBAJI Malikale ni urithi wa matokeo ya maisha ya binadamu katika harakati za kukabiliana na mazingira anayoishi wakati wa kutekeleza shughuli za kila siku. Katika kumudu maisha ya kila siku binadamu au kiumbe chochote lazima awe mbunifu wa teknolojia mbalimbali zitakazomwezesha kutengeneza vitu au rasilimali zitakazomwezesha kuishi na wale wanaoshindwa hutoweka. Malikale hizi zinazotengenezwa na jamii husika baada ya kuonekana ni muhimu huzitunza na kuzihifadhi na hatimaye hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine miaka hadi miaka. Urithishanaji huu wa malikale unakuwa ni sehemu ya utamaduni wao na huheshimiwa na jamii husika. Hivyo, Jamii huweka taratibu, kanuni na sheria za kuwezesha raslimali hizo kulindwa, kuhifadhiwa na hurithishwa kwa utaratibu maalum. Vilevile Malikale hujumuisha masalia ya binadamu, wanyama na mimea ambayo kutokana na tafiti mbalimbali zimeonyesha na kudhihirisha historia ya mabadiliko ya viumbe hivi kimaumbile, kifikra, kiteknolojia na kisayansi. Malikale pia hujumuisha mazingira aliyoishi au yaliyotumika na binadamu, wanyama na mimea. Malikale kwa ujumla ni urithi wa utamaduni unaonyesha binadamu alivyokuwa anaishi na hujumuisha mahali na mazingira aliyoishi, vitu alivyotumia, sanaa, teknolojia, fikra, mila na desturi kwa miaka kadhaa(ICOMOS 2002). Urithi huu huhifadhiwa kitaifa katika nchi mbalimbali na huweka utaratibu wa kuzihifadhi kiserikali au kwa kutumia sekta binafsi kwa ajili ya kumbukumbu ya kizazi kilichopo na kijacho. Pia, kwa baadhi ya nchi Malikale huendelezwa vizuri bila kuathiri uhalisia na kutumika kwa elimu na utalii ambao huchangia katika pato la Taifa. Malikale zenye sifa za kimataifa huhifadhiwa kama Urithi wa Dunia. Malikale katika Tanzania, kwa mujibu wa Sera ya Malikale ya mwaka 2008, hujumuisha rasilimali za urithi wa utamaduni zinazoshikika na zisizoshikika; zinazohamishika, na zisizohamishika, zilizo nchi kavu na majini ambazo zinadhihirisha mabadiliko ya kimaumbile, kifikra, zana, vyombo na mazingira aliyoishi na kutumia binadamu na zenye umri wa miaka mia moja (100). Malikale hizi zinajumuisha zana za mawe na chuma, vyombo vya usafiri, metali, miti na mifupa; visukuku vya binadamu, mimea na wanyama; michoro ya miambani; miji ya kihistoria, magofu ya majenzi. Rasilimali nyingine ni maeneo ya matambiko au ibada kama vile mapango, misitu, miti, mito, milima na mandhari iliyoteuliwa na jamii kwa madhumuni ya ibada; na kumbukumbu za matukio muhimu ya kihistoria, yakiwemo ya viongozi na mashujaa. Pia, Sheria ya Mambo ya Kale sura 333 ya mwaka 2002 sehemu ya pili kifungu cha tatu (3) Waziri mwenye dhamana ya Idara ya Mambo ya Kale anaruhusiwa kulitangaza eneo kuhifadhiwa chini ya Mambo ya Kale kutokana na sifa au umuhimu wake hata kama haijafikisha miaka 100. Tafiti za malikale zilizofanyika hapa nchini zilianza mwaka 1909 hadi leo na zimechangia sehemu kubwa katika chimbuko la wanyama mbalimbali na binadamu kuanzia maisha au mazingira aliyokuwa anaishi, vyakula alivyokuwa anakula, majenzi au majengo aliyojenga, zana na vyombo alivyokuwa akitumia. Matokeo ya Tafiti hizo yamewezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi ambazo zina utajiri mkubwa wa Malikale ambao baadhi kwa umaarufu wake umeweza kuitambulisha nchi yetu ndani na nje ya nchi. Mfano utafiti wa masalia ya mijusi mikubwa (dinosaria) yalichimbuliwa kutoka Tendaguru Lindi kuanzia mwaka 1909 hadi 1913 yenye miaka millioni 150 iliyopita. Utafiti huu ulifanyika baada ya Mjerumani

v mhandisi kugundua Masalia ya Mjusi Mkubwa mwaka 1906, huko Tendaguru Mkoani Lindi. Masalia hayo yalipelekea Makumbusho ya “Natural History” ya Ujermani kuja kufanya utafiti zaidi mwaka 1909 hadi 1913 (Heinrich, W., et all; 2011). Watafiti wengine kama Louis Leakey na Mary Leakey wataalamu wa akiolojia walipata umaarufu kutokana na uvumbuzi wa masalia ya binadamu wa kale ambayo ni vielelezo vya Chimbuko la binadamu katika bonde la Olduvai yanayoonyesha kugunduliwa kwa zamadamu wanne: Australopithecus boisei au Zinjanthropus boisie lililogunduliwa na Dkt. Mary Leakey na mumewe Dkt. Louis Leakey mwaka 1959, Homo Habilis aligunduliwa Mei 1960 Olduvai na Jonathan leakey mtoto wake leakey, ambaye inasadikika kuwa alitengeneza zana za Mawe Olduvai ziitwazo “Oldwan”, Homo erectus aligunduliwa Olduvai Desemba 1960 na Dkt. Mary Leakey na Homo sapiens sapiens. Aidha, Utafiti uliofanyika Laetoli mwaka 1978 uligundua nyayo za zamadamu wengine wa spishi ya “Australopithecus afarensis”, pamoja na za wanyama na ndege mbalimbali walioishi miaka milioni 3.6 iliyopita, zilizogunduliwa na Dkt.Mary Leakey mwaka 1976 katika Bonde la Oldupai na Laetoli, Arusha. Aidha, Tanzania kumefanyika tafiti nyingi za michoro ya miambani ambazo zimeonyesha uwezo wa binadamu kufikiri na kutunza kumbu kumbu kwa kutumia michoro kabla ya ugunduzi wa maandishi hadi sasa tunatumia Komputa. Michoro ya miambani Tanzania imegunduliwa Kondoa, Dodoma; Iramba, Singida; Iringa, Kagera, Arusha na Manyara. Hii ilikuwa njia ya kutunza kumbukumbu na mawasiliano. Wataalam wengine wa Mambo ya Kale wamefanya utafiti kwenye zana zilizotumika zamani kuanzia zana za Mawe kama Olduwan za Olduvai, Achelean huko Isimila na ufuaji na utengenezaji wa zana za Chuma uliofanyika katika mikoa mingi hapa Tanzania mfano Rukwa, Katavi, Kagera, Songwe na ukanda wa nyanda za juu kusini. Majengo ya kihistoria ni miongoni mwa maeneo yaliyofanyiwa utafiti na ikagundulika kuna magofu ya majumba ya kale na makaburi yaliyojengwa kwa matumbawe kuanzia karne ya nane na tisa hadi kumi na mbili katika sehemu kadhaa za pwani, kama vile Mkoa wa Tanga; Mkoa wa Pwani; Mkoa wa Dar es salaam; Mkoa wa Lindi na Mtwara. Maeneo mengine ni Kimondo, kilichopo kijiji cha Ndolezi, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe; visukuku vya kilimo cha umwagiliaji cha miaka zaidi ya mia tatu iliyopita vilivyopo Engaruka, Wilaya ya Monduli, Mkoa wa Arusha, na mengineyo mengi. Tafiti hizi za Malikale zilizofanyika katika Nchi ya Tanzania zimekuwa na umuhimu wa kipekee duniani kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta za kisayansi, kielimu, kiutamaduni na kiuchumi. Mchango wa malikale ni pamoja na: kutambulisha jamii; burudani; vituo vya elimu; vivutio vya utalii; vielelezo vya mabadiliko ya kihistoria, mazingira na chimbuko, maendeleo na uwezo wa binadamu hadi leo. Uhifadhi wa raslimali za malikale pia hujumuisha uhifadhi wa historia ya nchi yetu wakiwemo viongozi mbalimbali kuanzia machifu hadi Maraisi. Tanzania ni moja ya nchi za Afrika iliyokuwa na viongozi wenye sifa za kitaifa na kimataifa kwa umaahiri wao wa kupigania haki za binadamu kuanzia Machifu hadi Maraisi. Uhifadhi wa raslimali hizi za Malikale hauna budi kutekelezwa na kila mtu kwa sababu unamgusa kila mmoja kwa njia moja au nyingine na ni kumbukumbu kwa kizazi kijacho na Malikale hizi zikitumiwa ipasavyo zinaweza kuchangia pato la Taifa.

vi MUHTASARI Taarifa hii inaelezea kazi zilizotekelezwa na Idara ya Mambo ya Kale kuanzia 2015 hadi 2019 katika serikali ya awamu ya Tano. Katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano cha kufikia uchumi wa kati 2025 kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kuimarisha Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa katika mfumo wa muundo na utendaji. Lengo ni kuhahakikisha maeneo ya Mambo ya Kale yanaboreshwa na kutumika kama zao jipya la utalii ili kuongeza muda wa Watalii kukaa nchini, na kuchangia katika pato la Taifa na kuimarisha uhifadhi wa kumbukumbu hizi za Urithi wa Utamaduni. Katika mabadiliko hayo, Idara ya Mambo ya Kale imebaki na jukumu la kusimamia sera na sheria na kukabidhi baadhi ya majukumu ya kiutendaji au kiuendeshaji na uendelezaji Malikale kwa Shirika la Makumbusho. Vile vile Wizara iliangalia namna ya kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale vilivyo chini ya Wizara bila kuathiri uhalisia na historia yake kwa kutumia Taasisi za Wizara kama Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii alivyoeleza katika kikao cha Bunge la Mei 2018 wakati anawasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara ya mwaka 2018/2019. Sura ya Tano katika taarifa hii inaelezea hatua zote zilizochukuliwa kimaandishi za kukabidhi vituo vilivyo chini ya Wizara kwa Taasisi zilizo chini ya Wizara. Taasisi zilizokabidhiwa vituo hivyo tayari zimeshaanza kufanya tathimini ya namna ya kuvihifadhi mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) waliunda kikundi kazi walitembelea vituo vya Kimondo cha Mbozi, Songwe; Engaruka, Michoro ya Miambani Mumba na Engarasero ambayo ipo Mkoa wa Arusha na Mapango ya Amboni Tanga. Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) ilitembelea kituo cha kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni, Dar es Salaaam; kituo cha Caravan Serai, Bagamoyo na vituo vya Isimila na Kalenga Mkoani Iringa. Katika sura ya nne imeelezea mafanikio ya Idara katika kipindi hiki cha serikali awamu ya tano. Sura hii imeonyesha kazi zilizotekelezwa katika vituo vya Olduvai, Arusha; Kimondo cha Mbozi, Songwe; Mapango ya Amboni, Tanga; Makumbusho ya Nyumba ya Mwlimu Nyerere Magomeni, Dar es Salaam; Michoro ya Miambani Kolo, Kondoa; Makumbusho ya Mtwa Mkwawa Kalenga na Magofu ya Kunduchi, Dar es Salaam. Aidha, sura hii inalezea uanzishwaji wa Makumbusho Mpya ikiwemo Makumbusho ya Nyumba ya Rashidi Mfaume Kawawa. Taarifa hii pia imeonyesha historia ya Idara na majukumu yake, inafanya nini na imefanya nini. Katika sura ya kwanza hadi tatu imeonyesha Idara ilikoanzia, Sera, Sheria, Kanuni na miongozo iliyopo na inayotumika katika kusimamia, kutekeleza na kuongoza katika utendaji wa kazi za kila siku za Utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa Malikale; Muundo wa Idara; watumishi katika Idara ya Mambo ya Kale; aina za Malikale. Lengo ni kumwezesha mdau atakayesoma taarifa aelewe Idara ilikotoka, mahali ilipo, inakokwenda na majukumu yake. Mwisho taarifa hii inaonyesha Idara ilivyoshiriki katika utangazaji wa Malikale ndani na nje ya Nchi kwa kutumia machapisho, maonyesho au tamasha na vipindi vya television na ilivyoshirikisha jamii na wadau mbalimbali katika uhifadhi wa Malikale katika Serikali hii ya Awamu ya Tano kuanzia mwaka 2015 - 2019.

vii SHUKRANI

Awali ya yote Idara inampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa uongozi maahiri wenye maamuzi mahususi yanayokusudia kuboresha uchumi wa Taifa kufikia uchumi wa kati 2025 katika Serikali ya awamu ya Tano. Ameleta mabadiliko makubwa katika Taifa hili yanayoonekana ukianzia kwenye miundo mbinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, maji na umeme. Amefufua Shirika la ndege la Tanzania kwa kununua ndege mpya na ameimarisha utendaji wa watumishi katika serikali na mengineyo mengi. Shukrani za pekee ziende kwa Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. (Mb) kwa kutoa kipaumbele katika uhifadhi na uendelezaji wa Malikale. Lengo ni kuhahakikisha maeneo ya Mambo ya Kale yanaboreshwa na kutumika kama zao jipya la utalii ili kuongeza muda wa Watalii kukaa nchini. Vilevile Shukrani za pekee ziende kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii 2017 hadi 2018 Mheshimiwa (Mb) na Mheshimiwa Constantine Kanyasu (Mb) ambaye kwa sasa ndiye Naibu Waziri wa Maliasili kwa kazi nzuri ya walizofanya kwa Idara ya Mambo ya Kale. Shukrani za dhati ni kwa Katibu Mkuu Mstaafu “Major General” Gaudence Millanzi; Katibu Mkuu wa Sasa Prof. Adolf F. Mkenda, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Aloice Nzuki na viongozi wengine wa Wizara kwa umaahiri wao katika kusimamia maagizo ya Mh. Waziri ya kuendeleza Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa. Katibu Mkuu Mstaafu atakumbukwa kwa kutatua changamoto za kipindi kirefu kwa Idara ya Mambo ya Kale; Mfano, Kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga mgogoro ulianza 2014 hadi 2018 mwezi wa Tano Wizara ikiongozwa na Katibu Mkuu Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi na Mkoa ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Richard Kasesela na familia ya Mkwawa iliongozwa na Bw. Edmond Mkwawa. Maamuzi ya Kikao; Hiki ni kituo cha serikali na taratibu na sheria zizingatiwe. Nawapongeza Watumishi wa Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa kwa utendaji, ushirikiano na utulivu walionyesha katika Mabadiliko yaliyokuwa yanafanyika na uelewa mkubwa wa kukubali mabadiliko hayo. Tuendelee kufanya kazi kwa bidii ili mabadiliko haya yalete mchango chanya katika uhifadhi na uendelezaji wa Malikale ambayo yatatumika kwa elimu, kumbukumbu, utafiti na kuchangia pato la Taifa kiutalii. Shukurani nyingi kwa Uongozi wa Idara Wakurugenzi Wasaidizi Dkt. Fabian Kigadye, Bwana Tibaijuka Anthony na Bwana Anacleth Mwijage; Wakuu wa Vituo Kwa niaba ya Watumishi wote vituoni, ambao ni Bw, John Paresso, Bi Reinfrida Kapela, Bi. Siyawezi Hungo, Bw. Paul Ndahani, Bw. Mbaruku Salehe, Bw. Paul Nyelo, Bw. Jumanne Maburi, Bw. Jordan Erick, Bi. Mariam Mgusi, Bw. Ally Mbarouk, Bi. Neema Mbwana, Bw. Zuberi Mabie, Bw. , Bi. Nengai Nairouwa, Bw. Kelvin Ngowi, Bi Mercy Mbogerah, Bw. M. Ngoma. Maafisa wengine ni Dkt Bwasiri Emmanuel, Dkt. Christowaja Ntandu, Bw. William Mwita, Bw. Revacutus Bugumba, Bi Sikujua Ramadhani, Bw. Christognus Ngivingivi, Bi Frida Msongo, Bi Prisca Kirway, Bi Mwantum Haidari na Bi leila Mohamed. Asante kwa Bi Florida Munisi, Bi Zuena Mohamedi, Bi Labi Masalu kwa ushirikiano wanu wa karibu na Shukrani kwa madereva, maafisa utumishi, masjala, Wahasibu na watumishi wote kwa ushirikiano wenu kwa kipindi chote cha Uongozi wangu

Digna Faustin Tillya Kaimu Mkurugenzi Mambo ya Kale

viii SURA YA KWANZA UHIFADHI WA MALIKALE TANZANIA BARA 1.1 Utangulizi Sura hii inaelezea dhamana ya Idara ya Mambo ya Kale, historia ya Idara hii, Sera na Sheria zinazotumika katika kuteleza majukumu ya Idara ya Mambo ya Kale, Aina, Ubora na Umuhimu wa Malikale. 1.2 Historia ya Idara ya Mambo ya Kale Idara ya Mambo ya Kale ina dhamna ya kusimamia utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za Malikale zilizopo nchini kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho. Malikale ni rasilimali za urithi wa utamaduni zilizotengenezwa, zilizojengwa, zilizoundwa au zenye kuhusiana au kutumiwa na binadamu wakati wa maisha yake. Rasilimali hizi historia, ujuzi, mila na desturi za mababu au kizazi kilichopita. Rasilimali nyingi hurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kijacho. Kwa mujibu wa será ya Malikale ya mwaka 2008, Malikale hujumuisha rasilimali zinazoshikika, zinazohamishika na zisizohamishika na zinazopatikana juu na chini ya ardhi ambazo zinadhihirisha mabadiliko ya kimaumbile, kifikra, zana na mazingira aliyoishi na kutumia binadamu. Aidha, kuna Malikale ambazo kutokana na sifa au umuhimu wake kwa jamii husika na Taifa hata kama zina umri mdogo kuliko huo ulioainishwa na Sera na Sheria ya Mambo ya Kale, kulingana na sheria ya Malikale (Sura 333 ya Mwaka 2002) Waziri mwenye dhamana ana Mamlaka ya kuzitangaza kuwa Urithi wa Taifa (National Heritage). Uhifadhi wa Malikale ulianzia wakati wa Ukoloni mwaka 1937 ilipoanzishwa Sheria ya Uhifadhi wa Majengo ya Kihistoria (The Monument Preservation Ordinance, 1937). Wakati huo Serikali ya Kikoloni kupitia ofisi za Wakuu wa Wilaya ilijihusisha katika kutafuta na kuorodhesha kumbukumbu za kihistkoria hasa zilizohusiana na ukoloni katika maeneo ya mwambao. Mwaka 1956 Mambo ya Kale ilianzishwa na kuanza kufanya kazi rasmi mwaka 1957. Kitengo cha Mambo ya Kale kilipandishwa hadhi kwa kuanzishwa kwa Idara ya Mambo ya Kale Mwaka 2009 baada ya kuhamishiwa Wizara ya Maliasili na utalii mwaka 1999 kutoka Wizara ya Elimu na Utamaduni. Mwaka 1964, ilitungwa Sheria ya Mambo ya Kale Na. 10 ambayo ilifanyiwa marekebisho kwa Sheria Na. 22 ya mwaka 1979. Sheria ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 imeendelea kuwa sheria mama ya uhifadhi wa urithi wa utamaduni mpaka sasa (mwaka 2019) ingawa imefanyiwa maboresho madogo mwaka 2002 Sura 333. Tangu kuanzishwa kwake, Kitengo cha Mambo ya Kale kimekuwa kikihamishwa kutoka wizara moja hadi nyingine. Kitengo hiki kimehamishwa kwa takribani mara kumi na moja (11) mpaka mwaka 1999 kilipohamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii. Katika Wizara nyingine Kitengo kilikaa kwa muda mfupi sana jambo ambalo limeathiri sana kasi ya maendeleo ya uhifadhi wa Malikale. Ifuatayo ni Orodha ya Wizara ambazo Idara imezipitia na vipindi husika: 1957 – 1962 Wizara ya Elimu; 1962 – 1964 Wizara ya Utamaduni na Vijana; 1964 – 1967 Ofisi ya Rais; 1967 – 1968 Wizara ya Tawala za Mikoa na Maendeleo ya Vijiji; 1968 – 1980 Wizara ya Elimu ya Taifa; 1980 – 1984 Wizara ya Habari na Utamaduni;

1 1984 – 1985 Ofisi ya Waziri Mkuu; 1985 – 1988 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Utamaduni, Vijana na Michezo; 1988 – 1990 Wizara ya Utumishi wa Umma, Ustawi wa Jamii; 1990 – 1999 Wizara ya Elimu na Utamaduni; na, 1999 – 2019 Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa kipindi chote cha kuhamahama Kitengo na baadaye Idara ya Mambo ya Kale majukumu yake yalitekelezwa kwa kuzingatia Sheria ya Mambo ya Kale Na. 10 ya mwaka 1964 ambayo ilifanyiwa marekebisho kwa Sheria Na. 22 ya mwaka 1979 na sura 333 ya mwaka 2002. Hivyo maeneo ya Malikale yalibakia na uhalisia wake bila ya kubadilishwa. Baada ya Kitengo hiki kuhamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii maeneo haya yalianza kuendelezwa kiutalii kwa kuzingatia Sera ya Malikale iliyoanzishwa mwaka 2008. Pia, Muundo wa Kitengo cha Mambo ya Kale ulibadilishwa na kuundwa Idara ya Mambo ya Kale mwaka 2009 kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa majukumu ya utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa Maeneo ya Malikale bila kuathiri uhalisia. Lengo la Sera ya Malikale ya mwaka 2008 ni uhifadhi endelevu wa kuhifadhi na kuendeleza malikale kwa kuhusisha wadau mbalimbali. Sera hii inatoa fursa kwa kila Mtanzania kuwajibika katika suala zima la uhifadhi na uendelezaji wa Malikale. Hivyo, utekelezaji wa Sera ya malikale ya 2008 hauna budi kushirikisha Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali, Sekta Binafsi, Jamii, Jumuiya za Kikanda na Kimataifa na Mawakala wa Serikali na vyombo vingine vya dola. Katika kutekeleza uhifadhi wa Malikale, Maeneo yaliyohifadhiwa na Wizara chini ya Idara ya Mambo ya Kale ni 18 ambayo ni Olduvai Gorge na Nyayo za Zamadamu Laetoli Ngorongoro; Magofu ya Kaole, Mji Mkongwe wa Bagamoyo na Makumbusho ya Caravan Serai, Bagamoyo; Michoro ya Miambani Kolo, Kondoa; Makumbusho ya Mtwa Mkwawa Kalenga na Muhula wa Zama za Mawe Isimila, Iringa; Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, Lindi; Kimondo cha Mbozi, Songwe; Mapango ya Amboni na Magofu ya Tongoni, Tanga; Makumbusho ya Kumbukizi ya Dkt Livingstone Ujiji, Kigoma; Tembe la Dkt. Livingstone Kwihara, ; Makumbusho ya Nyumba ya Mwl. Nyerere Magomeni, Dar es Salaam na Magofu ya Kunduchi, Dar es Salaam; (Kiambatisho Na.1). Maeneo haya yana sifa za kipekee za kitaifa na kimataifa na yanatumika kiutalii na kielimu yana watumishi na huduma nyingine za kiutalii na kiuhifadhi. Maeneo ya Malikale Tanzania ni mengi na kutokana na tafiti zilizofanyika ni zaidi ya 500, kila Mkoa una maeneo ya Malikale na mengi yapo kwa watu binafsi au Taasisi binafsi. 1.3 Sera, Sheria na Miongozo inayotumika kwenye Uhifadhi wa Malikale Idara ya Mambo ya Kale katika utendaji wa kila siku inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 ya mwaka 2002, Sheria ya Makumbusho Na.7 ya mwaka 1980 na Sheria ya Nyaraka za Taifa Na. 3 ya mwaka 2002. Sheria nyingine ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 (Kifungu namba 9 (c)), Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1999. Aidha, Idara hutumia Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (5) 2016/2017 – 2020/2021, Ilani ya Uchaguzi ya ya 2015-2020, Maelekezo ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 11, Mpango Mkakati wa Wizara (2016/17 – 2020/21) katika kuteleza majukumu ya Wizara.

2 Madaraka makubwa ya kisheria amepewa Waziri mwenye dhamana ya Malikale akifuatiwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Kale, Serikali za Mitaa na Halmashauri. Sheria ya Malikale kwa kiasi kikubwa imetokana na Sheria ya kikoloni ya mwaka 1937 “The Monuments Preservation Ordinance” ambapo kwa kipindi hicho kipaumbele kwenye Malikale ilikuwa ni uhifadhi na utafiti tu. Mwaka 2008 Sera ya Malikale ilianzishwa kwa ajili ya kuboresha uhifadhi uliokuwa sio endelevu kuwa uhifadhi endelevu wa malikale. Lengo la sera hii ni kuongeza uelewa kwa jamii na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa Malikale na manufaa yake kiuhifadhi, kielimu, kiutalii ili wananchi waweze kutumia malikale hizo kujiongezea kipato. Sera hii hufafanua dhima na malengo ya malikale, kuainisha jinsi shughuli za malikale zitakavyoendeshwa na kusimamiwa, husisitiza umuhimu wa kutafiti na kuhifadhi malikale pamoja na kufafanua jinsi wadau mbalimbali ikiwamo serikali na taasisi zake, sekta binafsi na umma kiujumla watakavyoshirikishwa katika shughuli za uhifadhi wa malikale. kuzitumia kujiamini na kujivunia utaifa wao 1.4 Aina, Ubora na Umuhimu wa Malikale, Tanzania 1.4.1 Raslimali za Malikale Idara ya Mambo ya Kale ndiyo yenye dhamana ya kutafiti, kuhifadhi na kuendeleza raslimali za malikale Tanzania Bara. Utekelezaji wa majukumu ya Idara ya Mambo ya Kale Tanzania ni kwa mujibu wa sheria ya Mambo ya Kale ya Mwaka 2002 Sura 333, ambapo Malikale baada ya kufanyiwa utafiti na kuonekana ina vigezo vyote vinavyostahili huhifadhiwa kitaalam. Vigezo hivyo ni pamoja na uwepo wa malikale au vitu halisi vyenye historia au taarifa sahihi, vitu vyenye umri wa miaka mia au zaidi. Malikale zinazopatikana kwenye utafiti ni aina mbili; zinazohamishika na zisizohamishika. Malikale zisizohamishika hujumuisha Mazingira/maeneo aliyokuwa akiishi binadamu wa kale ambayo kupitia tafiti za Mambo ya Kale kumepatikana viashiria au masalia ya binadamu wa kale kama vile mifupa au zana alizokuwa akitumia kwa kuwinda, vitu au vyombo alivyotengeneza kwa ajili ya kupika chakula na kulia, vyakula alivyokuwa akitumia Mizizi, Miti, matunda na Wanyama na kadhalika. Malikale pia hujumuisha nyumba alizokuwa akijenga, nguo alizokuwa akitengeneza, Moto n.k. Malikale hizi baada ya kufanyika kwa tafiti za Mambo ya Kale kwa kuzingatia sheria na kanuni za Mambo ya Kale huhifadhiwa aidha kwenye eneo lililovumbuliwa au lilikopatikana Malikale hizo au kuhamishiwa Makumbusho au kituo cha taarifa kwa zile ambazo zinahamishika. Kutokana na tafiti hizo Tanzania inayo hazina kubwa yenye maeneo ya Malikale ambayo yapo katika makundi yafuatayo:- 1) Maeneo yenye masalia ya Paleontolojia na akiolojia, hii inajumuisha masalia ya vitu mfu vya kale vya zaidi ya miaka mia, maelfu hadi milioni iliyopita. Baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Bonde la Olduvai na Laetoli (Arusha), Bonde la Ruhuhu (Ruvuma), Shingo Pana Songwe, Tendaguru (Lindi) na Isimila (Iringa); 2) Magofu yenye hadhi ya kihistoria ambayo yamefikisha miaka iliyotajwa kwenye sheria na yenye sifa za kipekee. Baadhi ya magofu hayo ni kama yale ya Kaole na Bagamoyo (Pwani); Kilwa Kisiwani na Songo Mnara (Lindi); Magofu ya Tongoni na Pangani, (Tanga); na Magofu ya Kunduchi (Dar es Salaam); 3) Miji ya kihistoria: Hii ni miji iliyokuwepo zamani inayodhihirisha maendeleo ya mtanzania kabla na baada ya ujio wa wakoloni hadi sasa, kwa mfano mji wa: Bagamoyo (Pwani), Kilwa Kisiwani, Songo Mnara, Sanje kati (Lindi), Pangani (Tanga) na Mikindani (Mtwara);

3 4) Makazi ya kijadi haya ni mengi yapo katika Mikoa yote na yangestahili kila Mkoa kupewa jukumu la kuweka Kutunza Mfano Kalenga (Iringa) na Bweranyange (Kagera), Ruvuma, Tabora, Mwanza, Kilimanjaro n.k.; 5) Makazi, Nyumba na Makumbusho za Maasisi wetu Mfano Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere, Hayati Amri Abedi Amani Karume na Hayati Rashidi Mfaume Kawawa; 6) Maeneo yenye kumbukumbu za harakati za ukombozi wa bara la Afrika kama vile Jengo lilikuwa Ofisi ya Kamati ya Ukombozi wa Bara la Afrika Mtaa wa Ghana Jijini Dar es Salaam; Makambi ya Wapigania uhuru kusini mwa Afrika, ambayo yapo katika Mikoa mingi hapa nchini Mfano Mazimbu na Dakawa Morogoro na Kongwa Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma; 7) Majengo ya kihistoria ya muda mrefu na yenye hadhi ya kipekee yaliyojengwa nyakati mbalimbali. Haya ni majengo yaliyojengwa wakati wa ujio wa Wajerumani, Waingereza na Waarabu katika nchi yetu; 8) Maeneo yenye matukio au kumbukumbu maalum za kihistoria yaliyoainishwa kisheria, kwa mfano makaburi ya wakoloni, makaburi au masalia ya vita mbalimbali ikiwemo vita ya Kwanza na ya Pili ya Dunia, Minara na kuta zenye kumbukumbu au matukio ya kihistoria kama vita ya Kagera-Songea, vita vya Majimaji mfano Makumbusho ya majimaji Songea, Azimio la Arusha; 9) Maumbile asilia yenye historia au umaarufu kwa mfano Kimondo cha Mbozi (Mbeya), na Mapango ya Amboni (Tanga) ambayo yanatumika kwa shughuli za mila na desturi; 10) Michoro ya Miambani yenye kuonyesha mazingira binadamu aliyoishi na wanyama waliokuwepo, Mfano maeneo ya Kolo na SwagaSwaga-Kondoa; 11) Maeneo yaliyokuwa yanatumiwa na jamii kwa huduma mbalimbali mfano hospitali zenye historia, Shule alizosoma au kufundisha Baba wa Taifa na barabara, mitaa viwanja vyenye kumbukumbu ya kihistoria mfano Kiwanja cha Karimjee mahali paliposhushwa bendera ya Mwingereza na kupandishwa bendera ya Tanzania; na 12) Makumbusho mbalimbali zinazojumisha Makumbusho za serikali mfano Makumbusho ya Taifa, Makumbusho za binafsi Mikindani Mtwara; Urithi, Tanga na Makumbusho za dini mfano Makumbusho ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na Bujora Mwanza. Makumbusho hizi hutumika kwa ajili ya kutunza na kuhifadhi wa Malikale zinazohamishika kwa ajili ya utafiti kumbukumbu, maonyesho, machapisho, na kuelimisha umma kuhusu kuendeleza urithi wa utamaduni kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho. 13) Makumbusho au nyumba za Waasisi wa Taifa mfano Baba wa Taifa Mwalimu Butiama (Mara) na Magomeni(Dar es Salaam), Hayati abedi Amani Karume, (Zanzibar) na Hayati Rashid Mfaume Kawawa. 14) Maeneo au majengo ya kuabudia ya jamii mbalimbali kuanzia dini za mababu zetu hadi dini zilizoingia kutoka nje ya nchi za Kikristu na Kiislam.

4 1.4.2 Umuhimu/Thamani ya Raslimali za Malikale, Tanzania Tanzania na Duniani kote walikuwa wanaenzi na kuhifadhi vitu vya kale vilivyokuwa vimeipatia umuhimu au sifa fulani kutokana na mchango wake katika jamii husika na hurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Malikale hizi zikitumika ipasavyo hutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya wananchi na serikali. Umuhimu na faida ya Malikale katika jamii ni; 1.4.2.1 Kumbukumbu kwa kizazi kijacho Malikale nyingi zimetengenezwa na binadamu, na kwa maana hiyo kuna teknolojia iliyotumika au iliyobuniwa. Kwa hiyo zinapohifadhiwa husaidia kuthibitisha na kuonesha chimbuko la teknolojia na ustaarabu wa binadamu. Kizazi kinachokuja hupata historia ya kizazi kilichopita kwa kupitia Malikale zilizohifadhiwa vizuri na kujua maisha waliyokuwa wanaishi mababu na mababu. Uhifadhi wa kumbukumbu hizi ni muhimu na hurithishwa kwa kizazi kinachofuata na kwa wale wenye vipaji na ubunifu hutumia kumbukumbu hizi sambamba na zile za kisasa na hivyo kupanua wigo wa uwezo wetu wa kuyatawala na kuyatumia mazingira kwa njia endelevu. 1.4.2.2 Malikale ni utambulisho wa Taifa Malikale ni kitambulisho cha ukoo, kabila na taifa husika. Tanzania inazo Malikale nyingi muhimu zenye sifa za kitaifa na kimataifa. Baadhi yake zimeitambulisha na kuitangaza nchi yetu nje ya mipaka yake. Mifano halisi ni Masalia ya Mjusi aliyepatikana Tendaguru Lindi miaka millioni 150 iliyopita, fuvu la zamadamu aliyeishi miaka milioni 1.75 iliyopita lililogunduliwa mwaka 1959 katika Bonde la Oldupai, na nyayo za zamadamu aliyeishi miaka milioni 3.6 zilizogundulika miaka katika eneo la Laetoli, ni nyayo ambazo zinaonyeha binadamu kipindi hicho alikuwa anatembea kwa miguu miwili. Mifano mingine ni Michoro ya miambani ambayo inapatikana katika maeneo mengi Tanzania mfano Kolo Kondoa. 1.4.2.3 Elimu kwa vizazi vijavyo Malikale ni moja kati ya nyenzo muhimu katika kuwaelimisha watu au jamii juu ya historia na utamaduni wao. Huonyesha historia na mabadiliko ya binadamu kimaumbile kutoka kwenye miili mikubwa kama ya Dinosaria mpaka maumbile ya sasa hivi, huonyesha chimbuko na maendeleo ya Binadamu maisha aliyokuwa akiishi na zana alizokuwa akitumia mfano mapango kabla ya kujenga nyumba hadi leo ambapo kuna aina mbali za ujenzi wa nyumba, zana za mawe kabla ya ugunduzi wa chuma hadi silaha za Chuma, Utengenezaji au uundaji wa vyombo mbalimbali magari au baiskeli za miti hadi sasa kuna magari, ndege n.k. Malikale huonyesha uwezo wa binadamu kufikiri na kutunza kumbukumbu kabla ya ugunduzi wa maandishi mfano Michoro ya miambani Kondoa hadi sasa tunatumia Komputa. Utunzaji wa hazina hii ni muhimu kuwawezesha vizazi vijavyo kuona vitu halisi vitokanavyo na urithi wa utamaduni. Zaidi ya hayo, malikale huwawezesha watu kutambua na kuthamini utu wao, historia yao na utamaduni wao. Kumbukumbu hizi zikitunzwa vizuri zitaelimisha umma kwa kuwaonyesha walikotoka na kuona umuhimu wa kuutunza, kuuendeleza na kurithishana urithi huu kwa manufaa ya elimu kwa kizazi kilichopo na kijacho. 1.4.2.4 Malikale chanzo cha mapato Malikale ni kitegauchumi muhimu sana kinapotunzwa na kuendelezwa bila kuathiri uhalisia wake, ni kivutio kizuri cha watalii. Nchi nyingi duniani hupata mapato makubwa kutokana na utalii unaotegemea vivutio vya malikale. Utalii huchangia na kuongeza pato la serikali na la wananchi wanapofanya kazi katika sekta ya Malikale ama wanapouza bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwa watalii.

5 Wizara kupitia Idara ya Malikale na katika kutekeleza Sera ya Malikale 2008 na kwa mujibu wa sheria ya Mambo ya Kale sura 333 ya 2002 imeboresha na kuanza kukukusanya mapato kupitia vyanzo vifuatavyo: 1) Viingilio Haya ni mapato yatokanayo na viingilio wanavyotozwa wageni watembeleao maeneo ya Mambo ya Kale pamoja na makumbusho. 2) Ada za utafiti Haya ni mapato yatokanayo na ada zinazotozwa kwa watafiti wafanyao tafaiti mbalimbali za Mambo ya Kale nchini. Watafiti hawa wanaweza kuwa wa ndani na wa nje ya nchi. Idara inatoza 5% ya ghrama za utafiti kama inavyoonekana katiaka sheria ya Mambo ya Kale 3) Mrabaha Haya ni mapato yatokanayo na uwekezaji katika rasilimali za Malikale kama vile, majengo ya kihistoria na mikusanyo inayotumiwa na watafiti mbalimbali hususani ile iliyohifadhiwa nje ya nchi. Kwa sasa Idara inapata mrahaba mmoja tu utokanao na Mkataba (MoU) iliyoingiwa na Idara ya Mambo ya Kale NCAA ambapo Mamlaka ya Hifadhi ya NCAA inakusanya mapato yote ya Oldupai nusu ya mapato yanayopatikana hupewa Idara na yanayobakia hutumika kuendeshea kituo cha Oldupai. 4) Michango ya Wahisani wa Maendeleo (Grant) Idara hupata mapato yanayotokana misaada mbalimbali. Idara inatekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wakiwemo Washirika wa Maendeleo kwa lengo la kuhakikisha kuwa raslimali Malikale zinahifadhiwa kwa lengo la kuziongezea muda wa uwepo wake. Hivyo Idara huandika miradi mbalimbali itakayosaidia katika uhifadhi na uendelezaji wa Malikale zilizo chini ya Wizara. 5) Makusanyo ya mapato Mapato yote yanatokana na rasilimali za Malikale na kupitia vyanzo vilivyotajwa hapo juu yanakusanywa katika Mfuko wa Taifa wa Mambo ya Kale. Mfuko huu umeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya Mambo ya Kale Na. 22 ya mwaka 1979, kifungu kidogo cha 19B (au Sura 333 kifungu 22). Kifungu hiki kimeainisha vyanzo vya mapato ya mfuko huu na kuwa yanatumika kwa ajili ya Utafiti, uhifadhi na uendelezaji wa Raslimali za Malikale. Katika kusimamia makusanyo ya Mfuko wa Mambo ya Kale, kanuni huandaliwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maduhuli kwenye vituo vya Mambo ya Kale ambazo huboreshwa mara kwa mara ili kuendana na wakati na mazingira. Kanuni inayotumika kwa sasa ni kanuni Na. 497 ya mwaka 2014 (the Antiquities user fees rules, 2014). Lifuatalo ni jedwali na 1 linaloonyesha Mapato na wageni 2006 / 2007 hadi 2017 / 2018. Jedewali Namba 1. Mapato na wageni 2006/2007 hadi 2017/2018

Mwaka Wageni Mapato 2006/2007 95,265 236,666,079 2007/2008 120,919 266,241,803 2008/2009 102,528 216,507,549

6 2009/2010 103,777 212,867,609 2010/2011 161,666 231,825,095 2011/2012 125,490 516,496,180 2012/2013 214,214 1,321,340,797 2013/2014 154,930 1,124,559,323 2014/2015 107,334 1,023,860,957 2015/2016 110,500 1,308,080,760 2016/2017 118,566 1,824,538,604 2017/2018 128,268 2,213,388,590

Ongezeko la maduhuli kuanzia 2016 hadi 2018 limetokana na kuboreshwa kwa baadhi ya vituo kwa kuviendeleza na kuboresha miundombinu ikiwemo maji, umeme na ujenzi wa vituo vya taarifa na kumbukumbu katika vituo vifuatavyo; Makumbusho ya Kumbukizi ya Dkt. Livingstone, Ujiji mwaka 2006; Makumbusho ya muhula wa mawe, Isimila mwaka 2006; Michoro ya Miambani na kuiweka kwenye Orodha ya urithi wa Dunia mwaka 2006; Kukamilika kwa Ukarabati, Uboreshaji na kuzinduliwa kwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa ufadhili wa Serikali ya Sweden; Ukarabati, Uimarishaji na Uendelezaji wa Tembe la Kwihara, Tabora mwaka 2014; Kukarabati majengo katika Makumbusho ya Kalenga mwaka 2014 na kuimarisha mipaka ya kituo hicho mwaka 2018; Kujenga Makumbusho mpya Olduvai iliyofunguliwa tarehe 03 Octoba 2017 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Arusha; Kujenga jengo jipya la ofisi na kutoa taarifa Mbozi, Songwe na Mwisho Wizara iliboresha mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli ambao umesaidia mapato kupanda. Kwa ujumla haya ndio yaliyosababisha maduhuli kuongezeka kutoka 236,666,079 mwaka 2006/2007 hadi 2,213,388,590 mwaka 2017/2018. Fedha zinakusanywa hutumika kwa Utafiti, uhifadhi, uendelezaji na kuendesha vituo ikiwa ni pamoja na ukarabati wa majengo na majenzi ya kihistoria ulinzi, usafi, na utangazaji. Mwanzoni kabla ya Idara kuhamia Maliasili na Utalii vituo hivi kipaumbele ilikuwa kuhifadhi Malikale kwa kumbukumbu, Elimu na Utafiti na ukusanyaji wa maduhuli au mapato haukuwa kipaumbele. Makusanyo rasmi yameanza baada ya Idara kuhamia Wizara ya Maliasili na utalii na kuendelezwa kiutalii. Kwa miaka 12 iliyopita kuanzia 2006 hadi 2018 mapato yameongezeka kutoka 236,666,079 hadi 2,213,388,590. Hii inadhihirisha wazi kuwa vivutio vya Malikale vikitunzwa na kutangazwa vizuri vinaweza kutoa mchango mzuri katika Taifa kielimu na kiuchumi.

7 SURA YA PILI

MAJUKUMU, MUUNDO NA WATUMISHI WA IDARA YA MAMBO YA KALE

2.1 Utangulizi Sura hii inawasilisha majukumu ya Idara kuanzia kwa Mkurugenzi hadi kwa Wakurugenzi Wasaidizi na mabadiliko yaliyokuwa yakifanyika kimuundo kuanzia 2009 hadi 2019. Vilevile sura hii inaelezea watumishi wanaotakiwa kuajiriwa katika sekta hii ya Malikale, mafunzo, mfanyakazi bora na uteuzi wa watumishi wa Idara katika kushika vyeo vya Taifa na Wizara na Tanzania na imeonyesha vituo 18 ambavyo vinasimamiwa na Wizara yenye dhamana kupitia Idara ya Mambo ya Kale 2.2 Majukumu ya Idara Jukumu kubwa la Idara ni utafiti, uhifadhi na kuendeleza urithi huo wa Malikale kwa kuzingatia Sera na Sheria. Kwa ujumla katika kufanikisha utendaji Idara inatekeleza majukumu yafuatayo kwa mujibu wa muundo 2009 na maboresho ya 2018: 2.2.1 Kuandaa na kurekebisha na kusimamia utekelezaji Sera, Sheria na kanuni za Malikale; 2.2.2 Kusimamia na kuhakikisha kuwa uhifadhi na ulinzi stahili wa Malikale unafanyika; 2.2.3 Kusimamia na kuratibu tafiti za Malikale Tanzania Bara; 2.2.4 Kuhamasisha matumizi endelevu ya Malikale kama vivutio vya utalii na vituo vya mafunzo; 2.2.5 Kuhuisha na kusimamia mikataba ya kimataifa ambayo serikali imerithia inayohusiana na Uhifadhi wa Malikale mfano UNESCO; 2.2.6 Kushirikiana na jamii, watu binafsi, mashirika na taasisi za binafsi na serikali ikiwemo Makumbusho ya Taifa katika kulinda na kuendeleza rasilimalikale za Taifa na kutoa ushauri wa kitalaam kwa wadau mbalimbali wa Malikale. 2.3 Muundo wa Idara ya Mambo ya Kale Kwa miaka Idara ya Mambo ya Kale ilikuwa kama kitengo chini ya Mkurugezi mmoja mpaka mwaka 2009 ambapo muundo wa Kitengo ulibadilishwa na kuwa Idara kamili ya Mambo ya Kale yenye Mkurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi watatu. 2.3.1 Muundo wa Idara kuanzia mwaka 2009 Muundo wa Wizara uliopitishwa na serikali awamu ya nne mwaka 2009 ndio uliobadilisha Mambo ya Kale kutoka kwenye kitengo kwenda Idara kamili na kulikuwa na maboresho madogo mwaka 2013 wizara. Katika Muundo huo wa mwaka 2009 na 2013 idara iliongozwa na Mkurugenzi na iligawanyika katika sehemu kuu tatu zinazoongozwa na Wakurugenzi wasaidizi kama ifuatavyo:

8 2.3.1.1 Sehemu ya utafiti, Mafunzo na Takwimu; 2.3.1.2 Sehemu ya Uhifadhi na Ufundi na; 2.3.1.3 Sehemu ya Undelezaji wa Urithi wa Utamaduni Kazi zilizotekelezwa na Sehemu za Idara 2009 hadi 2018 Idara kwa Muundo wa mwaka 2009 hadi 2018 ilikuwa na sehemu tatu zenye Wakurugenzi Wasaidaizi kama zilivyoainishwa katika kifungu 2.3.1 na yafuatayo ni majukumu ya kila Sehemu: 2.3.2 Sehemu ya Uhifadhi na Ufundi. 2.3.2.1 Kusimamia na kuratibu Uhifadhi na Ufundi wa Urithi wa Utamaduni na majengo, Miji na maeneo ya akiolojia; 2.3.2.2 Kuandaa miongozo na kusimamia Uhifadhi na usimamizi wa Urithi wa Utamaduni; 2.3.2.3 Kuainisha na kuchambua miradi ya ukarabati na uendelezaji wa Majengo au Miji, Minara na maeneo ya kiakiolojia. 2.3.2.4 Kutoa idhini ya ukarabati na uendelezaji wa maeneo ya kihistoria, maeneo ya hifadhi ya Kihistoria na kiakiolojia. 2.3.2.5 Kutoa idhini ya ukarabati au uendelezaji wa maeneo ya kihistoria; 2.3.2.6 Kuandaa, kuratibu na kusimamia utayarishaji wa mipango ya usimamizi ya maeneo ya Urithi wa utamaduni, na: 2.3.2.7 Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa mipango ya usimamizi ya maeneo/ vituo vya Mambo ya Kale. 2.3.3 Sehemu ya Maendeleo ya Urithi wa Utamaduni na Mawasiliano. 2.3.3.1 Kuhamasisha Utalii katika maeneo ya Urithi wa Utamaduni; 2.3.3.2 Kuratibu, kuandaa kutathimini na kufanya maboresho kwenye Kanuni, miongozo na Viwango. 2.3.3.3 Kuandaa, kutathimini na kufanya maboresho kwenye Kanuni, miongozo na viwango. 2.3.3.4 Kuandaa mpango au mkakati wa kuhamasisha Utalii katika maeneo Urithi wa Utamaduni. 2.3.3.5 Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mifumo wa kutoa habari. 2.3.3.6 Kuandaa na kusimamia mifumo bora ya ukusanyaji maduhuli na mipango ya matumizi ya Idara. 2.3.3.7 Kuelimisha jamii, wageni, shule, watoto, watafiti kuhusu urithi wa utamaduni. 2.3.3.8 Kuratibu Ushirikiano wa Kitaifa, kikanda na Kimataifa.

9 2.3.4 Sehemu ya Utafiti, Mafunzo na Takwimu 2.3.4.1 Kuainisha maeneo ya Utafiti, kupanga vipaumbele na kuratibu tafiti 2.3.4.2 zinazofanywa na Watafiti, Taasisi za utafiti katika Sekta ya malikale kutoka hapa nchini na nje ya nchi; 2.3.4.3 Kuandaa na Kuratibu Mpango wa Mapango Mafunzo wa Idara; 2.3.4.4 Kufanya na kuratibu kazi za Upembuzi Yakinifu wa Athari za Urithi wa Utamaduni katika Miradi mikubwa ya Maendeleo; 2.3.4.5 Kutathinini na kuchambua Mipango ya Utafiti; 2.3.4.6 Kufanya tafiti za Urithi na Utamaduni na kuwasilisha matokeo ya tafiti kwa 2.3.4.7 jamii au taasisi husika; 2.3.4.8 Kutoa vibali vya utafiti, uchimbaji, upigaji picha na kusafirisha nje ya nchi mikusanyo ya Urithi wa utamaduni; 2.3.4.9 Kuandaa na kusimamia “inventory” ya Urithi wa Utamaduni na maeneo ya Urithi wa Utamaduni hapa nchini; 2.3.4.10 Kuandaa miongozo na kusaidia kufanya tafiti , mafunzo ya uhifadhi na kutoa. Pamoja na sehemu hizo, Idara ina jumla ya vituo kumi na nane (18). Kwa mujibu wa muundo wa Idara, vituo vinasimamiwa na Sehemu ya Uhifadhi na Ufundi. Vituo vya Mambo ya Kale vimeorodheshwa kwenye Kiambatisho Na. 1. 2.4 Mabadiliko ya muundo 2018 hadi 2019 Kwa mujibu wa Muundo Mpya wa Wizara, Julai 2018, Wizara nzima ikiwemo Idara ya Mambo ya Kale sehemu ya Utafiti, Mafunzo na Takwimu katika Idara zote za Wizara zilihamishiwa katika Kitengo kipya kilichoundwa na Wizara cha Takwimu na Mafunzo. Hivyo Idara ya Mambo ya Kale ilibaki na sehemu mbili ambazo ni; 2.4..1 Sehemu ya Uhifadhi na Ufundi na; 2.4..2 Sehemu ya Undelezaji wa Urithi wa Utamaduni na Mawasiliano. Vilevile, Wizara ya Maliasili na Utalii katika hotuba ya bajeti ya Mwaka 2018/2019 ilielezea Bunge kuwa imeandaa mkakati wa kundeleza vituo vya Malikale vilivyopo Wizarani ikiwa ni pamoja na kuhamisha baadhi majukumu ya Mambo ya Kale kwenda Makumbusho ya Taifa na Idara ya Mambo ya Kale kubakia na majukumu ya Sera na Sheria. Maelekezo haya yametekelezwa na majukumu yanayohamishiwa Makumbusho ya Taifa ni: (i) Kuhifadhi, kuendeleza na kulinda maeneo ya malikale; (ii) Kuandaa na kutekeleza Mipango ya Usimamizi na Uendelezaji wa maeneo ya malikale; (iii) Kuanzisha na kuendesha mifumo ya datakanzi za malikale; (iv) Kuhamasisha uhifadhi wa malikale kwa kushirikisha Jamii; (v) Kuhamasisha utalii wa utamaduni; (vi) Kufanya utafiti wa malikale Tanzania Bara;

10 (vii) Kuanzisha makumbusho na vituo vya kumbukumbu na taarifa; (viii) Kuhamasisha matumizi endelevu ya malikale kama kumbukumbu za Taifa; vituo vya elimu na mafunzo; na vivutio vya utalii; na, (ix) Kuendeleza vivutio vya utalii wa malikale kwa viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa. 2.5 Majukumu yanayobaki Idara ya Mambo ya Kale Baada ya kuhamisha majukumu ya usimamizi wa vituo vya mambo ya kale kwenda Makumbusho ya Taifa, majukumu yanayopendekezwa kubaki Idara ya Mambo ya Kale ni kama ifuatavyo: i. Kuandaa, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uhifadhi, Utafiti na Uendelezaji wa Malikale; ii. Kuratibu na kurekebu uhifadhi, uendelezaji na ulinzi wa malikale; iii. Kuandaa Vigezo vya kutambua na kusimamia malikale katika ngazi mbali mbali; iv. Kuandaa Vigezo vya kuanzisha makumbusho na vituo vya kumbukumbu na taarifa; v. Kuandaa Orodha ya Maeneo ya Mambo ya kale; vi. Kuweka vigezo na kuratibu uhamasishaji utalii wa urithi wa utamaduni; vii. Kuanzisha, kusimamia, kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa unaohusu masuala ya malikale na makumbusho. Muundo huu bado unafanyiwa kazi na Wizara na baadaye utapelekwa utumishi kwa ajili ya kuthibitishwa. Vilevile Sheria za Idara ya Mambo ya Kale na Shirika la Makumbusho ya Taifa hazina budi kubadilishwa ili kuendana na mabadiliko yaliyofanyika ambapo Makumbusho waweza kutekeleza majukumu waliyoongezewa na Idara ya Mambo ya Kale, kubaki na majukumu ya kisheria na kisera. 2.6 Watumishi wa Idara ya Mambo ya Kale na Viongozi 2.6.1 Watumishi wa Idara Idara ina vituo kumi na nane (18- ikijumuisha Olduvai na Laetoli ambapo Idara imeingia mkataba na Mamlaka ya Ngorongoro- NCAA ) vyenye maeneo madogo na makubwa. Mfano Kilwa kuna visiwa viwili, Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambapo Kilwa Kisiwani ni Kilomita za Mraba 32 na Songo Mnara Kilomita za Mraba 50. Mapango ya Amboni Sq km 39.5, Michoro ya miambani maeneo yapo kwenye vijiji 13 na ukubwa ni Kilomita za Mraba 2230, (huu ni mfano wa vituo vikubwa ambapo kituo kimoja kinatakiwa kuwa na watumishi 8 hadi 10). Kwa vituo vidogo kituo kimoja kinahitaji watumishi wanne. Mmoja akiwa ni Mkuu wa Kituo, mmoja kupokea wageni na kukusanya maduhuli na mwingine kushughulikia uhifadhi na uendelezaji wa Kituo na mwingine utangazaji na utafiti. Maeneo makubwa kama Michoro ya Miambani Kondoa na magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara watumishi wanaohitajika ni kuanzia nane (8) hadi kumi. Hivyo jumla ya watumishi wanaotakiwa katika Idara ya Mambo ya Kale ni zaidi ya 200 kwa vituo vyote kumi na nane vilivyopo Wizara ya Maliasili na Utalii. Wakati huo huo kuna haja ya TAMISEMI na wadau mbalimbali kuhamasishwa kuajiri wataalam wa Mambo ya Kale watakaoshirikiana na Idara kuhifadhi na kuendeleza vivutio vya Malikale vilivyopo katika Tanzania nzima.

11 Idara mpaka Aprili 2019 watumishi 68 ambapo 50 vituoni na 18 Makao Makuu. Idadi hii ya Watumishi wamepungua ukilinganisha na mwaka 2015/2016 ambapo ilikuwa na watumishi 75, kwa sababu waliostaafu na kufariki hawakuajiriwa wengine. Kutokana na uhalisia wa maeneo ya Mambo ya Kale ikijumuisha kazi zilizopo na ukubwa wa maeneo watumishi waliopo ni wachache, wanaotakiwa ni zaidi ya 200. Idara ya Mambo ya Kale taaluma mbalimbali za uhifadhi, utafiti, Makumbusho na kuongoza wageni zinahitajika. 2.5.2 Viongozi wa Idara ya Mambo ya Kale kuanzia Kitengo hadi Idara kamili Idara ya Mambo ya Kale baada ya uhuru ilitunga sheria na kuwa na uongozi ambao ulisimamia majukumu ya utafiti na uhifadhi wa Mambo ya Kale. Ifuatayo ni orodha ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi waliongoza Idara kwa nyakati tofauti. 2.6.2.1 Wakurugenzi

1961-1968 - Neville Chittick 1968-1981 - Amini Aza Mturi 1981-1985 - S. Mongela 1985-1997 - Simon S.A.C. Waane 1997-2017 - Donatius K. Kamamba 2018-2019 - Digna Faustin Tillya 2.6.2.2 Wakurugenzi Wasadizi Idara baada ya kuwa Idara kamili mwaka 2009 Muundo uliopitishwa ulikuwa na Mkurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi watatu hadi 2017 mabadiliko ya muundo yalipofanyika katika Idara na kubakia na sehemu Mbili. Wakurugenzi Wasaidizi Walioteuliwa mwaka 2009 hadi sasa ni; 1) 2009-2012 Bwana Felix Ndunguru, Mkurugenzi MsaidiziUtafiti Takwimu na Mafunzo 2) 2009-2017 Bwana John Kimaro, Mkurugenzi Msaidizi Ufundi na Uhifadhi 3) 2009-2017 Bibi Digna Faustin. Tillya, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Urithi Utamaduni 4) 2015-2017 Bibi Eliwaa Maro, Mkurugenzi Msaidizi Utafiti Takwimu na Mafunzo 5) 2017-2019 Dkt Fabian Kigadye Mkurugenzi Msaidizi Ufundi na Uhifadhi 6) 2017-2018 Bwana Anthony Tibaijuka,Mkurugezi Msaidizi Utafiti Takwimu na Mafunzo(sehemu imehamishwa) 7) 2017-2018 Bwana Anacleth Mwijage, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Urithi wa Utamaduni 2.6.3 Mafunzo au uendelezaji wa Watumishi wa Idara Idara ya Mambo ya Kale ni moja ya Idara ambazo ni mtambuka. Kutokana na majukumu ya kazi Idara huhitaji fani mbalimbali ili kuweza kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Fani zinazotakiwa ni za ufundi wa Mambo ya Kale kama vile ujenzi au ukarabati, uchoraji, upimaji, sorovea kwa majengo ya kihistoria na maeneo ya kihistoria yanahitaji kuhifadhwa

12 bila kuharibu uhalisia wake. Aidha Idara hufanya utafiti na matokeo huwezesha kupatikana kwa historia, makazi, majengo, vifaa, nguo, zana za Mawe na Chuma, vyombo na vitu vilivyokuwa vikitumika kama silaha n.k. Vyote vinahitaji utaalamu wa kuvijali katika utunzaji kwa sababu ni vya siku nyingi utunzaji sio wa kawaida. Malikale aina ya floro na fauna ni masalia yanayotokana na wanyama na mimea nayo kuna utunzaji wake ni wa hali ya juu. Kuna fani za Makumbusho ambazo zina utaalamu wake ni wa ajili ya maonyesho mbalimbali yanayowekwa katika Makumbusho zote mahali popote. Taaluma za mambo ya kale zinazohitajika ni Akiolojia; Jiolojia; Palentolojia; Anthropolojia; Sosholojia; Uhifadhi na Usanifu wa majengo ya kihistoria; Jiographia; Historia; Ethnolojia; Elimu ya viumbe; mipango miji; na Uhifadhi na Usimamizi wa Malikale.Aidha, Idara huandaa Mpango wa Mafunzo ya Muda mrefu na Mfupi kuwezesha watumishi kufanya kazi hizo kwa ufanisi. Kwa miaka 2016 hadi 2019 Idara iliwezesha watumishi mbalimbali kushiriki katika mafunzo yafuatayo; Katika kuhakikisha kuwa miji na majengo ya kihistoria nchini yanaendelea kuhifadhiwa kwa lengo la kutunza historia na kumbukumbu ya Taifa kwa mwaka 2016/2017 watumishi 2 wa Wizara walishiriki katika mafunzo yaliyoandaliwa na Mji wa Kihistoria wa Humburg, Ujerumani ambao una mashirikiano na Jiji la Dar es Salaam. Mafunzo hayo yalihusu uhifadhi na ukusanyaji wa kumbukumbu na taarifa za majengo na miji ya kihistoria. Baada ya kupata mafunzo hayo, Wizara imefanya tathmini ya hali ya uhifadhi wa majengo ya kihistoria 27 ndani ya Jiji Dar es Salaam. Aidha, watumishi wanne wamepata mafunzo ya muda mrefu; watatu wamepata Mafunzo ya Shahada ya uzamili (MA) kuanzia 2017 hadi 2018 na mmoja amemaliza masomo ya uzamivu (PHD) mwaka 2018 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Watumishi wanne wamepata mafunzo ya muda mfupi: mmoja alipata mafunzo ya dereva, mmoja alipata mafunzo ya kusimamia miradi, Katibu Muktasi alisomeshwa kwenye kozi za Katibu Muktasi. 2.6.4 Mfanyakazi Bora wa Wizara, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara na Mwenyekiti wa TUGHE 2018 Katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu tano watumishi wa Idara wamechaguliwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Wizara na pia kupata ufanyakazi bora. Kwa mwaka 2018 Aprili, Mfanyakazi bora wa Wizara alichaguliwa kutoka Idara ya Mambo ya Kale.mfanyakazi huyu Bwana Idiphonce Mlowoka alipatikana kwa kushindanishwa na watumishi wengine 12 wa Idara na vitengo vya Wizara ya Maliasili na Utalii. Mtumishi anaipenda kazi yake na anaifanya kwa kujituma na mazingira magumu. Taaluma yake ni Fundi mhifadhi wa Mambo ya Kale anatumika katika kuhifadhi majengo ya Kihistoria na magofu. Hii kazi ni ngumu na ni tete kwa sababu majenzi hayo yana zaidi ya miaka 50 na mengine mia, kinachotakiwa kuyarudishia kama yalivyo na mara nyingi usipokuwa makini huporomoka. Hivyo mwaka 2018 Wizara iliamua kumtunuku mtumishi huyu Idiphonce Mlowoka Mfanyakazi bora wa Wizara. Mwaka 2019 Aprili kwa mara ya pili Idara imepata mfanyakazi bora wa Wizara, Bi Neema Mbwana kutoka kituo cha Mwalim Nyerere Magomeni. Aidha kwa Mwaka 2018 Wizara ilimteua Bwana Anthony Tibaijuka kuwa Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Wizara na Bwana William Mwita alichaguliwa kuwa Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambalo Mwenyekiti ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii. 2.6.5 Uteuzi Maalum Katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu hii ya Tano watumishi wawili waliteuliwa na kupewa kazi nyingine. Mtumishi mmoja Mheshimiwa Simon Ezekiel Odunga aliteuliwa kutoka Idara ya Mambo ya Kale na Muheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma Mwaka 2016. Mtumishi mwingine Dkt. Emmanuel Bwasiri aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi kitengo cha utafiti na mafunzo cha Wizara ya Maliasili na Utalii mwaka 2019. Haya ni mafanikio makubwa kwa Idara katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano na haijawahi kutokea kwa miaka ya nyuma.

13 SURA YA TATU

USHIRIKI WA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI KATIKA UHIFADHI WA MALIKALE 3.1 Utangulizi Sura hii inaeleza umuhimu wa uhifadhi wa Malikale na jinsi Taasisi za serikali kuanzia Makumbusho saba zinazosimamiwa na Wizara ambazo zipo Arusha, Dar es Salaam, Mara na Mkoa wa Ruvuma hadi Makumbusho ya Iringa inayosimamiwa na Mkoa wa Iringa. Lengo kuelimisha jamii kuhusu Makumbusho hizo. Taasisi za binafsi zilipo katika Mikoa ya Tanga, Mtwara, Pwani na Mwanza. 3.2 Umuhimu wa ushirikano wa Serikali na Sekta Binafsi katika Uhifadhi wa Malikale Uhifadhi wa malikale ni muhimu ili kuhakikisha kwamba maeneo yenye malikale yanadumu na kuendelezwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Maeneo ya Malikale yametawanyika katika Tanzania nzima. Mfano mzuri ni ule wa Machifu. Karibu kila kabila lilikuwa na utawala wa machifu na waliweka utaratibu wa namna ya kuhifadhi na kurithishana urithi wao wa kichifu. Makazi haya ya jadi yapo mpaka leo, kwenye baadhi ya maeneo yameendelezwa na hutumika kama vivutio vizuri vya utalii na elimu. Hivyo, imefika wakati sasa Sekta binafsi na Taasisi mbalimbali kuhamasishwa kuanzisha shughuli za makumbusho katika sehemu mbalimbali nchini. Kwa vile malikale nyingi ziko mikononi mwa jamii yenyewe, jamii ina haki ya kuelimishwa na kushirikishwa katika uhifadhi na kutambua umuhimu wa malikale hizo kama utambulisho wa ukoo, kabila na taifa. Jukumu la uhifadhi wa malikale ni la umma mzima. 3.3 Ushiriki wa Taasisi za Serikali. Shirika la Makumbusho ya Taifa ni Taasisi ya serikali kwenye Idara ya Mambo ya Kale ambayo ina jukumu kubwa la kuelimisha jamii umuhimu wa kuhifadhi Malikale. Shirika hili linaongozwa na Bodi ya Makumbusho ambaye mwenyekiti huteuliwa na Rais. Jukumu la Makumbusho ya Taifa ni kutafiti, kukusanya, kuhifadhi na kuelimisha Umma kupitia maonyesho, machapisho na mihadhara kuhusu umuhimu wa kuhifadhi na kuendeleza urithi wa utamaduni, unaohamishika kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho. Shirika la Makumbusho linatekeleza majukumu yake kupitia makumbusho saba ambazo zipo moja kwa moja chini ya Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa kwa kuzingatia Sheria ya Makumbusho Na.7 ya mwaka 1980. Makumbusho hizo ni: 3.3.1 Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es salaam Makumbusho hii ilianza kama Makumbusho ya Taifa na ilianzishwa mwaka 1934 na kuanza kutumika mwaka 1940 na ilijulikana kama Makumbusho ya Mfalme George wa Tano (v). Mwaka 1963 baada ya uhuru Makumbusho ilipanuliwa na kuongeza majego ya maonyesho mbalimbali. Mwaka 2010 upanuzi ulifanyika kwa kuongeza jengo ambalo kwa sasa linajulikana kama Nyumba ya Utamaduni ambayo ina kumbi za maonyesho mbalimbali ikiwemo sanaa, mgahawa, Studio na Ofisi.

14

Picha za juu: Januari 19, 2019 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) akiangalia kwa makini Tai iliyovaliwa wakati wa sherehe ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na mifupa na fuvu la binadamu (Skeletoni), Makumbusho ya Taifa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Constantine Kanyasu (Mb) Katikati akiangalia wadudu waliokaushwa stoo ya Biolojia Mwezi Februari 2019 Dar es Salaam.

15 3.3.2 Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam Makumbusho inayoonyesha nyumba na vifaa vya tamaduni mbalimbali zinazopatikana katika nchi ya Tanzania. Eneo hilo lipo katika jiji la Dar es Salaam Wilaya ya Kinondoni. Kijiji cha Makumbusho kipo mkabala na barabara ya Ally Hassan Mwinyi nje kidogo ya mji. Kijiji hicho kilianzishwa mwaka 1966 kwa ajili ya kuonyesha na kutunza tamaduni ikiwemo tamaduni za asili, ngoma na tamaduni za makabila mbalimbali kama Wanyakyusa, Makonde, Masai, Chagga, Haya, Ngoni, Yao na mengine mengi. 3.3.3 Makumbusho ya Azimio la Arusha Makumbusho haya yalianzishwa mwaka 1977 wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya Azimio la Arusha. Ilianzishwa kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za Azimio la Arusha kuhusu Siasa ya na kujitegemea. Jina la azimio la Arusha linatokana na mji wa Arusha lilikopitishwa tarehe 26-29 Januari 1967. Lengo la azimio hili ni kujikomboa dhidi ya umaskini wetu. (Chanzo - TANU, Dar es Salaam. (1967).

Makumbusho ya Azimio la Arusha, Chanzo: Makumbusho ya Taifa

3.3.4 Elimu ya Viumbe, Arusha Makumbusho ya Historia asilia Arusha ilifunguliwa mwaka 1987, na ni Makumbusho pekee nchini ya Historia asilia. Makumbusho hii ipo katika Mkoa wa Arusha na imejikita katika kutunza na kuhifadhi mikusanyo ya sampuli mbalimbali za Historia asilia, ikiwa ni pamoja na ukusanyaji wa kina wa masalia ya mifupa ya wanyama wenye uti wa mgongo pamoja na Historia ya mji wa Arusha - Boma. Makumbusho ya Historia asilia ipo katika Boma la zamani la kijeshi na ulinzi wa ukoloni wa wajerumani Arusha. Makumbusho hii inapakana na Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano ( AICC) na Manispaa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha. Mtindo wa awali uliboreshwa na wakazi wa mji wa Boma baada ya kipindi cha utawala wa Ujerumani. Maonyesho yaliyopo kwenye Makumbusho hiyo, yanaonyesha Chimbuko la Binadamu,Wanyama, Mimea na Mbuga Mbalimbali Mkoani Arusha. Kwa wanafunzi wanapata elimu ya Historia, Jiografia, Viumbe hai na mimea. Makumbusho hii ipo barabara ya Boma na inapakana na Ukumbi wa Arusha International Conference, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Manispaa ya Arusha.

16 Makumbusho ya Elimu Viumbe. Chanzo Makumbusho ya Taifa

3.3.5 Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwl. Nyerere Makumbusho hii ilianza mwaka 1999 mahali ambapo Baba wa Taifa Mw. Myerere alizaliwa na kuzikwa. Makumbusho hii inaonyesha Nyaraka binafsi za Mwalimu Nyerere pamoja na Maisha yake. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika kijiji cha mwitongo Wilaya ya Butiama mkoa wa Mara, alifariki Oktoba 14, 1999 nchini London, Uingereza. Hayati baba wa Taifa baada ya kufariki (14 Oktoba 1999), amezikwa kijiji cha mwitongo Wilaya ya Butiama mkoa wa Mara na makazi yake yamefanywa kuwa Makumbusho. Hivyo Makumbusho katika wilaya ya Butiama ziko mbili ambayo ipo chini ya Shirika la Makumbusho na makazi yake Baba wa Taifa yamekuwa nyumba ya makumbusho baada ya kufariki. Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere bado anakumbukwa na watanzania wengi kwa kupigania uhuru wa Tanganyika ambao ulipatikana 1961. Kwa bara la Afrika anakumbukwa kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu, hasa kwa mchango wake mkubwa wakati wa harakati za kupigania uhuru katika nchi mbali mbali barani Afrika na alitoa vitu na maeneo mbalimbali katika Tanzania yakatumika katika kupigania uhuru wa nchi nyingine za Afrika mfano, Afrika ya Kusini, Msumbiji, Namibia, Angola n.k. 3.3.6 Makumbusho ya Majimaji, Songea Mkoa wa Ruvuma Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 7/7/1980. Kuanzia hapo makumbusho haya yaliendelea kutoa huduma chini ya usimamizi wa Mkoa wa Ruvuma na wazee waliendelea kufanya maadhimisho ya siku ya Mashujaa katika eneo la Makumbusho haya kila mwaka mwezi Februari na ndio ambao wamekuwa wakitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea makumbusho hayo. Tarehe 1 septemba 2005 makumbusho haya yalikabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na mwaka 2010 yalikabidhiwa Wizara ya Maliasili na Utalii na yanasimamiwa na Makumbusho ya Taifa.

17 Makumbusho ya Majimaji. Chanzo: Makumbusho ya Majimaji

3.3.7 Nyumba ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa Tarehe 27 Februari, 2017 Familia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa maarufu kama Simba wa Vita iliikabidhi Wizara ya Maliasili na Utalii nyumba iliyopo Bombambili Songea, nyaraka na vifaa mbalimbali alivyokuwa akivitumia Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wake ili itumike kama sehemu ya Makumbusho ya Taifa. Wizara imekarabati nyumba hiyo, kuwekewa uzio na ilizinduliwa mwaka 2017 na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. tarehe 27/02/2017 kuwa miongoni mwa Makumbusho za Taifa.

Picha mbili za Nyumba iliyokabidhiwa Serikali na Familia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa. Picha ya kushoto, inaonyesha nyumba hiyo kwa nyuma na picha ya kulia inaonyesha nyumba hiyo kwa mbele

18 3.4 Ushiriki wa Sekta binafsi na Taasisi zisizo za serikali Idara ya Mambo ya Kale katika kutekeleza majukumu ya uhifadhi wa Malikale hushirikiana na wadau mbalimbali wa serikali na sekta binafsi kuhakikisha urithi huu unalindwa na kutumika kiendelevu. Taasisi za binafsi zinazojihusisha na uhifadhi na uendelezaji wa malikale ni pamoja na Uzikwasa Pangani, Urithi Tanga mjini, Mkoa wa Tanga; Trade Aid, Mikindani, Mkoa wa Mtwara; Makumbusho ya Kanisa Bagamoyo Mkoa wa Pwani; Makumbusho ya Bujora na Mkoa wa Mwanza. Hizi ni baadhi ya taasisi ambazo zinashiriki katika kuhifadhi na kuendeleza Malikale. Taasisi hizo hutumia Malikale hizo kutoa mchango katika uchumi kama kivutio cha utalii na uwezekaji kwa kuzingatia misingi na kanuni za uhifadhi na zinajiendesha zenyewe.

Kushoto BOMA Mikindani linatumika Trade Aid na Kulia BOMA, Tanga linatumiwa na Makumbusho Urithi Tanga, Majengo haya ya Kijermani yamebakia na uhalisia wake.

3.4.1 Taasisi ya Trade Aid. Trade Aid, Mikindani ni Shirika lisilo la Serikali ambalo Makao yake Makuu ni Uingereza. Shirika hili limeingia mkataba na Serikali kupitia Wizara ya Elimu tarehe 8 Agosti, 1997 kwa ajili ya kukarabati BOMA la Mikindani na kukamilika 1999. Baada ya ukarabati wa BOMA kukamilika jamii ya Mikindani ilishirikishwa kutoa maamuzi kuhusu jengo hilo litumikeje ili kulihifadhi na Jamii ya Mikindani kunufaika. Kazi zilizofanywa na Shirika hilo ni nyingi ikiwemo Elimu kwa vijana ya hotelia inayotolewa bure na mafunzo kwa vitendo wanafanyia hapohapo hotelini na kupata uzoefu zaidi wanapelekwa hoteli za nje ya Mikindani kama hoteli ya Serena ya Dar es Salaam, Pia Shirika hili limesaidia kutoa mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wafanya biashara wadogo kama washonaji, wavuvi, kupanda miti na Ufugaji wa nyuki. Wananchi baada ya kupata mafunzo ya ufugaji nyuki wameanza kufuga nyuki na Mikindani wamepata ushindi mara mbili ya kitaifa ya ufugaji nyuki. Shirika hili la Trade Aid limewapatia wananchi wa kijiji cha Mitengo bomba la maji, limekarabati Kisima cha maji cha Yakkata na limetoa mchango mkubwa kwa ukarabati wa majengo ya kihistoria ya Mikindani likiwemo BOMA, jengo la Livingstone na Ghofu la Gereza.

19 3.4.2 Taasisi ya Urithi Tanga URITHI Tanga ni makumbusho ya urithi wa Tanga, yalianzishwa mwaka 2007 na Taasisi au asasi isiyo ya kiserikali inayoitwa The Tanga Heritage Centre (URITHI). Makumbusho hayo yapo kwenye jengo lililokuwa Boma la Tanga. Boma hili lilijengwa mwaka 1890 kama ofisi na makazi ya mkuu wa wilaya. Jukumu kubwa ni kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kuhifadhi na kurithisha mila, desturi na tamaduni zake kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Ina Makumbusho kwenye BOMA la Tanga la Mkuu wa Wilaya ya Tanga

Kushoto, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2016 Mheshimiwa Anastazia Wambura alipotembelea Makumbusho hayo ya Urithi Tanga alipokuwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapo iliyolenga kujua uendeshwaji wa shughuli za kisekta. Mheshimiwa alipongeza Urithi Tanga kwa kuazisha Makumbusho hiyo ya kuweka kumbukumbu za Makabila ya Tanga pamoja na Mila na desturi.

3.4.3 Makumbusho ya Kanisa, Bagamoyo Makumbusho ya Bagamoyo yalianzishwa mwaka 1957 na ushahidi upo wa kanisa la kwanza katika mji huo la Wamisionari wa kwanza kuingia nchini kutoka Shirika la Roho Mtakatifu (Holy Ghost Fathers) ambao walifika Bagamoyo Aprili 3, 1868 na ndio mwanzo wa harakati za uinjilishaji na kuzaliwa kwa Kanisa Katoliki hapa nchini Bagamoyo.

Kushoto Makumbusho ya Kanisa na Kulia Kanisa ambalo mwili wa Dkt.. Livingstone uliwekwa na baadaye kusarishwa hadi London kuzikwa katika kanisa la Westminster Pia kanisa la kwanza Bagamoyo lina historia ya David Livingstone (19 Machi 1813 – 4 Mei 1873) alikuwa mmisionari na mpelelezi kutoka Uskotishi na alisafiri katika Nchi za Afrika ya kusini na kati. Livingstone aliaga dunia mnamo tarehe 30 Aprili 1873 katika kijiji cha Chitambo (Zambia). Watumishi wake chini ya uongozi wa Myao Susi walibeba mwili wake hadi Bagamoyo uliposafirishwa kwa meli hadi Uingereza na kuzikwa London katika kanisa la Westminster Abbey tarehe 18 Aprili 1874.

20 SURA YA NNE

MAFANIKIO YA IDARA KATIKA SERIKALI YA AWAMU YA TANO KWA MWAKA 2015 HADI 2019 4.1 Sura hii inaelezea mafanikio katika kazi mbalimbali za uhifadhi na uendelezaji wa Malikale na hasa katika vituo vya Mambo ya Kale vya Olduvai Arusha; Kalenga, Mkoa wa Iringa; Mikindani, Mkoa wa Mtwara; Michoro ya Miambani Kondoa, Mkoa wa Dodoma; Kimondo cha Mbozi Mkoa wa Songwe, Mapango ya Amboni Mkoa wa Tanga na Makumbusho ya Mkoa wa Mtwara na mafanikio katika Taasisi binafsi 4.2 Uhifadhi na Uendelezaji wa Malikale Katika kipindi hiki cha serikali awamu ya tano kuna mabadiliko makubwa yaliyofanywa kwenye Idara ya Mambo ya Kale. Lengo ni kuboresha maeneo ya Malikale na kuyaweka katika hali nzuri ya kutumika kiutalii, kielimu na kiutafiti na kuingizia taifa na wananchi kipato kwa huduma mbalimbali za kitalii. Uhifadhi na Uendelezaji wa maeneo yenye malikale kiutalii ni suala changa sana katika nchi ya Tanzania na Idara ya Mambo ya Kale. Jitihada zimeanza siku za karibuni ambapo maeneo mbalimbali yameanza kuongezewa yale mahitaji muhimu ya kiutalii ili kukidhi viwango vya kitaifa na kimataifa. Tanzania ina maeneo ambayo yana sifa za kipekee mfano Olduvai, Michoro ya Miambani, Mapango, Kimondo cha Mbozi, Majengo ya kihistoria, Makazi ya Jadi, Mila na desturi zetu, vyakula, Ngoma,lugha, mavazi n.k. Imeonekana urithi huu wa Malikale ukitumiwa vizuri bila ya kuathiri uhalisia wake unaweza kuchangia pato la Taifa baada ya kuboreshwa kwa mujibu wa Sera na sheria ya Malikale. Katika kutekeleza azma hii kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya Tano, mafanikio yafuatayo yamepatikana. 4.3 Makumbusho Mpya katika Kituo cha Bonde la Olduvai Bonde la Olduvai ni maarufu duniani kutokana na kufahamika kwake kama chimbuko la binadamu wa Kale. Historia na umaarufu wa bonde hili unafuatia ugunduzi wa masalia ya zamadamu uliofanywa na watafiti Dkt Louis Leakey na mkewe Mary Leakey.

Mwonekano wa Bonde la Olduvai Fuvu la Zinjathropus Boisei 1959 lilipatikana eneo hili (FLK)

Fuvu la binadamu wa Kale maarufu kama Zinjanthropus boisie liligunduliwa kwenye bonde hili mwaka 1959, ikifuatiwa na Homo habilis Desemba 1960, Homo erectus May 1960 na Homo sapiens mwaka 1972. Kituo hiki kipo ndani ya Hifadhi ya NCAA na kinapata wageni wengi wa ndani na Nje ya Nchi ukilinganisha na vituo vingine vya Malikale.

21 B

A

Kushoto (A) Makumbusho mpya Olduvai na kulia (B) Makumbusho ya Zamani Kituo cha Olduvai kinaingiza mapato mengi kutokana na wageni wanaotembelea eneo hili. Kituo hiki pia bado kinatumiwa na watafiti wengi wa ndani na nje ya nchi. Kutokana na umaarufu wa Kituo hiki cha Olduvai Wizara kwa ufadhili wa Jumuiya ya nchi za ulaya (EU), imejenga Makumbusho Mpya ambayo ilifunguliwa tarehe 03 Octoba 2017 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Pia, yamejengwa majengo yatakayotumiwa na jamii na lingine kwa Chakula.

Makumbusho mpya ya Olduvai iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 03 Octoba 2017. Kushoto ni Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Maghembe (Mb) na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa .

22 4.4 Uendelezaji wa Kituo cha Kimondo, Mbozi, Mkoa wa Songwe. 4.4.1 Historia na Sifa ya Kimondo Kimondo cha Mbozi ni moja ya vituo vya Mambo ya Kale na kinahifadhiwa kwa mujibu wa sheria ya Mambo ya Kale Cap 333 ya mwaka 2002. Kimondo hiki kilianguka kutoka angani katika kilima cha Mlenje, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe. Kimondo cha Mbozi kiliwekwa kwenye maandishi mwaka 1930 baada ya kutembelewa na Mjerumani kwa jina la W. H. Nott na kilifanyiwa utafiti wa kimaabara mwaka 1931. Utafiti huo ulibaini uzito wa Kimondo cha Mbozi tani 12 na ni cha Pili Afrika kwa ukubwa na uzito na ni cha Nane katika Dunia kati ya vimondo 1036 kwa takwimu za mwaka 2002. Utafiti huo pia ulibaini Kimondo cha Mbozi kina madini ya Chuma asilimia 90.45, Nikeli 8.69, Shaba 0.66, Phosphorous 0.11 na sulphur 0.01. Kimondo cha Mbozi kina mvutano wa sumaku na kikiguswa ni cha baridi muda wote. Kutokana na sifa hizo na historia hii katika Taifa letu la Tanzania ilionekana ni muhimu kuhifadhiwa na kutangazwa katika gazeti la serikali mwaka 1967. Kimondo hiki kinatembelewa na Watalii, wanafunzi na watafiti ambao huwa wanashangaa wanapoelezwa namna ya vimondo duniani vinavyoaguka na wanatamani kuona jinsi vinavyoanguka. Kimondo cha kwanza katika Afrika na Dunia ni Hoba, kipo Nchi ya Namibia, kiligundulika mwaka 1920 na kina uzito wa tani 60.

Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha aina ya wageni wanaotembelea Kimondo cha Mbozi kwa lengo la kujifunza na kujua historia ya Kimondo hicho na kilidondokaje kutoka angani. Wataalam wa Mambo ya Kale wanaelezea vizuri kuhusu kimondo hiki kutokana na tafiti zilizofanyika.

23 4.4.2 Ziara ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kimondo cha Mbozi kimeiweka Tanzania katika ramani ya dunia katika masuala ya utalii ambapo kinaaminiwa kuwa ni kati ya vimondo nane vikubwa zaidi duniani kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 12, urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22. Wageni wanaofika eneo hilo bado sio wengi lakini kikitangazwa zaidi na miundo mbinu kuwekwa vizuri Tanzania itapata Watafiti na wanafunzi kwa wingi. Tafiti za kimondo zinaendelea kufanyika Duniani.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa ( wa pili kulia) akiangalia nguvu ya mvutano kwenye Kimondo

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa tarehe 23 Julai 2017 alitembelea Kimondo cha Mbozi, Mkoa wa Songwe na alipata maelezo kwa mtaalam wa Mambo ya Kale katika Kituo cha Kimondo, Mbozi Mheshimiwa Waziri Mkuu aliagiza eneo hilo lihifadhiwe vizuri na liendelezwe kwa ajili ya utalii na matumizi ya elimu kwa wanafunzi wanaojifunza kuhusu anga. Jamii zinazoishi karibu na kimondo zinaomba na kufanya mambo ya kimila kama makongamano ya makundi ya sherehe za kimila, na harusi au ndoa kwenye Kimondo. Kimondo cha Mbozi ni kivutio cha Utalii na Elimu. Hutumika kama Nyenzo ya kufundishia masomo ya Sayansi na elimu ya Anga. Pia ni fursa ya ajira kwa jamii katika uhifadhi wa kimondo na upatikanaji wa fursa za kibiashara wakati eneo hili litakapoendelezwa kikamilifu. Matarajio ya baadaye ni kufanya eneo hili litumike kuadhimisha Tamasha la Vimondo duniani kila mwaka litakalojumuisha wageni wa ndani na nje ya nchi.

24 4.4.3 Uongozi wa Wizara kuangalia na kushauri kuendeleza Kimondo cha Mbozi Mkoa wa Songwe

Picha ya juu, Mheshimiwa Japhet Hasunga ( wa kwanza kushoto) Mbunge wa Jimbo la Vwawa na Naibu Waziri Maliasili akiwa kwenye Kimondo mwaka 2018, akipata maelezo kutoka kwa mtumishi wa Idara ya Mambo ya Kale, kituo cha Kimondo Mbozi.

Picha ya chini Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii “Major General” Gaudence Milanzi, ( wa kwanza kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Mambo ya Kale wakati alipotembelea kituo hicho mwezi February 13 2018.

25 4.4.4 Maboresho yaliyofanyika katika Kituo cha Kimondo Mbozi Kimondo cha Mbozi Songwe ni moja ya vivutio vya utalii vya Malikale chini ya Wizara ya Maliasili na utalii ambapo kinalindwa, kinahifadhiwa na kuendelezwa kwa kujengwa kwa Jengo la kituo cha taarifa na kumbukumbu. Ujenzi wa Jengo hilo ulianza Mei, 2017 na kukamilika mwezi mei, 2018, baadae ilibakia kazi za kumalizia na kuboresha eneo la nje (land scaping) ambapo ilikamilika Februari mwaka 2019. Jengo hili limekuwa chachu ya kukuza utalii Mkoa wa Songwe.

Picha ya juu ofisi ya Zamani ya Kituo cha Mbozi na picha ya chini Jengo jipya kwa ajili ya ofisi na taarifa Kituo cha Mbozi.

26 4.4.5 Tamasha la Vimondo Duniani katika Kimondo cha Mbozi, Songwe Kwa mara ya Kwanza Tanzania kitaifa iliadhimisha Tamasha la vimondo lililofanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya Vimondo Duniani ambayo hufanyika Juni 30 kila mwaka kutokana na kikao cha Umoja wa Mataifa cha tarehe 6 Desemba, 2016 kilichopitisha maadhimisho hayo. Wizara kwa kushirikiana na Mkoa wa Songwe pamoja na wadau wengine wa uhifadhi na maendeleo ilifanya maadhimisho ya siku ya vimondo duniani katika kituo cha Kimondo cha Mbozi kijiji cha Ndolezi kata ya Mlangali, Wilayani Mbozi. Lengo la kuadhimisha siku ya Vimondo Duniani Kitaifa Mkoani Songwe ni kutangaza Kimondo cha Mbozi kilichopo hapa Tanzania kitaifa na kimataifa ili kuongeza idadi ya Watalii na kuvitangaza vivutio vingine vilivyopo hapa nchini hususan Ukanda wa Utalii wa Kusini. Tamasha hili lilifanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 27 hadi 30 Juni 2018 na mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Maji siku ya Ufunguzi na siku ya kufunga Mgeni Rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla (Mb) Waziri wa Malisili na utalii tarehe 30 Juni 2018 chini ya Uongozi wa Mkuu wa Mkoa Luteni Mstaafu Chiku Gallawa. Maagizo aliyoyatoa ni Wizara kwa ujumla Idara na Taasisi zake kushirikiana na Mkoa wa Songwe kuendeleza vivutio vya utalii vilivyopo Mkoani Songwe.

Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa Mambo ya Kale Bwana Filmerick Basange kuhusu Kimondo hicho cha Mbozi namna kilivyodondoka na sifa za Kimondo hicho. Afisa huyo wa Mambo ya Kale alimwambia Mheshimiwa Waziri, aina za madini zilizomo katika Kimondo hicho na uzito wake wa tani 12 ambao umefanya kimondo kuwa cha pili kwa ukubwa Afrika na cha nane duniani. Kimondo cha Mbozi ni baridi wakati wote na kina nguvu ya mvutano.

27 Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) Waziri wa Malisili na Utalii alipotembelea Kimondo cha Mbozi tarehe 30 Juni 2018 wakati wa Maadhimisho ya siku ya Vimondo Duniani akifanya majaribio ya kuangalia nguvu ya mvutano katika Kimondo hicho

Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) Waziri wa Malisili na Utalii Wakati wa kufunga maadhimisho ya Vimondo Duniani alimtunuku Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa zawadi kwa kufanikisha Tamasha hilo na kuhamasisha Utalii ukanda wa Nyanda za Juu Kusini.

28 Katika ufungaji wa Tamasha hili Mgeni rasmi Mheshimiwa Dkt.Hamisi Kigwangalla Waziri wa Maliasili na Utalii alipata nafasi ya kutembelea mabanda mbalimbali likiwemo la Maliasili na mengine ya Wajasiriamali. Mabanda hayo yalikuwa yamejipanga kwa Wilaya, hivyo alitembelea Wilaya zote na kuona kuna nini wanaweza kuviendeleza kama vivutio vya Utalii. Pia Mkuu wa Mkoa alinunua eneo kubwa karibu na Kimondo cha Mbozi ambalo kila Wilaya itaweka vivutio vyake vya utalii ikiwa ni pamoja na utamaduni uliopo, uwekezaji, kilimo, viwanda machimbo ya madini yalipo Mkoani Songwe. 4.5 Mfumo wa Kukusanya Maduhuli Idara ya Mambo ya Kale katika awamu hii ya serikali ya awamu ya Tano imekuwa mstari wa mbele katika kusimamia ukusanyaji wa Maduhuli. Imeshirikiana na Kitengo cha Wizara cha TEHAMA katika kuandaa mfumo wa kukusanya mapato kwenye vituo vya Mambo ya Kale. Watumishi wa vituoni walielemishwa kuhusu Mfumo huo na walishiriki katika kuainisha mahitaji ya mfumo wa kukusanya mapato kilichofanyika jijini Arusha kati ya tarehe 07-21/11/2017. Idara kwa kushirikiana na Kitengo cha TEHAMA imefanya tathmini ya miundombinu ya TEHEMA kwenye vituo vya Mambo vya Kale. Hadi kufikia tarehe 10/06/2018 kazi hiyo imefanyika katika vituo vya Mikindani, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, Makumbusho ya Mwalimu Nyerere, Magomeni na Kunduchi, Dar es Salaam; Isimilia na Kalenga Iringa, Ngome Kongwe, Caravan Serai Magofu ya Kaole, Bagamoyo, Kwihara - Tabora na Ujiji – Kigoma. Kolo Kondoa na Amboni, Tanga. Kwa sasa vituo vyote 16 vimeshaingizwa katika Mfumo wa Wizara wa Kukusanya maduhuli (MNRT-PORTAL) na watumishi wa vituo 16 walipata Mafunzo ya kutumia POS kwaajili ya kukusanya maduhuli. 4.6 Uendelezaji wa Vituo vya Mambo ya Kale Mkoa wa Iringa Mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa iliyopo Nyanda za Juu Kusini na umetanda kati ya latitudo 7º 05˝ na 12º 32˝ kusini, na longitude 33º 47˝ hadi 36º 32˝ mashariki mwa Meridian. Mkoa huu una maeneo yenye mwinuko kati ya mita 1200 hadi 2000 hupata mvua nyingi kiasi cha milimita 2000. Hali ya hewa ni kuanzia 15-25 ºC. Mkoa huu una mandhari na vivutio vizuri vya utalii kama vile Isimila, jiwe la Gangilonga, Makumbusho ya Chifu Mkwawa huko Kalenga, mbuga za Ruaha ambavyo kwa pamoja vikiendelezwa na kutangazwa vitaingiza mapato. Iringa ni mojawapo ya miji ya kihistoria nchini na ilianzishwa kama kambi la jeshi wakati wa vita ya Wajerumani dhidi ya Wahehe. Wahehe waliongozwa na Chifu Mkwawa ambaye makao yake makuu yalikuwa Kalenga. Asili ya jina la Iringa ni neno la Kihehe „liliga“ lenye maana ya boma. Mji umejengwa juu ya mlima ukitazama mto Ruaha bondeni. Mji huu ulijengwa baada ya kuharibu boma la mtemi Mkwawa huko Kalenga mwaka 1894. 4.7 Ukarabati wa BOMA la Iringa Katika kipindi hiki cha serikali awamu ya Tano Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia (Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho) kwa kushirikiana na Mkoa wa Iringa na Chuo Kikuu cha Iringa kupitia mradi wa Fahari Yetu imekarabati Boma la Mjerumani na kulifanya kuwa Makumbusho ya Mkoa wa Iringa na Kituo cha Utamaduni. Ukarabati huu ulifadhiliwa na Jumuia ya Umoja wa Ulaya(EU). Ukarabati wa Boma hilo, umewezesha kuwepo kwa Makumbusho ya Mkoa, maduka ya zawadi, studio ya mziki wa asili, na mgahawa na umeleta manufaa ya kuongeza kivutio cha utalii na fursa za ajira kwa wananchi wa Iringa. Jengo hili lilijengwa kipindi cha utawala wa Wajermani mwaka 1896 na lilijengwa kwa mawe, matofali ya kuchoma ya udongo na plasta.

29 4.7.1 Hali Halisi kabla ya Ukarabati mwaka 2015

30 4.7.2 BOMA Wakati na baada ya ukarabati

Picha ya juu ukarabati uliofanyika kwenye BOMA kipindi cha awamu ya Tano na picha ya chini Mwonekano wa BOMA la Iringa baada ya ukarabati mwaka 2015 - 2016

31 4.7.3 BOMA kwenye Ufunguzi baada ya ukarabati

Makumbusho hii ilizinduliwa na Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa tarehe 25/06/2016

Muonekano wa Makumbusho ya Mkoa wa Iringa (BOMA) baada ya Ukarabati

32 4.7.4 Uongozi wa Wizara kutembelea BOMA Mheshimwa Naibu, Waziri Japhet Ngailonga Hasunga (Mb) katika ziara ya Nyanda za juu Kusini Octoba mwaka 2017 moja ya eneo alilotembelea ni Makumbusho ya Mkoa wa Iringa alikutana na Uongozi wa Makumbusho ya Mkoa wa Iringa akiwemo Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga na Mkuu wa Wilaya ya Iringa vijijini Mh. Richard Kasesela. Makumbusho hii inatoa fursa nyingi za utalii wa kiutamaduni kwa wenyeji, wakazi pamoja na watu kutoka kwa nje ya Iringa na Tanzania

Picha hii inaonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga (Mb) (kwanza kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ( wa pili kuanzia kushoto) wakimsikiliza Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga ambaye pia ni Meneja Msaidizi wa Mradi wa Fahari Yetu unaojishughulisha Uendelezaji na Utangazaji wa utalii Nyanda za Juu Kusini Octoba 2017 ndani ya Makumbusho hiyo.

Picha hii inaonesha ujumbe kutoka Mkoa wa Iringa, Wizara ya Maliasili na Utalii na Idara ya Mambo ya Kale ukipata maelezo kutoka Mhadhiri wa Chuo Kikuu Iringa, Jimson Sanga katika Makumbusho hiyo

4.8 Uhifadhi na uendelezaji wa Makumbusho ya Chifu Mkwawa Kalenga 4.8.1 Historia na Umaahiri wa Chifu Mkwawa Chifu Mkwawa au kwa jina refu Mkwavinyika Munyigumba Mwamuyinga alikuwa chifu wa kabila la Wahehe. Jina la Mkwawa ni kifupisho cha Mukwava ambalo tena ni kifupisho cha Mukwavinyika, lililokuwa jina lake la heshima likimaanisha “kiongozi aliyetwaa nchi nyingi”. Mkwawa alizaliwa mnamo mwaka 1855 mahali palipoitwa Luhota karibu na

33 Iringa mjini. Alikuwa mtoto wa chifu Munyigumba aliyeaga dunia mwaka 1879. Baba yake Munyingumba aliwahi kuunganisha temi ndogo za Wahehe na makabila ya majirani kuwa dola moja. Makumbusho ya Kalenga ni kaburi (Museleum) linalohifadhi fuvu la Chifu Mkwawa kuanzia mwaka 1954. Pamoja na makaburi mengine, kaburi hilo lipo katika eneo ambalo ni makazi au makao makuu rasmi ya Chifu Mkwawa ambaye alikuwa maarufu sana. Chifu Mkwawa alipata umaarufu huu kufuatia kuwaunganisha wananchi wake kupinga ukoloni wa Kijerumani kwa kupigana vita na majeshi yenye silaha za sasa ya Kijerumani. Katika awamu ya kwanza ya mapambano kati yake na jeshi la Wajerumani, Chifu Mkwawa alishinda vita kwa kuliangamiza jeshi la Kijerumani chini ya kamanda Von Zelewsky katika eneo la lugalo. Mwaka 1898 mnara ulijengwa ili kuweka kukumbuka ya Wajermani waliokufa katika vita ya Wajermani na Wahehe mwaka 1891. Mnara huu umetangazwa kwenye gazeti la Serikali mwaka 1953 kwa GN Na. 89. Mnara huu umejengwa katika kijiji cha Lugalo, Kata ya Lugalo, Tarafa ya Mazombe, Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa upo umbali wa Km 25 kutoka Iringa mjini sambamba na barabara kuu kuelekea Morogoro hadi Dar es salaam (Alison Redmayne 1968, Erick Jordan 2018)

Katika mwezi Julai 1891 Von Zelewski aliongoza kikosi cha maafisa Wajerumani 13 na askari Waafrika hasa kutoka Sudan 320, pamoja na wapagazi 113. Walikuwa na bunduki za kisasa, bunduki za mtombo na mizinga midogo. Zelewski aliwadharau Wahehe waliokuwa na mikuki na pinde tu. Kwa hiyo hakuona haja ya kutuma wapelelezi wa awali. Tarehe 17 Agosti 1891 Von Zelewski na jeshi lake walipita kwenye manyasi marefu karibu na Lugalo. Mkwawa alikuwa alimsubiri na Wahehe 3,000 walionyamaza hadi Wajerumani waliotembea kwa umbo la safu ndefu walipokuwa karibu kabisa wakawashambulia. Wajerumani walikosa muda wa kuandaa silaha zao wakashtushwa kabisa. Sehemu kubwa ya askari waliuawa katika muda wa dakika chache pamoja na jemadari von Zelewski.(Alison Redmayne 1968)

Hata hivyo, baadaye majeshi ya Chifu Mkwawa yalishindwa na yeye mwenyewe kuamua kujiua kwa risasi ili kujiepusha na kukamatwa na majeshi ya Kijerumani. Makazi haya ya Kalenga inasadikika yalianza kujengwa mwaka 1887 na kumalizika mwaka 1891 4.8.2 Uanzishwaji wa Makumbusho ya Chifu Mkwawa, Kalenga Katika eneo hili, lililokuwa makazi ya Chifu Mkwawa katika kijiji cha Kalenga, imejengwa Makumbusho ndogo mwaka 1953 inayohifadhi fuvu la Chifu Mkwawa. Baada ya Chifu Mkwawa kujiua wanajeshi wa Kijerumani walichukua kichwa chake wakakipeleka Ujerumani kwa sababu za kiutafiti na kiuhifadhi katika Makumbusho ya Berlin. Tarehe 09 Juni, 1954 (African Heritage - http//Afrolegends.com - 2018) ikiwa ni miaka 56 tokea kifo cha Chifu Mkwawa, Gavana wa mwisho wa koloni la Kiingereza nchini Tanganyika, Sir. Edward Twining alikabidhi fuvu hilo kwa Chifu Adam Sapi Mkwawa aliyekuwa mrithi

34 wa kiti cha uchifu kwa wakati huo. Kurudishwa kwa fuvu hili kulifuatia utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Versaille wa tarehe 28 Juni, 1919: Kifungu VIII sehemu ndogo ya 246. Kifungu hicho kilihusu makubaliano yaliyofikiwa kati ya Uingereza na Ujerumani kufuatia nchi ya Ujerumani kushindwa vita vya kwanza vya dunia na hivyo makoloni yake kukabidhiwa chini ya Umoja wa Mataifa. Uangalizi wa Tanganyika ikapewa nchi ya Uingereza. Makumbusho Chifu Mkwawa ya Kalenga ni kielelezo cha Makazi ya jadi, inatunza na kuhifadhi historia ya Chifu Mkwawa. Kijiografia, kituo kipo umbali wa kilometa 13 kutoka Iringa mjini na umbali wa takribani mita 500 kutoka barabara ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Makumbusho ya Kalenga inatoa historia ya Chifu wa Wahehe-Mkwawa pamoja na kuhifadhi fuvu lake lililorudishwa kutoka nchini Ujerumani mnamo tarehe 9 Julai, 1954. Utawala wa Kiingereza ulijenga Makumbusho ya kuhifadhi fuvu hilo mahali palipokuwa makazi ya Chifu Mkwawa-Kalenga. Kwa sasa makumbusho hiyo ya Kalenga na fuvu la Chifu Mkwawa vinalindwa na Sheria ya Mambo ya Kale sura 333 kama maeneo yenye kubeba historia ya Taifa na Makazi ya Kijadi.

Jengo lilohifadhi fuvu la kichwa cha Chifu Mkwawa lililorudishwa kutoka nchini Ujerumani tarehe 09 Juni 1954 na kukabidhiwa kwa Chifu Adam Sapi tarehe 19 Juni 1954 Kalenga na Gavana Sir Edward Twining. Eneo hili ni la Serikali linalindwa na Sheria ya Mambo ya Kale sura 333 ya mwaka 2002.

Mpaka sasa eneo hili la Makumbusho wanazikwa Machifu na pia hutumika kurithishana uchifu. Mheshimiwa Februari tarehe 16, Februari 2015, akiwa na Chifu mpya wa Wahehe, Chifu Adam Abdu Mkwawa, aliungana na mamia ya waombolezaji katika kumhifadhi Chifu wa Kabila la Wahehe, Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa aliyefariki tarehe 15 Feb 2015 katika kituo cha Kalenga na pia alishiriki katika kusimika Chifu mpya mtoto wa kwanza wa marehemu Chifu Abdu Adam Sapi Mkwawa kijana wa miaka kumi na nne ( Chanzo https://www.google.co.tz/search?q=Chifu+Abdu+Adam)

35 Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Chifu wa Wahehe Chifu Adam Abdu Mkwawa Mei Mosi 2018 wakati wa ziara yake Mkoani Iringa katika uwanja wa Samora .

4.8.3 Uhifadhi na Uendelezaji wa Kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga Makumbusho ya Kalenga ni kituo cha mambo ya kale chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii. Kituo kipo karibu umbali wa kilometa 13 kutoka Iringa mjini na umbali wa karibu mita 500 kutoka barabara ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Makumbusho ndogo ya Kalenga inatoa historia ya Chifu wa Wahehe-Mkwawa pamoja na kuhifadhi fuvu lake lililorudishwa kutoka nchini Ujerumani mnamo tarehe 9 Juni 1954. Katika kufanikisha majukumu ya kila siku, kituo kina vitendea kazi vifuatavyo: Ofisi ndogo inayotumika kupokelea wageni pamoja na kutunza kumbukumbu za ofisi; Makumbusho ndogo ambayo fuvu la Mkwawa na vitu vichache vya kiutamaduni vya kabila la Wahehe vimehifadhiwa; Pikipiki ambayo hutumiwa na watumishi katika kutekeleza majukumu ya kiofisi ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za kikazi ndani ya Halmashauri ya Wilaya Iringa; Maji kwa watumishi na wageni wanaotembelea kituo na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na usafi wa kituo. Umeme ambao hutumika kwa shughuli za ofisi na wakati wa usiku kurahisisha ulinzi na usalama wa eneo la Kituo. Katika uendelezaji wa kituo hicho hatua ya kwanza iliyochukuliwa na Wizara ni kuondoa mgogoro uliokuwa unaendelea tangu 2013 kwa kushirikiana na Mkoa. Mgogoro huu ulizuia baadhi ya kazi kutofanyika vizuri katika kituo na pia kutoendelezwa inavyotakiwa. Tarehe 17 Mwezi wa tano mwaka 2018 kilifanyika kikao kilichojumuisha Familia ya Mkwawa, Mkoa na Wizara ya Maliasili na utalii na kuweka Maazimio ambayo yakisimamiwa kikamilifu migogoro hiyo haitakuwepo. Wakuu wa kituo hicho walihamishwa kwa kukosa amani na kushindwa kutekeleza majukumu yao. Mgogoro huu ulitatuliwa na Wizara akiwemo Katibu Mkuu Wizara Maj. Gen. Gaudence S. Milanzi na kwa upande wa Mkoa ujumbe ukiongozwa

36 na Mkuu wa Wilaya Mheshimiwa Richard Kasesela na familia ya Mkwawa iliongozwa na Msemaji wa Familia Edmond Mkwawa na ikakubalika kuwa hiki ni kituo cha serikali inatakiwa taratibu na sheria za kiuhifadhi zizingatiwe.

Mwezi Mei 2018 Wizara, Mkoa na Familia ya Mkwawa walikuwa na kikao cha kuangalia namna ya kuendeleza Kituo cha Kalenga. Kwa upande wa Wizara ya Maliasili na Utalii, kiliongozwa na Meja Generali Gaudensi S. Milanzi Katibu Mkuu Maliasili na Utalii Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Wilaya Iringa vijijini Mheshimiwa Richard Kasesela na Edmond Mkwawa aliongoza ujumbe wa familia waliokaa katikati kwenye picha. Maazimio baada ya kikao baina ya Serikali na Wanafamilia mwaka 2018. · Serikali kwa kushirikiana na wanafamilia walipiga marufuku kwa mtu yeyote kutembelea kituo cha Kalenga na kuleta fujo. · Wananchi watambue kuwa makumbusho ya Chifu Mkwawa Kalenga ni mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo ni kosa kufunga kituo hicho. · Kikao kilikubaliana kuwa familia iwe na msemaji kwa ajili ya kurahisisha shughuli mbalimbali za maendeleo katika eneo la Kalenga. · Serikali inafanya mawasiliano kwa maandisi wanafamilia watumie maandishi kuikumbusha serikali jambo lolote kulitekeleza au kuwasilisha malalamiko. · Kuhusu Makaburi huwa familia wana taratibu za kutunza na wanapalilia wenyewe na wanaruhusiwa kuabudia. · Bi Fatuma asirudie kujichukulia hatua mkononi na afuate taratibu za mawasiliano serikalini kwa kuwa anazifahamu na yeye ni mtumishi wa Umma na · Wizara kuweka mikakati ya kuendeleza kituo hicho kwa kushirikisha familia na Wananchi.

37 4.8.4 Kuimarisha Utendaji wa Kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga 4.8.4.1 Kuimarisha Uongozi wa Kituo Mwaka 2017/2018 Wizara iliamua kubadilisha watumishi wawili waliokuwepo kituo cha Kalenga mmoja yupo Dodoma na mwingine amepelekwa Mikindani kwa lengo la kuimarisha kituo hicho. Watumishi wawili (2) hao mmoja katoka kituo cha Mbozi na Mwingine kituo cha Kaole Bagamoyo walihamishiwa Kituo cha Kalenga na wana elimu ya Chuo Kikuu. Mkuu wa kituo ana shahada ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Dares Salaam Shahada ya Usimamizi wa Malikale na Diploma ya usimamizi wa Malikale na kuongoza Watalii na msaidizi wake ana Shahada ya Anthropolojia na Utalii katika Malikale kutoka Chuo Kikuu cha Iringa. Pia, Kituo kina walinzi kutoka kampuni binafsi ya ulinzi ya JBM Security and General Services CO. Limited na vibarua wa usafi kutoka kampuni binafsi ya ulinzi ya Sokoni Patners. Lengo lilikuwa kuimarisha kituo hicho kuondoa mgogoro iliyokuwa inaendelea mara kwa mara katika kituo cha Kalenga tangu Novemba, 2013 hadi 2018. 4.8.4.2 Kuimarisha Mipaka katika kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga, Mkoa wa Iringa Kazi ya kuhakiki na kupima upya mpaka wa Kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga ilifanywa na Wizara kwa kushirikiana na Mkoa na Halmashauri ya Mji wa Iringa vijijini tarehe 27-28 Juni 2018 kwa kushikisha wenyeviti wa Vijiji vya awamu zote nne waliokuwa wanauelewa Eneo hilo. Wenyeviti hao ni Bwana Ibrahimu Mbeju, Raymond Kalinga, Yunus Mwaugali na Francis Kalinga ambaye ndiye mwenyekiti wa sasa. Kwa upande wa familia ya Mkwawa alipatikana Bi Fatma Mkwawa. Baada ya uhakiki nguzo 14 na becoans 12 zilitumika kuimarisha mipaka kuzunguka eneo lote la Kalenga lenye jumla ya hekta 7.6. Kazi hii ilifanywa kwa ushirikiano wa Mkoa wa Iringa, Familia ya Mkwawa, Wenyeviti wa Kijiji cha Kalenga wanne na Wizara ya Maliasili na Utalii mwezi Juni 2018. Baada ya Michoro kukamilishwa na Halmashauri ya Iringa ilipelekwa Wizara ya Ardhi Octoba 2018 na imeshathibitishwa na kukabidhiwa kituo cha Chifu Mkwawa Kalenga tarehe 28 Octoba 2018. Kinachofuatia kukamilisha taratibu za kupata Ramani na Hati. 4.8.5 Ushirikiano wa Serikali na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi ya Mambo ya Kale nchini Katika jiihada za Serikali za kuendeleza ushirikiano na jamii zinazozunguka maeneo ya hifadhi nchini, Mwezi Octoba 2017, Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa msaada wa mabati sitini kwa ajili ya kuezeka madarasa ya shule ya msingi Kipanga baada ya kuezuliwa na kimbunga katika kijiji cha Ubwachana Wilaya ya Iringa mkoani Iringa. Msaada huo ulitolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga alipotembelea kituo cha Malikale cha Isimila mkoani humo ambacho kinapakana na shule hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja Mkoani humo. Akikabidhi mabati hayo, Naibu Waziri Japhet Hasunga alisema Serikali inatambua mchango wa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kwenye uhifadhi shirikishi hivyo ni jukumu la Serikali kuwaunga mkono pale wanapopatwa na majanga ya aina mbalimbali. Aidha, aliwataka baadhi ya wananchi wanaochimba mchanga kwenye maeneo ya vivutio katika kituo hicho waache mara moja kabla ya kuchukuliwa hatua za kisheria kwakuwa wanahatarisha uhai wa kingo za miamba ya kale ambayo na kivutio kikubwa cha utalii wa asili katika ukanda wa kusini. Katika ziara hiyo ya Mh. Japhet Hasunga (Mb) ya Mkoa wa Iringa ya kutembelea Maeneo ya Mambo ya Kale alifuatana na ujumbe wa Mambo ya Kale uliongozwa na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Kale Bi. Digna Tillya. Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya mambo

38 ya Kale, Bi. Digna Tillya aliwasihi wananchi wanaozunguka kituo hicho kushirikiana na Serikali katika uhifadhi na ulinzi wa kituo hicho ambacho ni moja ya maeneo muhimu ya Mambo ya Kale yanayojulikana ndani na nje ya nchi kwa Chimbuko la Zana za Mawe. Pia kujiepusha na vitendo vya uharibifu wa mazingira.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akimkabidhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Ubwachana, Donatus Lihoha mabati 60 kwa ajili ya kuezeka vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Kipanga ambayo iliezuliwa na kimbunga ikiwa ni kutambua mchango wa wananchi katika uhifadhi shirikishi wa Kituo cha Mali Kale cha Isimila Mkoani Iringa. 4.9 Mapango ya Amboni 4.9.1 Historia ya Mapango Mapango ya Amboni yapo kilomita 8 kaskazini magharibi mwa jiji la Tanga. Yanafikika kwa njia ya Barabara Tanga-Horohoro-Mombasa katika kijiji cha Kiomoni mwendo wa takriban daika 20 kwa gari kutokea Tanga mjini. Mapango ya Amboni ni moja kati ya mapango maarufu duniani yaliyofanyika katika miaka milioni tatu iliyopita. Mabadiliko ya tabia ya hali ya nchi, yamesababisha miamba hiyo yenye asili ya chokaa kuunda taswira/sanamu za vitu na maumbo mbalimbali. Mapango ya Amboni yapo nane (8) ambayo yanasadikiwa kuchukua ukubwa wa kilometa za mraba 234. Mapango haya yapo katika kijiji cha Kiomoni. Eneo hili linapakana na bahari ya Hindi pamoja na mto Mkurumuzi. 4.9.2 Hali ya Uhifadhi wa Mapango ya Amboni Mapango ya Amboni ni Urithi na Kumbukumbu ya Taifa na yamehifadhiwa kwa Tangazo la Serikali (GN) namba 331 la tarehe 1 Oktoba, 1954 wakati wa Serikali ya kikoloni ya Waingereza.Mapango haya yapo katika hali nzuri ya uhifadhi, kwani mazingira na mandhari ya mapango yamehifadhiwa kisheria na kitaalamu ili kuzuia uharibifu utokanao na shughuli za kibinadamu na asili kutoathiri uasili wa mapango. Hata hivyo nje ya mapango hayo kuna mto wa mkurumuzi ambao wakati masika hutokea mafuriko na kuathiri eneo la mapango. Vilevile eneo la jirani na mapango kuna uchimbaji wa kokoto unaotumia baruti/milipuko ambayo tunadhani inaathiri uhifadhi wa mapango hayo na wakati mwingine wageni huogopa

39 wasikiapo milipuko hiyo. Kutokuwa na hati miliki ya eneo hivyo kusababisha migogoro na wanakijiji pale inapotekea uharifu wowote wa mazingira. Ukosefu wa maeneo ya kupumzikia watali wanapokuja kuangalia mapango (recreational areas). Kwa mwaka 2017/2018 Kamati ya Bunge ilitembelea maeneo hayo na kuagiza Wizara kuweka mikakati ya kuendeleza kituo hicho kiutalii. Kazi iliyofanyika kwa mwaka 2017/2018 niniuhakiki mipaka ya kituo cha Mapango ya Amboni, Tanga na kuweka beacons. Eneo lina jumla ya Sq km 39.5. Mipaka ya Kituo cha Mapango ya Amboni ilihakikiwa na Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale sehemu ya uhifadhi kwa kushirikiana na Manispaa ya Mkoa waTanga na Kitengo cha Manunuzi cha Wizara. Kinachotakiwa sasa hivi ni kushikiana na Mkuu wa Kituo kupata hati.

Picha za juu kushoto Becoans zilizowekwa na kulia njia ya kuingia kwenye Mapango Amboni na Picha ya chini Mheshimiwa Waziri alipotembelea Kituo cha Mapango ya Amboni, Kiomoni, Mkoa wa Tanga

Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangala Waziri wa Maliasili na Utalii ndani ya Mapango ya Amboni alipotembelea kituo cha Amboni tarehe 22 Februari 2019

40 4.10 Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe wa Mikindani Mtwara 4.10.1 Historia ya Mji Mkongwe Mikindani Mtwara Mji wa Mikindani ulikuwa na makazi ya watu tangu karne ya 9 BK. Mji ulikuwa na wafanyabiashara Waarabu kutoka Omani waliojenga nyumba zao Mikindani wakitumia bandari ya zamani ya Mikindani kabla ya kuhamishwa kwenda Mtwara mjini. Kuanzia karne ya 16 hadi 19 Mikindani ilikuwa bandari muhimu upande wa kusini ya Kilwa wakati wa biashara ya misafara ya watumwa na ndovu. Mwezi Agosti 1888 Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ilikodisha pwani la Tanganyika kutoka Sultani wa Zanzibar. Mwaka 1916 wakati wavita kuu ya kwanza ya dunia majengo karibu na bandari yaliharibiwa kutokana na uvamizi wa Kiingereza. Baada ya vita hiyo Mikindani ilikuwa makao makuu ya wilaya ya Mikindani chini ya Waingereza. Waingereza Walihamisha utawala wa wilaya kwenda Mtwara waka 1947 walipoanzisha Mji mpya. Picha za chini zinaonesha Boma la Mikindani lililojengwa mwaka 1895

Picha ya juu BOMA lilojengwa na Mjermani kabla ya ukarabati na picha ya chini baada ya ukarabati na Trade Aid mwaka 1997 hadi 2000

41 Trade Aid Mikindani ni Shirika lisilo la Kiserikali ambalo Makao yake Makuu ni Uingereza. Shirika hili liliingia mkataba na Serikali kupitia Wizara ya Elimu tarehe 08 August, 1999 kwa ajili ya kukarabati BOMA la Mikindani. Baada ya ukarabati wa BOMA kukamilika jamii ya Mikindani ilishirikishwa kutoa maamuzi jengo hilo litumikeje ili kulihifadhi na Jamii kuweza kunufaika. Uamuzi uliotolewa ni kuwa litumike kama hoteli na kituo cha mafunzo ya ujasiriamali. Kuanzia mwaka 2000, jengo hilo lilianza kutumika kama hoteli na kutoa mafunzo ya fani mbalimbali za hoteli kwa vijana wa Mikindani na Mtwara ili kuwasaidia kujiriwa na kujiajiri kwa lengo la kupunguza umaskini. 4.10.2 Uzinduzi na Uhifadhi wa Mji wa Kihistoria Mikindani Wizara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Mikindani Mkoa wa Mtwara na Trade Aid ilikamilisha zoezi la kupima na kuweka mipaka (beacon) ya mji wa kihistoria wa Mikindani. Aidha, Maeneo yote yenye majengo ya kihistoria yameonyeshwa kwenye ramani. Ramani hiyo iliwasilishwa Wizara ya Ardhi Dar es Salaam na kupatiwa namba na kukamilisha utangazaji wa eneo hilo katika Gazeti la Serikali kuwa urithi wa Taifa. Mji wa Kihistoria wa Mikindani Ulitangazwa rasmi kuwa kumbukumbu ya kihistoria na Urithi wa Utamaduni wa Taifa kwa Tangazo la Serikali No.308 la tarehe 25/8/2017. Vilevile, Mwaka 2016 Wizara ilianzisha kituo kipya cha Mambo ya Kale, Mikindani ambacho kina watumishi wawili kutoa ushauri kuhifadhi na kuendeleza mji huo. Pia, Wizara imeorodhesha majengo ya kihistoria, imetathmini hali ya uhifadhi wa sasa, umiliki, mahali yalipo, picha zake na mapendekezo ya ukarabati.

A B

Juu Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akipewa maelezo na Meneja Mradi wa Trade Aid, Emmanuel Mwambe( wa pili kushoto). Chini Mh Naibu Waziri akipata maelezo ya ukarabati wa Kisima na Rehema Abdalah mkazi wa Mikindani. Picha hizi zilichukuliwa katika Tamasha la Urithi na Siku ya Mikindani. C

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Japhet Hasunga (Picha A wa tatu kushoto) akipewa maelezo na Meneja Mradi wa Trade Aid, Bwana. Emmanuel Mwambe( wa pili kushoto picha A) kuhusiana na

42 ukarabati wa Old Boma (Picha B) ambalo kwa sasa linatumika kama hoteli na pia kama kituo cha kufundishi vijana zaidi ya 400 kuhusiana na kozi ya ukarimu kwa watalii. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni siku ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambo ya kale kwa mikoa ya Kusini. Wanne kulia ni Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Monica Mussa. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah (Picha C) ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima cha mnamo karne ya 15. Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Mheshimiwa Japhet Hasunga Naibu waziri wa Maliasili na Utalii kwa niaba ya Mh. Waziri Mkuu alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii kwa mikoa ya Kusini. Tamasha la uzinduzi wa mji wa mkongwe wa mikindani lilifanyika kuanzia tarehe 1-6/10 /2018 na yalifanyika sambamba na Tamasha la Urithi, kilele chake kilikuwa tarehe 6/10 siku ambayo mji huo ulizinduliwa.

Katika uzinduzi wa mji huo Mgeni rasmi alisema kazi ya kuhifadhi na kutangaza rasilimali za Mambo ya Kale ni jukumu la wananchi wote hivyo hawana budi kushiriki katika kuhifadhi na kutangaza. Sheria ndogo ndogo na kanuni zinazosimamia uhifadhi na uendelezaji wa eneo la Mikindani ziandaliwe na aliwapongeza Shirika lisilo la kiserikali Trade Aid kwa jitihada linalofanya la kuhamasisha wananchi kuhifadhi mji huo. Kufutia juhudi hizo za Serikali za kutaka kuongeza idadi ya watalii, Naibu Waziri alisema juhudi hizo zitasaidia kutangaza na kuhamasisha jamii kupenda na kuenzi utamaduni wao na hivyo kuulinda na kuutumia utamaduni kama fursa ya kukuza utalii kwa mikoa ya kusini. Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema tamasha hilo limekuwa muhimu kwa Wanamtwara kwa vile linafungua milango kwa watu binfasi pamoja na Mashirika kuwekeza kwenye utalii wa mambo ya kale. Kwa upande wake, Kaimu Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andy Karas, ameipongeza Serikali kwa hatua inazozichukua za kuhakikisha maeneo yenye historia yanatunzwa na kuenziwa. Mji mkongwe wa Mikindani ni mojawapo ya maeneo yenye majengo mengi mazuri ya kihistoria yaliyojengwa karne ya 15 na 19 wakati wa utawala wa kikoloni hapa nchini.

43

Mwonekano wa Mji wa Kihistoria wa Mikindani, Mtwara 4.10.3 Uwezeshwaji wa jamii ya Mikindani Shirika lisilo la kiserikali la Trade Aid katika kusaidia jamii ya Mikindani imejenga Bomba la Maji kwa ajili ya kuwapatia Wananchi wa Kijiji cha Mitengo, Mikindani, Mtwara maji safi. Kazi hii imefanywa kwa ushirikiano wa Mkoa Trade Aid na Wizara ya Maliasili Utalii.

Mhe. Fatuma Ally, Mkuu wa Wilaya ya Mikindani Mtwara kulia na kushoto Bwana Brian Currie Mwenyekiti wa bodi ya Trade Aid Uingereza wakizindua Bomba la Maji, kwa Wananchi wa Kijiji cha Mitengo, Mikindani, Mtwara Mwaka 2015.

44 4.10.4 Kuanzishwa kwa Makumbusho katika Mji wa Kihistoria, Mikindani Kuanzishwa kwa Makumbusho ya Mikindani katika mji wa Kihistoria wa Mikindani, Mtwara ni kuboresha na kuongeza wigo wa vivutio vya Utalii Mkoa wa Mtwara. Makumbusho itatumika kama kituo cha elimu na mafunzo na pia kuweka kumbukumbu kwa ajili ya kizazi kinachokuja. Lengo ni kurithisha utamaduni wa mji wa kihistoria wa Mikindani. Makumbusho haya yalifunguliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) tarehe 06 Octoba 2018.

Kushoto ni Bwana Emmanuel Mwambe akielezea onesho la nyumba za jadi zinazojengwa Mkoa wa Mtwara, kitanda na vifaa vya ndani. Picha ya kulia inaonyesha vyombo vya ndani kama vyungu vya jadi, nguo za magome, jiwe la kusagia, vyombo vya waarabu, makonde “mask”, vinyago, mazao ya uvuvi, kilimo n.k.

Mji waMikindani kihistoria Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Constantine Kanyasu (Mb) (kulia) akipewa maelezo na Bwana Paul Ndahani Mkuu wa Kituo cha Mikindani, ndani ya Makumbusho tarehe 02 Machi 2019 kuhusu ukubwa na uhifadhi wa mji wa Kihistoria Mikindani (Picha ya kushoto ni mchoro uliyokuwa akionyeshwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wa mji wa Kihistoria wa Mikindani)

45 4.10.5 Ukarabati wa Kisima cha Kihistoria, Haikata, Mikindani, Mtwara

Kisima cha Haikata Picha ya kwanza na pili kwenye ukurasa huu Wananchi wa Mikindani wakishiriki katika kazi ya ukarabati wa Kisima cha kihistoria cha ‘Haikkata.’

Ukarabati wa kisima cha kihistoria cha Yakata ‘Haikkata’ ni kwa ufadhili wa Shirika la Trade Aid lengo ni kulinda historia ya kisima hicho ni cha karne ya 15. Kisima hiki ni sehemu ya matambiko kwa jamii ya makabila ya Mtwara.

Kisima baada ya ukarabati kilizinduliwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (Mb) Octoba 2018

46 4.11 Uhifadhi wa Michoro ya Miambani, Tanzania 4.11.1 Historia ya Michoro ya Miambani Michoro ya miambani katika Tanzania ipo katika Mikoa mbalimbali ikijumuisha mikoa iliyopo kanda ya Ziwa Victoria ambapo kuna maeneo yenye michoro zaidi ya 200 na mikoa ya kanda ya kati, Kaskazini na nyanda za juu kusini ambapo kuna maeneo zaidi ya 550 (Prof. Pamella Wilii 2013). Michoro ya Miambani iliyopo Wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma nchini Tanzania, Mapango au nusu mapango haya zaidi ya 150 yanapatikana mfululizo kwenye vilima vinavyotazama mtelemko wa Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. Michoro hii inaonyesha picha za watu, wanyama na uwindaji. Hii inatazamwa kutoa ushuhuda wa namna ya maisha ya wachoraji waliokuwa wawindaji hasa. Hakuna mapatano kama michoro hii ilikuwa sehemu ya ibada za kuomba mafanikio katika uwindaji au labda ilikuwa namna ya kusimulia habari za maisha haya au labda tu sanaa ya awali bila ya makusudi. Wataalamu wengine huamini ya kwamba picha hizi zilichorwa tangu miaka 1500 iliyopita na jamii za wawindaji waliokalia eneo hili, lakini wengine husema inaewezekana ni za zamani zaidi, labda hata miaka 50,000 iliyopita. Kuna dalili ya kwamba sehemu ilichorwa na Wasandawe na Wahadzabe ambao walihifadhi desturi ya kuchora mwambani hadi miaka ya karibuni na walikuwa wawindaji hadi leo. Mwaka 2006 eneo hilo liliingizwa katika orodha ya Urithi wa dunia kwa sababu ya wingi wa michoro hii na ni eneo lenye thamani za kipekee za michoro ya miambani na zenye kuonyesha Uwezo wa binadamu kufikiri na kutunza kumbu kumbu kwa kutumia michoro kabla ya ugunduzi wa maandishi. Mahali pazuri pa kuangalia michoro kadhaa kwa urahisi ni kijiji cha Kolo kilichopo kwenye barabara kuu kati ya Babati na Kondoa. Kutoka hapo si mbali hadi sehemu kadhaa penye michoro.

Mifano ya Michoro ya Kondoa Kolo Mkoa wa Dodoma 4.11.2 Kukarabati jengo la kituo cha Michoro ya Miambani Kolo na kuweka umeme Kituo cha michoro ya Miambani Kondoa kilichopo katika kijiji cha Kolo Mkoa wa Dodoma kilomita 184 kutoka Dodoma mjini kina majengo mawili ambayo hutumika kama ofisi pamoja na kituo cha taarifa kwa wageni. Mgawanyo wa majengo haya ni kuwa vyumba viwili vya jengo kubwa hutumika kama ofisi za watumishi wa kituo hicho na vyumba viwili vikubwa hutumika kwa kupanga onesho linalotoa taarifa za awali kwa wageni wanaotembelea kituo hiki na katika jengo hili pia kuna stoo ya kutunzia vifaa vya usafi pamoja na choo. Maonyesho hayo yanaelezea rasilimali kale zinazopatikana katika Kondoa ambazo ni kielelezo muhimu cha Historia ya watu wa jamii mbalimbali kama Wasandawe (Waokota matunda na wawindaji),

47 Warangi, Burunge, Maasai, Wabarbaigi, (Wakulima na wafugaji) na ni kielelezo cha urithi wa kale unaonesha kwa namna gani kizazi kilichopita waliweza kuitafsiri na kuielezea dunia kwa njia za michoro kabla ya kugunduliwa maandishi. Idara kwa kutumia Mafundi wa Wizara, mwezi Septemba 2018 imeboresha Kituo cha Taarifa ambacho kipo Kolo Mjini, Wilaya ya Kondoa. Kazi nyingine zinatakiwa kufanyika ni kuangalia namna ya kuendeleza maeneo yenye michoro kwa lengo la kuvutia watalii na kupata mapato zaidi kwa kuboresha miundo mbinu, kama barabara au njia za kupita, umeme, maji, vyoo, mahali pa kupumzika na kupata vinywaji baridi na taarifa mbalimbali za kituo; kuwa na eneo la kujenga hoteli, mgahawa na maduka ya kitalii; kuandaa orodha ya maeneo yote ya michoro; na kuyatangaza.

Ofisi ya michoro ya miambani Kolo Kondoa, Mkoa wa Dodoma 4.11.3 Ukarabati wa Ofisi ya Michoro ya Miambani Kolo Kondoa

Maboresho yaliyofanyika ni pamoja na kuanua onyesho lote na kuweka onyesho upya, kuweka ceiling mpya jengo lote na kuondoa popo wote, kuziba nyufa za ukutani, kubandua sakafu na kuweka upya na jengo hilo lilikuwa halina umeme hivyo ilibidi umeme uwekwe kwenye kila ofisi na eneo la kutolea taarifa.

48 4.11.4 Utalii wa ndani (Michoro ya miambani Kolo, Kondoa) Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea Michoro ya Miambani Kolo, Kondoa Dodoma Septemba 2018, Njia ya kwenda kwenye michoro inahitaji maboresho kidogo bila kuharibu uhalisia.

Watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliotembelea Michoro ya Miambani Kolo, Kondoa wakipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa Kituo Bwana Zuberi Mobie 4.12 Mafanikio ya Idara kwa upande wa Sekta binafsi 4.12.1 Maadhimisho ya miaka 150 kwa Kanisa katoliki la Bagamoyo Mji wa Bagamoyo upo wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na upo kwenye Mwambao wa bahari ya Hindi. Umejengwa na waswahili na una historia ya biashara ya utumwa na dini mbalimbali za Kikristo na Kiislamu. Bagamoyo kama kituo cha biashara ya Watumwa, inaonyesha jinsi Wamisheni wa Shirika la Roho Mtakatifu walivyowasili mwaka 1847 na kujenga Kanisa Katoliki ambalo waamini wake wa awali walikuwa watumwa waliokombolewa katikati ya Bahari ya Hindi kutoka kwa wafanyabiashara wa Kiarabu kwa kupitia kanisa hilo na kuachiwa huru. Bagamoyo ikiwa kama lango la Dini ya ukristo kwa Afrika Mashariki na Kati, Mwaka 2018 Shirika la Roho Mtakatifu liliadhimisha Jubilee ya Miaka 150 ya uwepo na utume wake nchini Tanzania. Maadhimisho ya miaka 150 tangu ukatoliki uingie Tanzania Bara kupitia mji mkongwe wa Bagamoyo na miaka 100 tangu Kanisa Katoliki lipate PaDkt.i wa kwanza mzawa yaliadhimishwa Novemba 4, 2018. hii ni kumbukumbu nzuri ya historia Bagamoyo. http://sw.radiovaticana.va Katika kipindi hiki cha serikali awamu ya tano la Maaskofu la Tanzania (TEC) liliazimia Bagamoyo kuwa jimbo linalojitegemea kwa kuwa Bagamoyo ilikuwa mlango mkuu wa kuenea kwa Kanisa katika Afrika Mashariki na Kati. Katika kuadhimisha miaka 150 ya Kanisa Katoliki, iliamuliwa kuwa jimbo linalojitegemea ili kuwezesha jimbo hilo kuimarika kidini na kiutalii. Bagamoyo lilikuwa linapata huduma zote kutoka katika jimbo la Morogoro.

49 MSALABA wa Jubilei ya Miaka 150 ya Uinjilishaji Tanzania Bara iliyoadhimishwa Mji wa Bagamoyo Novemba 4, 2018. Msalaba huu unatumika kwa ajili ya Utalii wa dini (kuhiji) Eneo hili ni sehemu ya Makumbusho ya Kanisa na hutunzwa na Kanisa Katoliki

Kwa Hivi sasa Bagamoyo ina wageni wengi ambao wengi wanaokwenda kiutalii kupata historia ya Bagamoyo na wengine kidini (kuhiji) na hivyo kuonekana kuwa na uhai. Kanisa katoliki Bagamoyo kuwa jimbo kutaimarisha Makumbusho ya Kanisa Katoliki Bagamoyo na tayari wamshaanza kujenga hoteli nzuri za malazi kwa wageni wanaokwenda Bagamoyo. Pia wageni wanaokwenda kanisani hupata fursa ya kutembelea maeneo mengine ya Kihistoria Bagamoyo kama Kaole, Caravan Serai, Mji Mkongwe wa Bagamoyo na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii. 4.12.2 Makumbusho ya Wasukuma ya Bujora (Bujora Sukuma Museum Makumbusho ya wasukuma, Bujora Mkoa wa Mwanza ni moja ya makumbusho ya mfano nchini Tanzania kutokana na kuhifadhi kumbukumbu mbalimbali zikiwemo Mila, tamaduni na desturi na mgawanyo wa tawala wa kabila hilo katika himaya ya kisukuma katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. Makumbusho haya yapo eneo la Kisesa nje kidogo ya jiji la Mwanza. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa tawala za kisukuma zilianza kuimarika na kustawi tangu miaka ya 1505, lakini ni moja ya makabila nchini Tanzania ambayo yamekuwa mstari wa mbele katika kuenzi mila na desturi zao zikiwemo za kuvaa nguo za Rubega, shughulii za ufugaji na utamaduni wa kucheza ngoma za asili zinazoambatana na maonyesho ya mazingaobwe, nyoka,fisi nk na mashindano hayo ya ngoma huwa kwa makundi na hufanyika kila mwaka. Huu ni mfano wa makabila yote ya Tanzania kuiga na kuwekeza katika kujenga makumbusho ya mila na tamaduni zao kwenye mikoa yao kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

50

4.13 Kuendeleza kituo cha Kunduchi, Dar es Salaam Kituo cha Kunduchi kina Magofu 58 ya makaburi ya Masultani, Msikiti wa karne ya kumi na tano, makaburi ya kawaida pamoja na masalia mbalimbali ya Kale ni udhibitisho wa kuwepo bandari ya Kale kuanzia karne ya nane na kuendelea wakati wa utawala wa masultani katika Pwani. Wanahistoria na wanaakiolojia wa Afrika ya Mashariki wameita ni eneo lenye kuonyesha “kilele chenye kuonyesha ustaarabu juu wa Kiswahili”. Eneo hili ni sehemu ya nchi ya iliyokuwa inaitwa “Azania au Zanj” Magofu haya yalianza kujengwa kipindi cha karne ya 9 - 18 mpaka karne ya 18, kipindi cha uhamiaji uliofanywa na wageni kutoka nchi za Oman, Persia na Uarabuni na kabla ya magofu hayo kulikuwa wabantu wa pwani wakifanya uvuvi, ufuaji chuma, utengenezaji wa chumvi na shughuli zingine. Eneo hili lina fukwe nzuri za kupumzikia na pia lipo karibu na Kisiwa cha Mbudya ambacho kwa sasa hivi kinapata wageni mbalimbali wanaokwenda kupumzika kisiwani na kufanya utalii wa baharini. Uongozi wa Wizara ulitembelea eneo hilo kuangalia namna ya kuliendeleza siku za mbeleni wageni wamekuwa na hamasa ya kutembelea hili na kufanyia ibada kwa masultani na wengine kujua historia. Eneo liko wazi kwa Watanzania kutembelea kuona mambo mengi ya historia ya kujifunza na hata hali ya hewa inavutia na inafaa kwa mapumziko.

Katibu Mkuu Prof. na Wadau wakitembelea eneo la Kunduchi na kuangalia namna ya kuliendeleza eneo hilo.

51 SURA YA TANO

KUENDELEZA VITUO VYA MAMBO YA KALE NA MAKUMBUSHO VILIVYOPO CHINI YA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

5.1 Utangulizi Sura hii inaelezea maagizo ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) Mwaka 2018 alitoa maelekezo mbalimbali ya kuhifadhi na kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale wakati alipokuwa kwenye ziara mbalimbali katika vituo Mambo ya Kale. Kwa lengo la kuhakikisha kuwa vinatoa mchango kiuchumi na kijamii katika kuongeza pato la Taifa kwa kuongeza muda wa Watalii kukaa nchini na kuimarisha kumbukumbu hizo. Aidha, Wizara katika hotuba ya bunge la bajeti ya mwaka 2018/2019 maelekezo hayo yaliwasilishwa. Maelekezo hayo ni: * Kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi za Wizara ambazo ni NCAA, TANAPA, TAWA na TFS * TANAPA kuendeleza kituo cha Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni * Kuhamisha baadhi majukumu ya Mambo ya Kale kwenda Makumbusho ya Taifa na Idara kubaki na masuala ya kisera na kisheria. Lengo ni kuendeleza Sekta ya malikale ili kuchangia katika maendeleo ya sayansi, mapato ya nchi na ustawi wa jamii.

Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) akiisoma hati ya Uhuru iliyotolewa na Malikia wa Uingereza mwaka 1961

52 5.2 Kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi 5.2.1 Kuundwa kwa Kamati ya kutekeleza maelekezo hayo Wizara iliunda vikundi kazi vya aina mbili moja ni kwa ajili ya kuangalia taratibu na sheria zinazohusika katika kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii bila kuathiri utendaji wa Taasisi hizo. Kamati hii ilijumuisha Taasisi zote za Wizara Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA), Wakala wa Misitu(TFS), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na Makumbusho ya Taifa (NMT). Kamati ya pili ilihusika na kuaangalia ni majukumu yapi ya Mambo ya Kale yahamie Makumbusho ya Taifa na Idara ibakie na majukumu ya kisera na sheria. Kamati zote zilipewa hadidu za rejea. Kamati ya kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi za Wizara ilifanya kazi hiyo kwa awamu mbili; awamu ya kwanza ilianza mwezi wa tano hadi wa sita 2018 na kuwasilishwa kwenye kikao cha menejimenti ya Wizara tarehe 15 mwezi Nane 2018 na awamu ya pili ilipitia sheria husika na taarifa iliwasilishwa kwenye kikao cha menejimenti cha tarehe 19/12/2018. Ifuatayo ni taarifa ya awamu zote mbili: 5.2.2 Taarifa ya awamu ya kwanza Kamati hii ilifanya kazi kwa kuangalia na kuzingatia mambo yafuatayo; umuhimu wa Sekta ya Malikale katika kukuza utalii hapa nchini, Umiliki wa vituo vya Mambo ya Kale vitakavyoboreshwa; Mapendekezo ya Muundo wa Usimamizi na Uendelezaji wa Vituo; Masuala ya watumishi walioko vituoni kwa sasa na baada ya maboresho; Ushiriki wa Sekta binafsi katika kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale; Mapitio ya sheria ya Mambo ya Kale katika masuala ya uwekezaji na ushirikishaji; Mapendekezo ya namna bora ya kujenga uwezo wa Idara ya Mambo ya Kale na Taasisi/Mashirika katika kuendesha na kusimamia vituo vya Mambo ya Kale; Mgawanyo wa mapato yatokanayo na viingilio vya watalii katika vituo vitakavyoboreshwa; Mapendekezo ya Vituo vitakavyopewa kipaumbele katika kuboresha na Taasisi na Mashirika hayo; na mapendekezo ya namna ya kuendesha vituo hivyo kibiashara na Mgawanyo wa Vituo. Ifuatayo ni taarifa ya Kamati awamu ya kwanza (nina nukuu 5.2.3 hadi 5.2.6). 5.2.3 Muundo wa Usimamizi na uendeshaji wa vituo vya malikale Kamati ilipitia Sera ya Malikale ya mwaka 2008 pamoja na Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 ya mwaka 2002 na kubaini kuwa Sera inaruhusu watu binafsi, taasisi za umma na binafsi kuwekeza katika malikale. Hivyo, kupendekeza usimamizi na uendeshaji wa vituo kwa kipindi chote cha uboreshaji kuwa kwenye taasisi. Aidha, vituo vya malikale ndani ya maeneo yaliyohifadhiwa visimamiwe na taasisi/mamlaka husika na Idara ya Mambo ya Kale itoe maelekezo ya kisera na kisheria. Katika kipindi chote cha uboreshaji, Kamati ilipendekeza vituo viwe chini ya usimamizi na uendeshaji wa taasisi kupitia mikataba wa makubaliano (MoU) itakatayosainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Wizara na Wakuu wa taasisi husika. Mapitio ya MoU yatafanyika baada ya miaka mitatu endapo kutakuwa na haja ya kufanya hivyo. Vile vile, Kamati inapendekeza kuundwa kwa Mamlaka maalumu ndani ya sekta itakayokuwa na jukumu la kumiliki, kusimamia na kuendesha vituo na maeneo ya Malikale yatakayobaishwa kuwa na sifa za malikale. Hivyo, vituo vitakavyoboreshwa na taasisi vikabidhiwe kwa Mamlaka hiyo ili Idara ibaki na majukumu ya kusimamia Sera na Sheria ikiwa ni pamoja kubaini maeneo mapya. Msingi wa pendekezo la kuanzishwa kwa Mamlaka unatokana na vituo hivi kuwa na mahitaji mengi ikiwemo wigo mpana wa taaluma na ujuzi unaohitajika ambao Wizara haiwezi kuupata kupitia muundo wa wake. Aidha, ni vigumu kwa Wizara kuendesha vituo hivi kibiashara kutokana na misingi ya kuanzishwa kwake na maelekezo ya Serikali.

53 5.2.4 Mapendekezo ya mgawanyo wa mapato Kamati ilijadili kwa kina kuhusu mgawanyo wa mapato na kubaini kuwa uboreshaji wa vituo unahitaji kiasi kikubwa cha fedha. Uwekezaji mkubwa kama huu kupitia taasisi na mashirika ni lazima ufuate taratibu na upate kibali cha Msajiri wa Hazina ambaye ni Msimamizi wa Mashirika na Taasisi hizi kibajeti. Hivyo, Kamati inapendekeza kuwa mapato yote yatakayopatikana kutokana na shughuli za malikale katika vituo hivi yakihusisha shughuli za kiutafiti na kiutalii yakusanywe na taasisi zitakazoendeleza kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti Na.11 ya mwaka 2015 na kusiwepo na mgawanyo wa mapato ili yabaki katika vituo kwa ajili ya shughuli za usimamizi na uendeshaji. Aidha, Kamati ilipendekeza kuwa ushiriki wa Idara ya Mambo ya Kale katika utekelezaji wa majukumu yake ndani ya vituo hivi upitie kwenye bajeti za Mashirika na Taasisi ambazo zimeandaliwa kwa mujibu wa sheria tajwa hapo juu. 5.2.5 Usimamizi wa watumishi katika vituo vitakavyoboreshwa Kamati ilipendekeza watumishi waliopo katika vituo vitakavyoboreshwa wawe chini ya usimamizi wa taasisi na stahili za posho za kiutumishi zilipwe kwa viwango vya taasisi husika. Mashariti mengine ya ajira zao yabaki kama yalivyo katika barua zao za ajira. Lengo la watumishi kuwa chini ya taasisi katika muda wa maboresho ya vituo ni kujenga uwezo wa taasisi kusimamia sekta ya malikale na pia kurahisisha mawasiliano na utendaji kazi wakati wa maboresho. Watumishi hao watarejea Idarani wakati wowote watakapo hitajika au mara baada ya Mamlaka ya Usimamizi na Uendeshaji wa Vituo vya Mambo ya Kale itakapoundwa. 5.2.6 Mapendekezo ya namna ya kuendesha vituo kibiashara Kamati ilipendekeza kuwa taasisi zitakazopewa kituo kwa ajili ya maboresho ianishe na kuandaa mpango wa matumizi ya ardhi ili kuruhusu uwekezaji; mpango biashara wa kila kituo; na kutangaza vivutio vilivyopo kwenye vituo hivi ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji. Kazi hizi zimeainishwa kwenye Mpango Mkakati. Aidha, baadhi ya mapendekezo kwenye hadidu za rejea ni sehemu ya Mpango Mkakati wa uboreshaji wa Sekta. 5.3 Taarifa ya Awamu ya Pili 5.3.1 Kuchambua Sheria za Taasisi na Mambo ya Kale Kamati iliwasilisha taarifa ya awamu ya kwanza kwenye kikao cha Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi na kuagiza 15/08/2018. Kikao hicho kilitoa maamuzi kuwa kamati hiyo ipitie sheria zote za Taasisi na Mambo ya Kale na kuangalia namna ya kutekeleza maagizo haya kwa kutumia sheria hizo. Hii ni kwa sababu uhifadhi wa maeneo ya Mambo ya Kale ni kwa mujibu wa sheria ya Malikale hali kadhalika Taasisi husika nazo zinatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. Utekelezaji Kamati hiyo ilikutana kwa mara ya pili mwezi tisa 2018 na ilichambua sheria ya Mambo ya Kale pamoja na sheria za taasisi zote za Wizara zinazotarajiwa kuhamishiwa vituo ili kubaini iwapo sheria inaruhusu utaratibu huo. Sheria zilizochambuliwa ni: Sheria ya Mambo ya Kale, Sura 333; Sheria ya Makumbusho ya Taifa, Sura 281; Sheria ya Hifadhi za Taifa, Sura 282;k Sheria ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Sura 284; Amri ya kuanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tangazo la Serikali Na. 135 la mwaka 2014); na Amri ya kuanzisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Tangazo la Serikali Na. 269 la

54 mwaka 2010. Baada ya uchambuzi, Kamati imejirisha kuwa hakuna ukinzani wa kisheria katika kuhamisha vituo na kufanya uwekezaji kwa maelekezo ya Waziri. Ili kufanikisha adhima hii, maelekezo ya Waziri yanatakiwa kuenda sambamba na Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya kale kukabidhi vituo kwenye taasisi kwa kuzingatia kifungu cha 25 cha Sheria ya Mambo ya Kale. Kamati ilichambua na kufanya kazi ya kuoanisha wa Sheria na utaratibu wa kukabidhi vituo kama ifuatavyo (na nukuu 5.3.2 hadi 5.3.3): 5.3.2 Sheria ya Hifadhi za Taifa “Makabidhiano yatafanyika baina ya Mkurugenzi wa Mambo ya Kale na Bodi ya Wadhamini na Mkurugenzi Mkuu. Aidha Waziri kupitia kifungu cha 16 cha Sheria ya Hifadhi za taifa, Sura 282 atatoa maelekezo kwa Bodi ya Wadhamini kupitia “Administrative Directive” akiwataka Wadhamini kuboresha na kusimamia vituo hivyo. Baada ya makabidhiano, Bodi ya Wadhamini watatumia mamlaka yao chini ya kifungu cha 18 kufungua Ofisi za Shirika katika vituo hivyo”. 5.3.2.1 Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Makabidhiano yatafanyika baina ya Mkurugenzi wa Mambo ya Kale na Bodi ya Wakurugenzi na Mhifadhi. Kifungu cha 6 kinaipatia Bodi mamlaka ya kutekeleza masuala yote ambayo itaona yanafaa kwa lengo la kuongeza sifa ya Mamlaka na kuongeza imani ya umma (public confidence); kufanya chochote na kuingia katika makubaliano yoyote ambayo Bodi itaona yanalenga kuwezesha utendaji mzuri wa kazi za Mamlaka ikiwa ni pamoja na kuanzisha matawi ndani ya Jamhuri ya Muungano. Aidha, kifungu cha 19 kinampa Rais mamlaka ya kutoa maelekezo ya jumla au mahususi kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Bodi, kwa kuwa Mhe. Rais alitoa “instrument” kwa Waziri kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Waziri anaweza kutoa maelekezo “Administrative Dicrective” akiitaka Bodi ya Wakurugenzi kuboresha na kusimamia vituo hivyo. 5.3.2.2 Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Makabidhiano yatakuwa baina ya Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Kale na Bodi ya Wakurugenzi na Mkurugenzi Mkuu. Kwa mujibu wa Muundo wa TAWA (Organization Structure) Waziri anaweza kutoa maelekezo kwa Bodi ya TAWA “Administrative Directive” akiitaka Bodi ya Wakurugenzi kuboresha na kusimamia vituo hivyo. 5.3.2.3 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Makabidhiano yatafanyika baina ya Mkurugenzi wa Mambo ya Kale na Bodi ya Ushauri na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Aidha, kupitia kifungu cha 5 cha Sheria ya Wakala wa Serikali, Waziri au Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii atatoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa TFS “Administrative Directive” akiitaka Bodi ya Wakurugenzi kuboresha na kusimamia vituo hivyo. 5.3.2.4 Makumbusho ya Taifa Kifungu cha 4 cha Sheria ya Makumbusho ya Taifa kinatoa mamlaka kwa Bodi ya Makumbusho ya Taifa kushirikiana na chombo au mtu mwingine ikiwemo Serikali Kuu au Serikali za Mitaa katika kutekeleza majukumu yake. Kifungu cha 25 kinampatia Mkurugenzi wa Mambo ya Kale mamlaka yakuteua “Honorary Antiquities Wardens” ambao watakuwa na jukumu la kusaidia kusimamia utekelezaji wa Sheria hii na kuzuia na kubaini makosa chini ya sheria hii. Aidha Waziri kupitia kifungu cha 6 cha Sheria ya Mashirika ya Umma, Sura 257 ikisomwa kwa pamoja na Waraka wa Uteuzi wa Waziri atatoa maelekezo kwa Bodi

55 ya Makumbusho ya Taifa kupitia “Administrative Directive” . Makabidhiano yatafanyika baina ya Mkurugenzi wa Mambo ya Kale na Bodi ya Makumbusho ya Taifa.

Vituo vya Malikale ambavyo vinalengwa kuingizwa katika utaratibu huu vilianzishwa na vinasimamiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mambo ya Kale, Sura 333(kifungu cha 4). Hivyo utaratibu wowote wa kuviboresha na kuvisimamia lazima uzingatie matakwa ya sheria hiyo. Taasisi yoyote itakayopewa jukumu la kusimamia vituo hivi lazima ipewe mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Mambo ya Kale. Ili Taasisi hizi ziweze kusimamia vituo hivyo, lazima majukumu ya Mkurugenzi yakasimishwe kwa Watendaji Wakuu ambao watasimamia vituo hivyo. Hii itawawezesha kutekeleza Sheria ya Mambo ya Kale na itawezekana kwa kutumia kifungu cha 25 cha Sheria ya Mambo ya Kale ambacho kinasema: “The Director may appoint fit and proper persons to be Honorary Antiquities Wardens for the purpose of assisting in the carrying out of the provisions of this Act and, in particular,k but without prejudice to the generality of the foregoing, in the prevention and detection of offences under this Act.” Kwa kifungu hiki Mkurugenzi wa Mambo ya Kale atateua Wenyeviti wa Bodi au Wakuu wa Taasisi kulingana na sheria ya taasisi husika kuwa Wahifadhi wa Mambo ya Kale wa heshima na kuwakasimisha majukumu ya kutekeleza chini ya sheria hiyo. Aidha, ili kuleta usimamizi wa pamoja wa maeneo hayo, kifungu cha 20 cha Sheria ya Mambo ya Kale kinachohusu Baraza la Ushauri wa Malikale kitumike kuunda Baraza ambalo litajumuisha Watendaji Wakuu wa Taasisi ambazo zitapewa jukumu la kuboresha na kusimamia vituo hivi. Baraza hili litasaidia kuendeleza mshikamano wa vituo hivi kwa kuwa vyote vitaendelea kusimamiwa chini ya Sheria ya Mambo ya Kale, kumuwezesha Mkurugenzi wa Mambo ya Kale kuendelea kuratibu uendelezaji wa vituo hivi kwa kuwa atakuwa ndiye Katibu wa Baraza hili, kuwezesha kuishauri Serikali kuhusu masuala ya uendelezaji wa Malikale nchini.

Boma la Tanga lililokarabatiwa na Taasisi ya Urithi Tanga

56 5.3.3 Taasisi kuteuliwa kuwa Wahifadhi wa heshima “Honorary Antiquities Wardens” wa vituo vya Malikale Wizara iliziteua Bodi za Taasisi za TANAPA, TAWA, TFS, NCAA, na NMT kuwa Wasimamizi wa Malikale wa Heshima (Honorary Antiquities Warden) kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 na kuwakasimisha vituo vya mambo ya kale kwa ajili ya kuviendeleza kama ifuatavyo:-

Taasisi Vituo vilivyopangwa Wilaya Mikoa Na 1.1 Magofu ya Engaruka Monduli Arusha 1.2 Engare-sero Ngorongoro Arusha 1 NCAA 1.3 Mumba Rock Shelter Karatu Manyara 1.4 Mapango ya Amboni Tanga Mjini Tanga 1.5 Kimondo cha Mbozi Mbozi Songwe 2.1 Magofu ya Tongoni Tanga Mjini Tanga 2.2 Ngome Kongwe- Bagamoyo Bagamoyo Pwani 2.3 Tembe la Kwihara - Tabora Tabora Mjini Tabora 2 TFS 2.4 Old Afya Building Tabora Mjini Tabora 2.5 Magofu ya Kaole Bagamoyo Pwani 2.6 Michoro ya Miambani ya Kolo Kondoa Dodoma 3.1 Magofu ya Kunduchi Kinondoni Dar es Salaam 3 TAWA 3.2 Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Kilwa Lindi 4.1 Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere Kinondoni Dar es Salaam 4.2 Makumbusho ya Caravan Serai Bagamoyo Pwani 4 TANAPA 4.3 Eneo la Zana za Mawe -Isimila Iringa Vijijini Iringa 4.4 Makumbusho ya Mkwawa- Kalenga Iringa Vijijini Iringa 4.5 Makumbusho ya Dkt. Livingstone – Ujiji Kigoma Kigoma

5.3.4 Kikao cha Uongozi wa Idara ya Mambo ya Kale na Katibu Mkuu Baada ya Maamuzi ya kikao cha tarehe 19/12/2019 cha Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi utekelezaji uliendelea ambapo Wizara ilikasimisha vituo hivyo kwa ajili ya maboresho au kuviendeleza kiutalii kuongeza muda wa Watalii kuishi Tanzania kwa lengo la kukuza pato la taifa na pia kuimarisha uhifadhi wa kumbukumbu hizo. Tarehe 5-6 Desemba 2019 Idara ilifanya kikao cha Uongozi wa Idara na baadhi ya viongozi wa Wizara kwa lengo la kupeana taarifa kuhusu vituo kukasimiwa kwenye Taasisi na baadhi ya majukumu ya Idara kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa. Aidha, katika kikao cha Wakuu wa Vituo waliambiwa taratibu za kuhamishwa kwa watumishi na vituo vitakavyo kasimiwa kwa Taasisi.

57 Kikao cha Wakuu wa Vituo Februari 5-6 2019 kuhusu kuendeleza vituo kwa kutumia Taasisi za Wizara kwa kuzingatia maagizo ya Mh. Waziri wa Maliasili na utalii na Sheria. 5.4 Kuendeleza Kituo cha kumbukizi ya Mwalim Nyerere Magomeni Makumbusho hii ya Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ipo chini ya usimamizi wa Idara ya Mambo ya Kale toka mwaka 2001 na imeanza kupokea wageni mwaka 2011. Nyumba hii kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ipo Kata ya Mzimuni, Mtaa wa Makumbusho, barabara ya ifunda plot namba 62, katika Tarafa ya Magomeni, Wilaya ya kinondoni. Nyumba hii inalindwa na kuhifadhiwa chini ya sheria ya Mambo ya Kale Na 10 ya mwaka 1964 na marekebisho ya sheria 22 ya mwaka 1979 na Sura 333 ya mwaka 2002 Hii ni moja ya Nyumba za Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliyoishi kipindi cha harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika mwaka 1959. Nyumba hii kwa sasa ni Makumbusho kumbukizi ya mwalimu Julius kambarage nyerere Rais wa kwanza wa Tanganyika na baadae Tanzania. Baadhi ya Mikakati na mipango ya kudai uhuru wa taifa letu ilifanyika katika nyumba hii, jambo ambalo limefanya nyumba hii kuwa na umuhimu mkubwa katika historia ya nchi yetu. Hivyo Idara ya Mambo ya kale inatunza nyumba hii kwa lengo la kutunza historia na kuelimisha jamii juu ya harakati za mwalimu nyerere katika Ukombozi wa Nchi yetu. 5.4.1 Maagizo aliyotoa Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Ukarabati wa Nyumba ufanyike mapema ili kulitoa katika hatari ya kuharibika zaidi pamoja na kurudisha hadhi ya historia ya jengo, hii ni pamoja na kujenga paa upya, kuziba nyufa, kupaka rangi, kubadilisha geti na milango, ukarabati wa choo na mabomba ya maji pamoja na ukuta. Kuangalia namna ya kuongeza eneo kwa kununua nyumba za jirani na kupata mahali kuegasha magari, kujenga ofisi za wafanyakazi pamoja na jengo la taarifa (information center), chumba cha maktaba ili kuruhusu jamii kusoma makala za Mwalimu Nyerere pamoja na chumba cha studio kwa ajili ya audio na video za mwalimu Nyerere.

58

Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni, Dar es Salaam

Picha zote mbili;

Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) Tarehe 26 Januari 2018 kwenye Nyumba ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni, Dar es Salaam

59 5.4.2 Ukarabati wa Nyumba ya Mwalimu Nyerere Mheshimiwa Waziri alielekeza Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Idara ya Mambo ya kale kwa kushirikiana na kituo cha Nyumba kumbukizi ya Mwl. Nyerere kuendelea na uboreshaji wa Kituo cha Nyumba kumbukizi ya mwalimu Nyerere, wakati taratibu za manunuzi ya nyumba mbili zikiendelea. Wizara kupitia kitengo cha Manunuzi (DPMU aliwasiliana na wakala wa ujenzi wa taifa (TBA) ili kutathmini gharama za ukarabati wa Nyumba ya Mwalimu Nyerere pamoja na kushauri kwa michoro juu ya ujenzi wa Jengo jipya litakalokuwa na Ofisi za watumishi, kituo cha kutolea taarifa, maktaba na studio, pamoja na kutoa makadirio ya gharama ya ujenzi wa jengo hilo. Gharama za ukarabati wa Nyumba ya Baba wa Taifa ni sh 116, 488,253.50 na Ujenzi wa jengo jipya la taarifa na ofisi ni sh 670,380,760.00 haya ni makisio ya TBA. Tarehe 3 Mei 2018 TANAPA walitembelea Nyumba kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ili kufatilia maagizo ya Muheshimiwa Waziri, pamoja na kuchukua BOQ ya TBA juu ya ukarabati wa Nyumba kumbukizi ya Mwalimu Nyerere na Ujenzi wa Jengo Jipya. Baada ya kikao cha menejimenti ya Wizara tarehe 19 Desemba 2019 uliridhia mgawanyo wa maeneo kwenye Taasisi, Nyumba ya ya Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni ilikabidhiwa TANAPA Feb 2019 kwa ukarabati na mkandarasi ameshaanza kazi. Aidha, Mwezi March 2019 bodi ya TANAPA iliendelea kufanya ukaguzi wa maeneo yote matano yaliyokasimishwa TANAPA na Wizara ambayo ni Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere, Makumbusho ya Caravan Serai, Mkumbusho ya Zana za Mawe –Isimila, Makumbusho ya Chifu Mkwawa- Kalenga na Makumbusho ya Dkt. Livingstone – Ujiji 5.4.3 Upanuzi, Eneo la Kituo cha Kumbukizi ya mwalimu Nyerere Magomeni Wizara kupitia Idara na Mkuu wa Kituo cha Nyumba kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ilifanikiwa kuwapata wamiliki wa Nyumba zinazotakiwa kununuliwa pamoja na Mkurugenzi wa manispaa ya Wilaya ya kinondoni na wote wamekubali kuachia maeneo yao kwa ajili ya upanuzi ili kupanua eneo la Kituo hicho cha makumbusho kumbukizi ya mwalimu Nyerere lakini kwa makubaliano tofauti. Mkurugenzi wa Manispaa ya kinondoni alikubali kutoa eneo la ofisi ya kata na kuomba kupatiwa Vyumba Vya ofisi tano (5) zitakazotumiwa na Mkurugenzi wa kata, Mtendaji wa kata. Diwani, na watumishi wengine wa Kata hiyo. Faustin Kanga, Mmiliki wa Kiwanja namba 61W, Nyumba namba 196, alikubali kutoa Nyumba yake kwa Masharti ya yeye kununuliwa Nyumba ingine yoyote maeneo ya magomeni mpaka upanga yenye ukubwa unaokaribiana na Nyumba yake, taratibu zinaendelea kupata nyumba ingine na Abel Edward Kasonga, Mmiliki wa Kiwanja namba 60W, Nyumba na 193, amekubali kutoa Nyumba yake lakini alipwe gharama za nyumba hiyo. Manunuzi ya Nyumba mbili taratibu kwa ajili ya upanuzi wa eneo hilo zinaendelea. 5.4.4 Tathmini ya thamani ya Nyumba hizo kupitia Afisa Ardhi wa Serikali (government valuer). Katika taratibu za manunuzi serikali kabla ya kununua kiwanja na Nyumba yeyote lazima tathmini ifanywe kupitia Wizara ya ardhi. Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale kwa kushirikiana na Idara ya DPMU na Mkuu wa Kituo cha Nyumba Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere, iliwasiliana na Wizara ya Ardhi wa Serikali kwa ajili ya kufanya tathmini ya thamani/gharama za Nyumba hizo ili kujua bei stahiki ya Nyumba hizo. Kazi ya tathimini kwa nyumba zote tayari imefanyika mwezi August 2018. 5.4.5 Mawasiliano na TANAPA TANAPA katika kutekeleza agizo la Mh. Waziri la kukiendeleza Kituo hiki cha Magomeni tarehe 3 Mei 2018 TANAPA walitembelea Nyumba kumbukizi ya Mwalimu Nyerere ili kufuatilia maagizo ya Mheshimiwa Waziri, pamoja na kuchukua BOQ ya TBA ya ukarabati

60 wa Nyumba kumbukizi ya Mwalimu Nyerere na Ujenzi wa Jengo Jipya ambao utafanyika baada ya kununua nyumba mbili za jirani. Wizara imeteua Bodi ya Taasisi ya TANAPA, kuwa Msimamizi wa Malikale wa Heshima (Honorary Antiquities Warden) kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mambo ya Kale Na. 333 na walishakasimiwa Kituo kwa ajili ya kukiendeleza. 5.4.6 Hati ya Nyumba kumbukizi Mwalimu Nyerere Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alijenga nyumba hiyo kiwanja Na 62 kitalu ‘w’ Magomeni yenye hati 13085 mwaka 1959 na alikabidhi kwa Bwana mmoja aliyeitwa Ndugu Tibandebage (Balozi). Mwaka 1964 Nyumba hiyo ilichukuliwa/kununuliwa na NUTA- Chama cha wafanyakazi ambacho kwa sasa ni TUCTA. Mwaka 1974 walimrudishia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kama zawadi wakati akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 10 tangu kuzaliwa NUTA alikabidhiwa na wanaharakati kwa kazi nzuri aliyoifanya kwa Ukombozi wa Tanzania na Afrika. Mwalimu Nyerere aliipokea lakini aliamua kuikabidhi serikalini na hatimaye kukabidhiwa Idara ya Mambo ya Kale ambayo ndiyo iliyokuwa na dhamana ya kuhifadhi vitu vya Kihistoria au Kale. Nyumba hiyo ilikabidhiwa bila hati. Wizara kupitia Idara na watumishi wa Kituo cha Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere mwezi wa kumi 2018 ilifuatilia hati hiyo TUCTA (NUTA). TUCTA walikabidhi kimaandishi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii hati hiyo kupitia Idara ya Mambo ya Kale na sasa imehifadhiwa Wizarani. Kwa vile Wizara ilikuwa haina Hati ya Nyumba ya Kumbukizi ya mwalimu Nyerere hivyo ilikuwa ni vigumu kuhifadhi na kuendeleza eneo husika. Kwa vile Hati hiyo ya nyumba ipo Wizarani kwa sasa hivi, Wizara inaedelea na taratibu za kuibadilisha na kupata hati ya Wizara kwa jina la Idara ya Mambo ya kale. Pia, Wizara inaendelea na taratibu za kuitangaza kama urithi wa Taifa kwenye gazeti la serikali (Government Notice). 5.5 Idara ya Mambo ya Kale kuhamisha baadhi ya majukumu kwenda Makumbusho ya Taifa. Wizara iko katika mpango wa kuboresha Sekta ya Malikale ili iweze kuhifadhi, kusimamia na kuendeleza malikale kama kumbukumbu za urithi wa utamaduni wa Taifa, vituo vya elimu na mafunzo; na vivutio vya utalii. Kusudio la Serikali ni kuimarisha Sekta ya Malikale ili kuhakikisha kuwa inatoa mchango mkubwa kiuchumi na kijamii katika kuongeza pato la Taifa. Katika kufanikisha azma hiyo, Wizara imekasimisha vituo vya Mambo ya Kale kwenda kwenye Taasisi na baadhi ya majukumu kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa ili Idara ya Mambo ya Kale ibaki na jukumu la kuratibu na kusimamia Sera na Sheria za Sekta. Kwa makusudio hayo, Wizara iliunda kikundi kazi chenye Wajumbe kutoka Taasisi ya Makumbusho ya Taifa, Idara ya Mambo ya Kale, Idara ya Sera na Mipango, Idara ya Utawala na Rasilimaliwatu; na Kitengo cha Sheria kuangalia ni majukumu gani yahamie Makumbusho. Kikundi kazi hicho kilipitia muundo na majukumu ya Idara ya Mambo ya Kale kuona ni majukumu yapi yanatakiwa kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa. 5.5.1 Muundo na Majukumu ya Idara ya Mambo ya Kale Kwa mujibu wa Muundo wa Idara ya Mambo ya Kale wa Septemba 2018, Idara inaongozwa na Mkurugenzi, akisaidiwa na Wakurugenzi Wasaidizi wawili wanaoongoza Sehemu za Uhifadhi na Ufundi; na Maendeleleo ya Urithi wa Utamaduni na Mawasiliano. Kada za watumishi watendaji zinajumuisha Wahifadhi Mambo ya Kale, Wahifadhi Mambo ya Kale

61 Wasaidizi, Mafundi Wahifadhi na Mafundi Wahifadhi Wasaidizi. Aidha, kwa mujibu wa Sera ya Malikale ya mwaka 2008, Sura ya Tano, kifungu 5.1, majukumu ya Idara ni: 1) Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria ya Malikale; 2) Kusimamia uhifadhi na ulinzi stahili wa malikale; 3) Kutambua na kuanzisha mfumo wa usimamiaji wa malikale kwa kushirikiana na jamii na wadau; 4) Kusimamia, kuendesha na kuratibu utafiti wa malikale; 5) Kuhifadhi na kuendeleza maeneo yenye malikale kwa ajili ya kumbukumbu, vituo vya mafunzo; na utalii; 6) Kuhamasisha matumizi endelevu ya malikale kama kumbukumbu za Taifa, vituo vya elimu na mafunzo; na vivutio vya utalii; 7) Kuendeleza utalii wa malikale kwa viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa; 8) Kusimamia, kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa unaohusu masuala ya malikale. 5.5.2 Majukumu ya Idara ya Mambo ya Kale yanayopendekezwa kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa Baada ya uchambuzi wa Sera, Sheria na Miundo ya Kitumishi inayohusu Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa, Kikundi kazi kilibaini kuwa majukumu yanayotakiwa kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa ni pamoja na: 1) Kuhifadhi, kuendeleza na kulinda maeneo ya malikale; 2) Kuandaa na kutekeleza Mipango ya Usimamizi na Uendelezaji wa malikale; 3) Kuanzisha na kuendesha mifumo ya datakanzi za malikale; 4) Kuhamasisha uhifadhi wa malikale kwa kushirikisha Jamii; 5) Kuhamasisha utalii wa utamaduni; 6) Kufanya utafiti wa malikale Tanzania Bara; 7) Kuanzisha makumbusho na vituo vya kumbukumbu na taarifa; 8) Kuhamasisha matumizi endelevu ya malikale kama kumbukumbu za Taifa; 9) Kuendeleza vivutio vya utalii wa malikale kwa viwango vinavyokubalika Picha zifuatazo A, B, C and D ukurasa wa 63 zinazoonyesha baadhi majukumuyaliyokuwa yatekelezwa na Idara ya Mambo ya Kale kuhamishiwa Makumbusho ya Taifa.

62

C B

Picha za juu; Ukarabati wa Gofu la Ngome ya mreno/Gereza (B,C) Kilwa, kuziba mipasuko katika kuta, kurudisha dari katika baadhi ya vyumba.

A D Utafiti wa uchimbuzi wa mabaki ya Chuma Uchambuzi baada ya Utafiti: Chanzo Makumbusho ya Taifa- Prof. Terry Harisson na Dkt. Amandus Kweka.

5.5.3 Majukumu yanayobaki Idara ya Mambo ya Kale Baada ya kuhamisha baadhi ya majukumu kwenda Makumbusho ya Taifa, majukumu yanayobaki Idara ya Mambo ya Kale ni kama ifuatavyo: 1) Kuandaa, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya Uhifadhi, Utafiti na Uendelezaji wa Malikale; 2) Kuratibu na kurekebu uhifadhi, uendelezaji na ulinzi wa malikale; 3) Kuandaa Vigezo vya kutambua na kusimamia malikale katika ngazi mbali mbali; 4) Kuandaa Vigezo vya kuanzisha makumbusho na vituo vya kumbukumbu na taarifa; 5) Kuandaa Orodha ya Maeneo ya Mambo ya kale; 6) Kuratibu na kuhamasisha utalii wa urithi wa utamaduni; 7) Kuanzisha, kusimamia, kuendeleza na kudumisha ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa unaohusu masuala ya malikale na makumbusho.

63 5.6 Hatua iliyofikiwa ya uendelezaji wa vituo vya Mambo ya Kale Sehemu kubwa ya maelekezo ya Mheshimiwa Waziri kupitia hotuba ya bunge la bajeti ya mwaka 2018/2019 yametekelezwa kama ifuatavyo: 5.6.1 Wizara iliunda vikundi kazi vya aina mbili moja ni kwa ajili ya kuangalia taratibu na sheria zinazohusika katika kuendeleza vituo vya Mambo ya Kale kwa kutumia Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utalii bila kuathiri utendaji wa Taasisi hizo. Kamati hii ilijumuisha Taasisi zote za Wizara TANAPA, Wakala wa Misitu(TFS), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro(NCAA), Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania 5.6.2 Kamati ya pili ilihusika na kuangalia ni majukumu yapi ya Mambo ya Kale yahamie Makumbusho ya Taifa na Idara ibakie na majukumu ya kisera na sheria na kupendekeza muundo mpya wa Idara ya Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa 5.6.3 Wizara ilipokea taarifa hizo na katika utekelezaji Wizara iliziteua Bodi za Taasisi za TANAPA, TAWA, TFS, NCAA, na NMT kuwa Wasimamizi wa Malikale wa Heshima (Honorary Antiquities Warden) kwa mujibu wa kifungu cha 25 cha Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 na kuwakasimisha vituo vya mambo ya kale kwa ajili ya kuviendeleza. 5.6.4 Mwezi Februari 2019 TANAPA walikasimishwa jengo la Nyumba ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Magomeni Dar es Salaam na Mkandarasi ameanza kazi. 5.6.5 Mwezi March 2019 bodi ya TANAPA iliendelea kufanya ukaguzi wa maeneo yote matano yaliyokasimishwa TANAPA na Wizara ambayo ni Nyumba ya Kumbukizi ya Mwl. Nyerere, Makumbusho ya Caravan Serai, Mkumbusho ya Zana za Mawe –Isimila, Makumbusho ya Kalenga na Makumbusho ya Dkt. Livingstone – Ujiji. 5.6.6 NCAA tayari wameunda kamati ambayo imeshaanza kupita maeneo yaliyokabidhiwa ikiwemo Engaruka, Engarasero, Michoro ya Mumba, Kimondo cha Mbozi, na Mapango ya Amboni. 5.6.7 Kamati iliyohusika na kuaangalia ni majukumu yapi ya Mambo ya Kale yahamie Makumbusho ya Taifa na Idara ibakie na majukumu ya kisera na sheria imekamilisha na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho amepelekewa ili atoe maoni Kazi zilipelekwa Makumbusho na Muundo Mpya wa Idara na Makumbusho; 5.6.8 Katika kutekeleza maelekezo haya ya Wizara ya kukasimu vituo Uongozi wa Wizara ilibidi kukutana na Viongozi na Wakuu wa vituo vya Mambo ya Kale kwa lengo la kuwapa habari Wakuu wa vituo kuhusu kuendeleza vituo kwa kutumia Taasisi na hatua zilizochukuliwa na taratibu zitazotumika kuhamisha vituo na Watumishi. 5.6.9 Sehemu kubwa ya kazi iliyokuwa ngumu imeshafanyika ambapo Wizara imeteua taasisi kuwa Taasisi kuteuliwa kuwa Wahifadhi wa heshima “Honorary Antiquities Wardens” baada ya mjadala mrefu wa wataalam na Mh Waziri amearithia na Administrative Directive” zimesainiwa, pia baadhi majukumu ya Mambo ya Kale yameainishwa yatakayokwenda Makumbusho ya Taifa na Idara kubaki na masuala ya kisera na kisheria. Kazi iliyobaki ni utekelezaji au utendaji 5.6.10 Kisheria Wizara imekasimisha vituo 15 kati ya 16 kwa Taasisi za TANAPA, NCAA, TFS na TAWA kwa kutumia ratiba iliyoandaliwa. Waliohusika katika zoezi hili ni Wakuu wa Vituo, Idara ya Mambo ya Kale, Kitengo cha Manunuzi, Sheria, Mhasibu mkuu, Idara ya Mipango na Utawala.

64 Kushoto: kikundi kazi cha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ikitembelea Kimondo cha Mbozi na kilizungukia maeneo yote ya Mambo ya Kale yaliyokasimishwa NCAA.

Bodi ya Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania TANAPA ilitembelea Makumbusho ya Mtwa Mkwawa Kalenga na ilizungukia maeneo yote ya Mambo ya Kale yaliyokasimishwa TANAPA. Kushoto:Nyumba Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalim Nyerere Magomeni ilikasimishwa TANAPA na Ukarabati ulianza kufanyika Machi 2019 na wakati huo majadiliano yanaendelea ya upanuzi wa eneo hilo ili kupatikana sehemu ya kujenga ofisi na kituo cha taarifa au maktaba.

65 SURA YA SITA

UTANGAZAJI NA UHAMASISHAJI WA VIVUTIO VYA MALIKALE 6.1 Utangulizi Sura hii inaelezea utangazaji na uhamasishaji wa maeneo ya Malikale yalioyopo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii hasa vituo vya Mambo ya Kale na Makumbusho ya Taifa Utangazaji wa vivutio vya Malikale ni muhimu unasaidia kizazi kilichopo kupata historia ya kizazi kilichopita kujua walikuwa wana maisha ya aina gani na walikuwa wanarithishanaje. Kwa upande wa pili husaidia kupata pato kwa jamii na kwa Taifa kama vitatangazwa ipasavyo kujulikana ndani na nje ya nchi. Wageni watakaokuja kutembelea Malikale aidha kupata historia ya nchi, vizazi vilivyopita na vilivyopo na utamaduni wao. Aidha, wanafunzi kujifunza na kufanya utafiti wa maeneo hayo ya kihistoria. Uhamasishaji unafanywa kuelimisha jamii umuhimu wa Malikale na kuzihifadhi. Kwa siku za nyuma utangazaji wa vivutio vya Malikale ulikuwa sio kipaumbele. Vivutio hivi vilikuwa vimehifadhiwa zaidi kwa ajili ya kumbukumbu,elimu na utafiti. Hata sheria ya Mambo ya Kale Na 10 ya mwaka 1964 ilikuwa inasisitiza na kutilia mkazo kwenye utafiti utunzaji na uhifadhi. Kadiri ya miaka ilivyokuwa inapita kasi ya maendeleo na mabadiliko ya uchumi, jamii, siasa na mazingira iliongezeka sana Wizara ya Maliasili na utalii iliona umuhimu wa kuendeleza zao hili la Malikale kiutalii kwa lengo la kupata vivitio vingi vya utalii kwa lengo la kupata mapato na vituo hivi kuweza kujihudumia vyenyewe. Hivyo Sera iliamua kuwa Sera itakayo kuwa dira katika kuhifadhi na kuendeleza vivutio hivi vya Malikale bila kuharibu uhalisia. Lengo la jumla la Sera ya Malikale ni kuboresha mchango wa Sekta ya Malikale katika kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za utamaduni ikiwa ni pamoja na kuendeleza utalii wa urithi wa utamaduni kwa ajili ya ustawi wa taifa na kizazi kijacho. 6.2 Ushiriki wa Idara katika utangazaji na uhamasishaji Idara ilianza kushiriki na kutangaza utalii wa utamaduni kupitia maonesho ya Historia, Sanaa na Utamaduni kwa Nchi za Afrika Mashariki; Utumishi wa umma; Nane nane; Sabasaba; Wiki ya Utalii; na Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na uchapisha wa vipeperushi na matangazo mbalimbali kwa lengo la kuuza Idara kitalii. Katika awamu ya tano Idara imeshiriki katika maonesho ya Sabasaba yaliyofanyika kuanzia tarehe 28/06 hadi 13/07/2018, katika uwanja wa maonesho wa kimataifa wa Sabsaba jijini Dar es Salaam; Kauli mbiu ikiwa ni “Ukuzaji wa biashara kwa maendeleo ya viwanda”. Vionyeshwa vilivyotumika vilikua ni vipeperushi, vitabu na mabango yanayoelezea matumizi endelevu ya Malikale. Wadau wa ndani walihamasika kutembelea vituo vya Malikale. Idara imeshiriki katika maonyesho ya Historia, Sanaa na Utamaduni kwa Nchi za Afrika Mashariki yaliyofanyika Kampala Uganda kuanzia tarehe 05 – 12/09/2017; Vionyeshwa vilivyotumika vilikuwa ni vipeperushi, vitabu na mabango yanayoelezea matumizi endelevu ya Malikale;Kauli mbiu ikiwa ni, “Utamaduni na ubunifu kichocheo cha umoja na ajira”. Vile vile mwaka 2017 Idara ilishiriki katika maonesho ya Nane nane yaliyofanyika Mkoani Lindi na Tabora kwa kutumia watumishi wa vituoni kuanzia tarehe 1/8/2017 hadi 10/8/2017, kauli mbiu ikiwa ni, “Zalisha kwa tija mazao ya bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”. Vionyeshwa vilivyotumika vilikua ni vipeperushi, vitabu na mabango yanayoelezea matumizi endelevu ya Malikale. Idara ilishiriki katika maonesho ya siku ya utalii Duniani yaliyofanyika mkoani Iringa kuanzia tarehe 27/09 - 03/10/2017. Idara ilishiriki katika tamasha la 36 la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kuanzia tarehe 23/9/2017 hadi 30/9/2017 ambapo Vionyeshwa vilivyotumika vilikuwa ni vipeperushi, vitabu na mabango.

66 6.3 Maboresho kwenye Makumbusho za vituo vya Mambo ya Kale na Makumbusho

Maboresho ya Maonesho yaliyofanyika katika kituo cha Kaole, Bagamoyo Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuweka taarifa sahihi kulingana na tafiti zinazofanyika katika kituo cha kihistoria cha Kaole.

Maboresho ya Maonesho yaliyofanyika katika Makumbusho mpya ya Olduvai, Mkoa wa Arusha

Maboresho ya Maonesho yaliyofanya katika Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam kuhusu chimbuko la binadamu na wanyama mbalimbali.

67 6.4 Maonyesho ambayo Idara ilishiriki 2018 / 2019

Picha ya juu inaonyesha ushiriki wa Idara katika Tamasha la utamaduni wa Mtanzania lililofanyika kijiji cha Makumbusho Dar es Salam Octoba 2018 kwa ajili ya jamii ya Mkoa wa Lindi Mgeni rasmi katika ufunguzi Mheshimiwa Dkt. Harison Mwakiembe Waziri wa Habari, Michezo, Sanaa na Utamaduni.

Picha ya Kushoto Idara kupitia vituo vya Kaole, Mji Mkongwe na Caravan Serai ilishiriki Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni ambayo yaliandaliwa na kufanyika mji wa Bagamoyo Octoba Mwaka 2018.

68 6.5 Tamasha la Urithi Tanzania Wizara imebuni maadhimisho ya Tamasha la Urithi wa Taifa (Urithi festival). Lengo la Tamasha hilo ni kunadi urithi na utamaduni wa Mtanzania ndani na nje ya nchi. Tamasha litajielekeza zaidi kwenye historia, utamaduni, malikale, lugha, chakula, mavazi, imani, mila na desturi. Wizara kwa kushirikiana na wadau imeanza maandalizi ya maadhimisho ya Tamasha hilo yatakayofanyika Septemba kila mwaka katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Katika kutekeleza azma hiyo, Kamati ya Kitaifa imeundwa ili kuratibu maandalizi ya Tamasha hilo. Aidha, Tamasha litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kunadi vivutio vya urithi wa taifa, kuongeza uelewa wa wageni kuhusu Tanzania na idadi ya siku ambazo watalii watakaa nchini. Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la urithi lilofanyika kati ya Septemba 15 hadi 22 mwaka 2019 jijini Dodoma. “Kauli mbiu ya maonyesho haya ni ‘Urithi wetu Fahari yetu’ na yatahusisha wadau kuonyesha mambo ya burudani, maigizo, utalii na tamaduni, malikale na kazi mbalimbali za mikono na sanaa. Tamasha hili la Urithi lilifanyika Mkoa wa Dodoma, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha, Mto wa Mbu na Mikindani Mkoa wa Mtwara.

Picha ya juu Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu akifungua Tamasha la Urithi Dodoma. Mheshimiwa Balozi Ali Abeid Karume (Mb), Picha ya chini kulia alifunga Tamasha la Urithi, Dar es Salaam.

69 6.6 Kilele cha Tamasha la Urithi lilifanyika Arusha

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa, akifunga Tamasha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba

Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa,akitembelea banda la Wajasiliamali katika Tamasha la Urithi, lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha Oktoba 13, 2018.

Wananchi kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki Tamasha la Urithi jijini Dar es Salaam.

70 6.7 Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji Tanzania ni moja ya nchi mbalimbali ambazo zilitaliwa na wakoloni. Kabla ya ukoloni makabila yalikuwa na utawala na uongozi wao. Uongozi uliokuwepo wakati huo ni wa Machifu. Wakati wakoloni walipoingia walipata wakati mgumu wa kupambana na makabila mbalimbali kama Meli na Sina wa Moshi, Abushiri Pangani, Mkwawa Uhehe, Mirambo wa Tabora. Vita vya majimaji ni moja ya vita ambavyo wakoloni walipambana navyo kabla ya kuchukua madaraka. Vita hivyo vilianza mwaka 1905 hadi 1907 vilishirikisha Machifu mbalimbali kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania na pwani. Vilianzia vilima vya Natumbi Kaskazini, Magharibi mwa Kilwa 27 Februari 1905. Chanzo cha vita ni wananchi kupinga vitendo viovu hasa vya kulazimishwa kulima mazao ya biashara, kulipa kodi na unyanyasaji uliotokana na mfumo wa utawala wa uliokuwepo. Walioanza vita ya majimaji ni Machifu na mganga wa jadi kutoka jamii za Wangindo, Wangoni, Wapogoro, Wandendeule, Wabena, Wasangu na nyingine nyingi. Jina la maji maji lilitokana na dawa iliyochanganywa na maji, punje za mahindi na mtama zilizosadikika kuwa zitampa mpiganaji kinga ya kutodhurika na shambulio la Risasi za Wajerumani. Mahenge ilikuwa ni kitovu cha Mapambano iliwabidi wajerumani kutumia na kuzima vita isizidi zaidi sehemu za magharibi mwa eneo la Uhehe. Vita ilidumu kwa kadiri ya miaka miwili Julai 1905 – Agost; 1907 (Chanzo - Makumbusho ya Maji maji - Songea mkoani Ruvuma). Kila mwaka Mkoa wa Ruvuma huadhimisha maadhimisho haya katika eneo la Makumbusho ya Majimaji. Kila mwaka kuanzia mwaka 1980 kila ifikapo tarehe 27 Februari wazee wa Baraza la Makumbusho ya Majimaji Songea Mkoa wa Ruvuma walikuwa wanaadhimisha siku hiyo kwa kuwakumbuka Machifu wao walionyongwa katika vita ya Majimaji na utawala wa Kijerumani. Eneo la Makumbusho ya majimaji linaonyesha makaburi ya Machifu walionyongwa wakati wa utawala wa Mjerumani na wakati wa vita ya majimaji 1905-1907. Makaburi hayo yapo mawili moja walilozikwa watu wengi ikiwa ni pamoja na machifu na moja alilozikwa Chifu Songea ambaye alinyongwa baada ya Machifu wengine. Makaburi hayo yapo katika hali nzuri. Makumbusho haya ya mashujaa wa vita vya Majimaji Songea yalikadhiwa Makumbusho ya Taifa mwaka 2010. Ni eneo ambalo limehifadhiwa vizuri na Serikali ili kuwawezesha watu mbalimbali kutembelea na kujifunza mambo mengi na ukibahatika kufika katika eneo hili utakuta kumbukumbu nyingi za kale ambazo ni kivutio kikubwa kiutalii na kiutamaduni. Wizara kupitia Idara hushirikiana na Makumbusho ya Taifa na Mkoa Ruvuma kuhahakikisha eneo hili linahifadhiwa na Maadhimisho haya ya kumbukizi ya vita vya Majimaji yanafanyika kitaifa na pia wakati mwingine hushirikisha nchi nyingine zenye Machifu wa Wangoni.

Picha hii inaonesha Wazee wa baraza la mila na desturi Mkoa wa Ruvuma kila mwaka wanawaombea mashujaa 67 waliouwawa wakati wa vita vya Majimaji.

71 6.7.1 Kilele cha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji Mwaka Februari 2016

Katika Kilele cha Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji 27 Februari 2016, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa manispaa ya Songea katika maadhimisho hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Mashujaa eneo la Makumbusho ya Majimaji mjini Songea alisema, serikali iko tayari kutoa utaalamu na miongozo kwa wadau wote ambao wako tayari kuanzisha makumbusho katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Ruvuma. Pia alisema, wakati umefika kwa sekta binafsi kuona umuhimu wa kuibua, kuanzisha na kushiriki kikamilifu katika uhifadhi na matumizi endelevu ya urithi wa utamaduni kwa lengo la kujipatia ajira na kuchangia katika mapato. Aidha, alisisitiza kuwa kuna haja halmashauri za wilaya, manispaa, majiji, taasisi za umma na watu binafsi kujenga utamaduni wa kutunza kumbukumbu pamoja na kuanzisha makumbusho na kuvitumia kama vituo vya mafunzo na vivutio vya utalii. Sera na sheria zinazosimamia urithi wa utamaduni zinaruhusu sekta binafsi kuwekeza katika urithi wa utamaduni. Mwisho Meja Jenerali, Gaudence Milanzi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii a Ameipongeza Serikali ya Mkoa wa Ruvuma chini ya Mkuu wa Mkoa huo Said Mwambungu kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhimiza uendelezaji wa utalii na urithi wa utamaduni katika mkoa huo. Aliongeza kuwa, hatua na juhudi zinazofanywa na Serikali ya Mkoa wa Ruvuma zinapaswa kuigwa na viongozi wa mikoa mingine wa kutumia urithi wa utamaduni katika kuchangia katika kutoa ajira, kuongeza kipato na kupunguza umasikini kwa baadhi ya familia hapa nchini. Katika kilele cha Maadhimisho ya kumbukizi ya vitavita ya majimaji kwa mwaka 2016 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu aliwapongeza familia ya Hayati Mfaume Kawawa kwa uamuzi wao nzuri kwa kukabidhi kuitoa nyumba hiyo kwa serikali ili iwe sehemu ya makumbusho ya taifa hatua ambayo itachangia sana kuongeza kwa vivutio vya utalii katika mkoa wa Ruvuma. Alisema uamuzi wa familia hiyo ni wa kijasiri kwa kuwa wangeweza kubadili matumizi ya nyumba hiyo na kuwapatia fedha nyingi. “Hata hivyo kutokana na moyo wao wa uzalendo kwa nchi yao wameamua kujitoa kwa serikali, jambo

72 linalopaswa kuigwa na watu wengine,” Alisema kutokana na umuhimu wa nyumba hiyo, Serikali ya Mkoa wa Ruvuma kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili itahakikisha inatunza nyumba hiyo ili iweze kutumika kwa lengo lililokusudiwa. Alisema nyumba hiyo itasaidia kuongeza ajira na kipato kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma. Mwambungu anasema ni matumaini ya wakazi wa mkoa huo watatumia fursa hiyo kujifunza historia mbalimbali za nchi hii pamoja na waasisi wa nchi yetu kupitia kumbukumbu alizoziacha marehemu Kawawa. Aliwaomba wananchi wanaoishi jirani na maeneo hayo kuhakikisha wanatoa ulinzi wa kutosha. 6.7.2 Kuanzishwa kwa Makumbusho ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa Katika kipindi hiki cha awamu ya Tano Familia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa ilikabidhi nyumba iliyokuwa ikitumiwa na familia hiyo kuwa Makumbusho ya Taifa tarehe 27 Februari 2016 siku ya Kilele cha Maadhimisho ya kumbukizi ya majimaji.

Picha ya Juu familia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa wakisaini Makabidhiano ya Nyumba itakayokuwa Makumbusho ya Hayati Rashid Mfaume Kawawa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali, Gaudence Milanzi na Mwanasheria wa Mkoa tarehe 27 Februari 2016. Picha ya Kushoto Mwanasheria wa Mkoa wa Ruvuma akisaini Makabidhiano

73 Familia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa ilikabidhi nyumba kwa Wizara ya Maliasilia na Utalii na Mkoa wa Ruvuma ili itumike kama Makumbusho kwa Taifa. Hati ya makabidhiano ikisainiwa na Wanafamiliwa Mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali, Gaudence Milanzi kama inavyoonekana hapo juu. Mtoto wa nne wa Mzee Kawawa, Hadija Kawawa alisema, familia hiyo imeamua kutoa nyumba hiyo kwa sababu Mzee Kawawa enzi za uhai wake alitumia muda wake mwingi kwa ajili ya kutoa mchango wa maendeleo kwa nchi yake bila kujali kile anachopata. Anasema Mzee Kawawa licha ya kuwa kiongozi mkubwa wa nchi, alishiriki moja kwa moja katika ukombozi wa Tanganyika na kuungana na wanaharakati wa ukombozi wa nchi nyingine kwa lengo la kuhakikika Afrika inakuwa huru. Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa maarufu kama Simba wa Vita ambaye ni miongoni mwa viongozi wachache hapa nchini ambaye Watanzania vizazi hadi vizazi wataendelea kumkumbuka siyo kutokana na kuwa mmoja wa waasisi wa taifa letu tu bali hata kutokana na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji wake kwa taifa hili. Akipokea nyumba hiyo kwa niaba ya serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali, Gaudence Milanzi, anasema serikali imekubali kupokea nyumba hiyo na kumbukumbu zote zilizopo ili itumike kwa ajili ya jamii kupata kumbukumbu ya nchi yao. Nyumba hiyo itakuwa ya pili kutolewa kwa familia za waasisi wa taifa letu ambapo nyumba ya kwanza ni ya mwasisi wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere iliyopo eneo la Magomeni, Dar es Salaam, mbali na nyumba iliyopo katika kijiji cha Butiama mkoani Mara. Nyumba hizo kwa pamoja zimeanza kutumika kwa ajili ya kumbukumbu mbalimbali za nchi ambapo wageni kutoka nje wanafika kwa lengo la kupata taarifa za kiongozi huyo. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amewataka viongozi na watumishi wa serikali hapa nchini, kuwa na moyo wa uzalendo, uadilifu na uvulivu kwa nchi yao na kujiepusha na tabia ya wizi na ufisadi, ambavyo vinachangia sana kurudisha nyuma juhudi kubwa zinazofanywa na baadhi ya watendaji wengine wa serikali ya kupigania maendeleo kwa nchi yao. Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, wakati wa hafla ya kupokea nyumba ya hayati Dkt. Rashid Kawawa iliyopo eneo la Bombambili kata ya Bombambili katika Manispaa ya Songea na kuifanya kuwa ya makumbusho ya taifa kwa ajili ya kumbukumbu ya kiongozi huyo wa zamani. Mwambungu anasema, hayati Dkt. Kawawa enzi za uongozi na uhai wake alikuwa mtu mpole na msikivu kwa kila mmoja jambo ambalo lilimletea heshima kubwa ndani na nje ya nchi ndiyo maana aliweza kushika nafasi mbalimbali kubwa katika nchi hii. Hayati Dkt. Mzee Rashid Mfaume Kawawa Simba wa vita alikuwa kiongozi shupavu aliyewahi kutokea, ambapo alikuwa kiongozi adhimu sana na mwenye moyo wa ajabu katika kuipigania nchi yake katika ufanyaji wa kazi mbalimbali za maendeleo. Alikuwa ni mtu asiyeogopa kazi hadharau kazi, hana makuu, hana makundi, hana majungu. Mdogo wake akifanywa mkubwa wake atafanya kazi chini yake kwa moyo wake wote, na uwezo wake wote; bila manung’uniko, na bila kinyongo. 6.7.3 Uzinduzi wa Makumbusho ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa Nyumba ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa baada ya Familia ya hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa kukabidhi nyumba kwa Wizara ya Maliasilia na Utalii na Mkoa wa

74 Ruvuma ili itumike kama Makumbusho kwa Taifa ilizinduliwa rasmi tarehe 27/02/2017 kama Makumbusho na Waziri wa Maliasili na utalii Mh. Prof. Jumanne Maghembe mbele ya Mkuu wa Mkoa, Dkt. . Nyumba hiyo itakayoonyesha maisha yake Hayati Dkt. Mzee Rashid Mfaume Kawawa “Simba wa vita” na vitu alivyokuwa akivitumia katika nyumba hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, tarehe 27 Februari 2017 Mheshimiwa Prof. Jumanne Maghembe akizindua Nyumba iliyokabidhiwa serikalini na familia ya Hayati Dkt. Rashidi Mfaume Kawawa

Kwenye picha kulia inaonyesha tarehe ambayo Makumbusho Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa ilifunguliwa na Mheshimiwa Prof. Jumanne Maghembe na kulia ni baadhi ya vionyeshwa vilivyopo kwenye Makumbusho hiyo.

75 Picha ya Juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Bilinith Mahenge wakiangalia baadhi ya Nishani alizokuwa amepewa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa.

Picha za chini, kulia inaonyesha mlango wa kuingilia kwenye Handaki lililoko kwenye nyumba hiyo na kuna njia ya kutokea nje ya nyumba kama inavyoonekana kwenye picha ya Kulia. Hii ilikuwa ni kwaajili ya usalama wa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa na familia yake ndio maana nyumba hiyo ilikuwa na Handaki.

76 6.7.4 Maadhimisho ya Kumbukizi ya Vita vya Majimaji Mwaka 2017 Idara ilishiriki katika maadhimisho ya kumbukuzi ya majimaji yaliyofanyika Mkoa wa Ruvuma tarehe 05-07 Februari 2017 Mkoa wa Ruvuma na katika maadhimisho hayo Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Magembe alifungua Makumbusho ya Nyumba ya Kawawa ambayo ilikabidhiwa Wizara ya Maliasili na Utalii na alikuwa mgeni wa heshima katika maadhimisho hayo na aliweka silaha ya jadi (rungu) kwenye mnara wa kumbukumbu ya mashujaa waliouawa kwa kunyongwa na wakoloni kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya miaka 110 ya vita vya Maji Maji yaliyofanyika mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea.

Picha ya Kushoto Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) 2017 (katikati) akizungumza na wananchi kwenye siku ya kilele cha Maadhimisho ya kumbukizi ya vita vya Maji Maji.

Kushoto Balozi wa Ujermani Nchini Dkt. Dethef Waechter Februari mwaka 2019 akiweka shada la maua kwenye kaburi la mashujaa 66 lililopo Makumbusho ya Majimaji Songea, Mkoa wa Ruvuma .

77 6.8. Kumbukizi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale na Kituo cha Magomeni iliweka onyesho kwenye nyumba ya Mwalimu Nyerere Magomeni tarehe 14/Octoba 2018 kwa ajili ya kukumbuka siku ambayo baba wa Taifa alifariki. Onyesho hilo lilivutia wageni wa nje na ndani kuazia asubuhi hadi jioni kituo kilipata wageni mbalimbali na walipata historia ya Baba wa Taifa. Tukio hilo linaonekana kwenye picha zinazofuata

Kushoto juu maandalizi na kulia mapokezi ya Wageni mbalimbali wa ndani na nje Nchi.

Wageni mbalimbali wa ndani na nje Nchi wakipata taarifa mbalimbali kutoka kwa Watumishi wa Idara ya Mambo ya Kale tarehe 14/Octoba 2018

78 SURA YA SABA MIKATABA YA KITAIFA, KIMATAIFA NA KUTOA USHAURI WA KITAALAM 7.1 Umuhimu wa Mikataba ya Kimataifa Shughuli nyingi za uhifadhi na uendeshaji wa malikale katika nchi yoyote zinahitaji sana suala zima la ushirikiano wa kitaifa kikanda na kimataifa. Mashirika haya yanasaidia kutoa fedha kwa ajili ya shughuli za uhifadhi; kujenga uwezo wa uendeshaji kwa njia ya misaada ya kiufundi, mafunzo, utafiti na ubadilishaji wa uzoefu; na kuwezesha utekelezaji wa majukumu. Baadhi ya mashirikino haya ni jumuiya ya kikanda, mashirika ya kimataifa, mikataba na miongozo ya kimataifa. Mashiriano hayo yamegawanyika katika makundi yafuatayo: 7.1.1 Jumuiya za Kikanda a) Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki; b) Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC); na c) Mfuko wa rasilimali za Urithi wa Utamaduni wa Dunia wa Afrika (AWHF). 7.1.2 Mashirika ya Kimataifa a) Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO),Paris b) Baraza la Kimataifa la uhifadhi wa Maeneo na Majengo ya Kihistoria ( ICOMOS); c) Kituo cha Kimataifa cha Mafunzo ya Uhifadhi na Ukarabati wa Malikale ICCROM); d) Baraza la Kimataifa la Makumbusho (ICOM). Serikali imerithia mikataba minne inayohusu uhifadhi wa urithi wa Utamaduni ambayo ni: Mkataba wa mwaka 1954 (The Hague Covention) ambao unahusu uhifadhi wa vifaa au maeneo ya malikale wakati wa vita; Mkataba wa mwaka 1970 unaozuia uingizaji ndani au utoaji nje ya nchi malikale haramu bila kuzingatia sheria za kitaifa na kimataifa uliorithiwa tarehe mbili Augusti, 1977; Mkataba wa mwaka 1972 unaohusu Uhifadhi na Ulinzi wa maeneo yenye Malikale na Asilia zilizopo katika Urithi wa Dunia tarehe mbili Augusti, 1977; na Mkataba wa mwaka 2003 unaohusu Uhifadhi na Ulinzi wa Urithi wa Utamaduni usioshikika uliorithiwa tarehe 18 Novemba, 2011. Mikataba hii Nchi inanufaika kwa kuhahakikisha kwamba hatua stahiki zinachukuliwa ili kulinda, kuhifadhi na kuendeleza Urithi wa Utamaduni nchini. Watumishi wa Idara wamekuwa wakipata mafunzo ya uhifadhi kutoka kwenye mashirika ya kimataifa na kikanda. Idara imekuwa nayo inapata fedha kutoka kwa mashirika haya kwa ajili ya kuendeleza maeneo ya malikale nchini. Mashirika haya yamesaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kuwa Magofu ya Urithi wa Dunia ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara yanaondolewa kwenye urithi wa utamaduni ulio kwenye hatari ya kutoweka (‘endangered World Heritage Site’) kwa kutoa misaada ya kifedha na utalaamu kwa watumishi wa Idara. Kwa kurithia mikataba hiyo Tanzania imenufaika na taasisi za UNESCO ambazo ni ICCROM, ICOMOS, na ICOM zinajihusisha na uhifadhi wa Malikale na Watumishi wa Idara wamekuwa wakipata mafunzo ya uhifadhi kutoka kwenye Taasisi hizi. 7.2 Kufanya tathmini ya Majengo ya kihistoria yenye asili ya Kijerumani yaliyopo nchini Wizara ilipata ufadhili kutoka Ubalozi wa Ujerumani kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya hali ya majengo 45 kwa majengo yenye asili ya Kijermani na imefanyika Januari na Februari

79 2018 katika Mikoa 10. Kazi iliyofanyika kupitia ufadhili wa Serikali ya Ujerumani. Kazi za Tathmini zilitekelezwa katika mikoa ya Dar, Tanga, Dodoma, Kilimanjaro, Lindi, Mtwara, Arusha, Mwanza , Tabora, Pwani, na Mara.Majengo kumi yaliyochaguliwa ambayo yanaweza kukarabatiwa ni: Cliff Block – Bombo Hospital – Tanga; Gunzert House – Mwanza; Fort Ikoma – Serengeti; Afya Building – Tabora; Dodoma Boma- Dodoma; Custom House – Mikindani; Lukuledi Main House (Masasi); Lindi Governors House; Hospital & Primary School ( Kilema) na Old Fort – Bagamoyo. 7.3 Mradi wa Kuhifadhi Magofu ya Kisiwa cha Mafia Mkoa wa Pwani Wizara ilipata ufadhili wa USD 150,000 kutoka Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya ukarabati na uhifadhi wa Magofu ya Kua yaliyopo Kisiwa cha Juani, Wilaya ya Mafia, Mradi huu unatekelezwa kwa kushirikiana na Taasisi ya “World Monument Fund” (WMF) kama wataalam washauri na watekelezaji wa Mradi. Mradi huu ulianza Marchi 2018 .Kazi ambazo zimeshafanyika na Mradi huu mpaka sasa sehemu kubwa ya magofu yote ya Kua yamekarabatiwa. Kazi bado inaendelea na inatarajiwa kukamilika Mwaka 2019. 7.4 Mkataba kati ya Idara ya Mambo ya Kale na NCAA Wizara ilisaini Mkataba ya kati ya Idara ya Mambo ya NCAA Mwaka 2014 ambao unaendelea mpaka sasa hivi. Moja ya makubaliano ni NCAA kusimamia kituo hicho na kukusanya maduhuli lakini asilimia 50 ya maduhuli yanayopatikana yanaletwa Idara ya Mambo ya Kale. Mmiliki wa vituo vya Mambo ya Kale ni Idara ya Mambo ya Kale hivyo uhifadhi, ukarabati na uendelezaji wa kituo hicho lazima Idara ya Mambo ya Kale ishirikishwe kikamilifu.Aidha Mradi umeanzisha Kikundi cha Kijamii (CBO) ambacho kimejengewa uwezo wa Ukarabati 7.5 Kutoa ushauri wa kuhifadhi Malikale Idara hutoa ushauri wa kuhifadhi malikale kwa kuanzia mtu mmojammoja , Taasisi za umma na binasi , kwenye mashirika au vikundi mbalimbali na kwa serikali na viongozi mbalimbali. Kwa mwaka 2019/2018 Idara ilipata ombi la kutoa utaalam wa kuhifadhi majengo ya Kihistoria ya Shule ya Msingi Mwisege, Mkoani Mara. Shule hii ni moja ya shule ambazo amesoma Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika ziara yake Mkoani Mara tarehe 05 Septemba 2018 alipata fursa ya kutembelea shule ya Msingi Mwisege iliyopo Manispaa ya Musoma na aliagiza Uongozi wa Mkoa wa Mara kuhahakikisha miundombinu ya shule hiyo inafanyiwa ukarabati. Idara tayari ilishatoa ushauri kuhusu ukarabati wa shule hiyo.

Kamati ya Kudumu ya Bunge la Ardhi, Maliasili na Utalii wakiangalia Handaki (Mreshe) katika Chuo cha wanyamapori Mweka Mkoani Kilimanjaro kama kivutio cha Utalii.Idara hutekeleza maelekezo, maagizo na ushauri unaotolewa na viongozi mbalimbali wakiwemo Wabunge na Mawaziri.

80 SURA YA NANE MAONI, USHAURI NA HITIMISHO 8.1 Maoni au ushauri kuhusu Malikale Mafanikio Makubwa katika serikali hii ya awamu ya Tano kwa Idara ya Mambo ya Kale ni kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya Malikale Kiutalii, hili ni zao jipya la utalii kama yataendelezwa ipasavyo. Mwanzoni maeneo haya yalikuwa yamehifadhiwa kwa ajili ya Elimu na kumbukumbu. Wizara kupitia Idara ya Mambo ya Kale iliweka Mkakati kuimarisha miundo mbinu iliyopo katika vituo au maeneo ya Malikale yaliyopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ili kuweza kukidhi mahitaji ya kitalii katika kiwango cha kinachokubalika kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja na kujenga vituo vya kuwapokea wageni na kuwapa taarifa kabla kutembelea kituo husika, kuweka miundo mbinu ya maji, umeme ambavyo vilikuwa havipo katika vituo vingi na kujenga mahali pa kupumzika na kupata chakula. Katika Serikali hii ya awamu ya Tano, Waziri wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Dkt. Hamisi Kigwangalla (Mb) pamoja na Uongozi wote wa Wizara wametoa mwongozo na msukumo mzuri wa kuendeleza Maeneo ya Malikale yaliyopo chini ya Wizara kwa kutumia Taasisi za Wizara. Tayari kazi hiyo imeanza kutekelezwa mwaka 2018/2019 ambapo maeneo 18 yaliyopo chini ya Wizara tayari yamekasimiwa kwenye Taasisi kwa kuteuliwa kuwa Wahifadhi wa Heshima “Antiquieties Honorary Waden”. Lengo ni kuhifadhi maeneo haya yaweze kutumika kwa Elimu, kumbukumbu na kiutalii. Kinachotakiwa ni kuzingatia sheria na taratibu za Mambo ya Kale katika kuhifadhi Malikale hizo ili ziendelee kuwepo maana Malikale ni utambulisho wa jamii husika, ukoo na taifa. Hivyo jukumu la uhifadhi ni muhimu kwa manufaa ya Taifa na nchi kwa ujumla. Kwa Malikale zilizo kwenye sekta binafsi, sera ya Malikale ya Mwaka 2008 imeweka utaratibu wa jamii husika kuhifadhi na kuziendeleza. Malikale nyingi ziko mikononi mwa jamii yenyewe, hivyo jamii hushauriwa kuzihifadhi kwa kuzingatia miongozo inayotoa maelekezo ya namna bora ya kuhifadhi na kunufaika na Malikale hizo ili kupata kipato na kupunguza uharibifu. Serikali kwa kipindi chote inafanya kazi na jamii kwa kutoa miongozo ya kuzingatiwa na kuhakikisha kuwa malikale ya nchi haiharibiwi wala kupotea na wakati mwingine hutafuta wafadhili kwa ajili ya uhifadhi wa maeneo hayo. Mfano mzuri ni Makumbusho ya Mkoa wa Iringa na Mikindani Mtawara. Miongozo pia imewekwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa kazi zote zinazohusu malikale unapata ridhaa ya wamiliki na kutambuliwa na uongozi wa Serikali eneo lilipo kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa. Ushiriki wa Sekta binafsi, Taasisi na Jamii mbalimbali katika uhifadhi na matumizi endelevu ya Urithi wa Utamaduni ni moja kati ya nyenzo muhimu katika kuhifadhi historia na urithi wa utamaduni wa vizazi vilivyopita. Ushirikishwaji wa Sekta binafsi au Taasisi mbalimbali na Jamii katika kuhifadhi na kuendeleza malikale ni kuwezesha urithi wa utamaduni uliopo kuhifadhiwa katika hali nzuri zaidi na kwa njia hii jamii itatambua kuwa kutunza, kuhifadhi na kuendeleza Malikale ni jukumu la kila mtu. Uhifadhi wa Malikale unasaidia vizazi vijavyo au jamii ijayo kuona vitu halisi vitokanavyo na ujuzi au ufundi na utamaduni waliokuwa nao vizazi vilivyopita au kilichopo na kutambua urithi huo kama utambulisho wao kiukoo, kikabila na kitaifa.

81 Wananchi wamekuwa wakichangia katika utoaji wa taarifa kwa watafiti wa malikale na kushiriki katika utafiti huo kwa viwango tofauti, jambo ambalo limeifanya Tanzania kuwa na mchango mkubwa katika kukua kwa sayansi ya malikale duniani. Katika kuchangia huduma za maendeleo katika baadhi ya vijiji, wanajamii wanatoa huduma ya ulinzi wa hiari wa malikale iliyoko katika maeneo yao hivyo ni vizuri kuwapongeza na kuangalia namna ya kuweka mahusiano mazuri. Raslimali ya Malikale ikitumika ipasavyo inaweza kuwa ni njia nyingine kwa jamii kujipatia kipato bila kuathiri uhalisia. 8.2 Hitimisho Sekta ya Malikale nchini Tanzania inaonyesha kukua kwa kasi kiutalii ambapo watalii na watafiti wanaendelea kuongezeka. Ili utalii wa malikale uweze kushindana Kimataifa, dhamira ya kweli na ya dhati kwa wadau wote inahitajika ili kuhifadhi na kuendeleza maeneo ya malikale na makumbusho kufikia viwango vya Kimataifa. Hivyo, ni muhimu jitihada za makusudi zikaelekezwa katika kuhifadhi, kuendeleza na kutangaza maeneo ya malikale kiutalii. Lakini ikumbukwe kuwa Malikale ni dhahabu yahitaji kulindwa na kuhifadhiwa kwa uangalifu, kwa sababu malikale nyingi ni za zamani hivyo ni tete (delicate or fragile) zikiharibiwa haziwezi kurudishwa katika hali yake ya awali. Kutokana na hatari iliyopo kuhusu kuharibika kwa malikale na kutorudishwa katika hali yake ya awali, kuna umuhimu wa wadau kuelimishwa na kushirikishwa katika uhifadhi na uendelezaji wake ili watambue kuwa kuna umuhimu wa kuzitunza na kuzilinda. Ushirikishwaji wa sekta binafsi jamii ua taasisi binafsi ni muhimu kwa sababu Malikale nyingi zipo mikononi mwao. Jamii ikielimishwa kuhusu faida inayotokana na uhifadhi wa Malikale, wao wenyewe watahifadhi kwa moyo mmoja kwa vile faida wanazijua ikiwa ni pamoja na kuwa ni utambulisho wao, kumbukumbu kwa kizazi kilichopo na kijacho na jamii au Taifa itanufaika na mapato yanayotokana na matumizi endelevu ya Malikale. Utangazaji wa vivutio vya malikale ni muhimu utaongeza idadi ya watalii na kupanua wigo wa mazao ya utalii. Hii itaongeza pato litakalotumika kwa uhifadhi na kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. Idara ya Mambo ya Kale kwa ujumla itaendelea na jukumu la kusimamia na kutoa ushauri wa uhifadhi, utafiti na uendelezaji wa Malikale kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali itakayowekwa kwa lengo la kudumisha uwepo wa Malikale hizo bila kuharibu uhalisia wa Urithi huo unaorithiwa kizazi hadi kizazi. Ni imani kuwa wasomaji wa kitabu hiki hasa wadau wa Malikale watahamasika na kushiriki kikamilifu katika kuhifadhi na kuwa na mpango wa matumizi endelevu ya Malikale kwa faida ya Kizazi cha sasa na kijacho.

82 UMRI milioni takribani Miaka 1.75 miaka Takribani millioni 3.6 Jurasia, cha Kipindi miaka milioni 150 Karne ya 13 hadi 15 Karne ya 19 Karne ya 19 Eneo aliloishi binadamu wa kale Eneo lenye nyayo za binadamu wa kale Afrika Mashariki katika Mapango makubwa ya jiolojia na Kati Amboni ina ukubwa wa ekari 39.5. na Waswahili wa na utamaduni Ushahidi wa makazi Uislamu. Makumbusho ya historia biashara utumwa kwenye kutoka Vipusa ya Utumwa na Njia ya Kati Biashara Ujiji Kigoma hadi Bagamoyo Majengo ya Historia Biashara Utumwa na vipusa watumwa, soko la kuelekea Bara Tanzania kutoka 1886 hadi Wajermani na Makao makuu ya Zanzibar Dar es Salaam. Boma 1900 kabla ya kuhamia Mzizima ni Ikulu kipindi hicho Ngome Kongwe kambi ya lilikuwa kijeshi, jengo la ushuru wa fedha kwenye, usagara house ya mazao, shule msingi mwambao stoo kwa ajili Waafrika shule ya kwanza na wajerermani ilijengwa ya hospitali kipindi hicho, Wazungu na Waarabu na kipindi hicho, Wajermani wilaya Bagamoyo ilijengwa ya na makaburi na wajermani lilijengwa soko la zamani Wajermani. UMUHIMU WAKE WILAYA WILAYA Ngorongoro Ngorongoro Mjini Tanga Mjini Tanga Bagamoyo Bagamoyo MKOA MKOA Arusha Arusha Tanga Tanga Pwani Pwani MAHALI KILIPO Kiambatisho Na. 1: Orodha ya Vituo vya Mambo ya Kale: Vituo ya Kiambatisho Na. 1: Orodha Makumbusho ya Bonde la Oldupai Eneo lenye Nyayo za Zamadamu, Laetoli ya lenye Mapango Eneo Amboni Eneo lenye Magofu ya Tongoni Makumbusho ya Kumbukizi ya Utumwa, Caravan Serai Mji Mkongwe Bagamoyo KITUO 1 2 3 4 5 6 Na.

83 UMRI Karne ya 13 300 takribani Miaka hadi 40,000 Karne ya 19 Karne ya 19 Haijulikani takribani Miaka 600,000 Karne ya 19 Karne ya 9 Karne ya 20 Karne ya 20 Ushahidi wa makazi na maisha ya Waswahili katika Waswahili ya na maisha Ushahidi wa makazi Afrika Mashariki Pwani ya Njia zilizotumika kuhifadhi na Kumbukumbu na taarifa na Kumbukumbu na kuhifadhi zilizotumika Njia za matukio kabla ya ugunduzi wa maandishi Kumbukumbu ya Biashara Utumwa kupitia njia za harakati Vipusa; ya Biashara Utumwa na kati kupiga marufuku biashara ya utumwa Kumbukumbu ya Biashara Utumwa kupitia njia za harakati Vipusa; ya Biashara Utumwa na kati kupiga marufuku biashara ya utumwa mwa 12 ni miongoni wa tani Kimondo chenye uzito vimondo kumi vizito duniani cha kipindi wa mawe katika muhula za mawe za Zana Acheulian wa na wakoloni kutawaliwa Ushahidi wa kupinga Tanganyika Kijerumani katika ardhi ya wa na utamaduni ya mwanzo Ushahidi wa makazi Afrika Mashariki katika pwani ya Waswahili wa na utamaduni ya mwanzo Ushahidi wa makazi Afrika Mashariki katika pwani ya Waswahili Mwl. Taifa wa Baba Hayati ya maisha za Kumbukumbu J.K. Nyerere UMUHIMU WAKE WILAYA WILAYA Bagamoyo Kondoa Mjni Tabora Kigoma Mjini Mbozi Iringa Vijijini Iringa Mjini Kilwa Kinondoni Kinondoni MKOA MKOA Pwani Dodoma Tabora Kigoma Mbeya Iringa Iringa Lindi Dar es Salaam Dar es Salaam MAHALI KILIPO Eneo lenye Magofu ya Kaole Michoro ya Miambani, Kolo Makumbusho ya Kumbukizi ya Dkt. Livingstone Kwihara, Makumbusho ya Kumbukizi ya Dkt. Livingstone, Ujiji cha Kimondo lenye Eneo Mbozi wa Makumbusho ya muhula mawe, Isimila Mtwa la Kaburi lenye Eneo Mkwawa, Kalenga Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara Magofu ya Kunduchi Makumbusho ya Kumbukizi J.K. Nyerere, Mwl. ya Magomeni KITUO 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 Na.

84 UMRI 600 Zaidi ya miaka iliyopita Karne ya 13-19 Ushahidi wa kilimo cha umwagiliaji katika ardhi ya Ushahidi wa kilimo cha umwagiliaji Tanzania Mji Mkongwe wa Kihistoria wenye Majengo ya Majengo wenye wa Kihistoria Mkongwe Mji na vipusa kutoka ya Utumwa Biashara ya kihistoria Bara kuelekea Tanzania UMUHIMU WAKE WILAYA WILAYA Ngorongoro Mikindani MKOA MKOA Arusha Mtwara MAHALI KILIPO Magofu ya Mfumo wa cha umwagiliaji Kilimo Engaruka Mji wa kihistoria wa Mji wa kihistoria Mikindani KITUO 17 18 Na.

85 Kiambatisho Na. 2 Faharasa

CA Chief Account - (Mhasibu Mkuu)

CBO Community based Organisation (Mradi wa Jamii)

DAHRM Director of Administration and Human Resources

(Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu)

DPMU Director of Procurement Management Unit

(Mkurugenzi Manunuzi)

ICOMOS International Council on Monuments and Sites

(Kamati ya Kimataifa ya Maeneo ya Malikale)

MB Member of Parliament - (Mbunge)

NMT National Museum of Tanzania - (Makumbusho ya Taifa ya

Tanzania)

NCAA Ngorongoro Conservation Areas Authority

(Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro)

TANAPA Tanzania National Parks (Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania)

TAWA Tanzania Wildlife Authority (Mamlaka ya Usimamizi

Wanyamapori Tanzania)

TFS Tanzania Forest Services Agency

(Wakala wa Huduma za Misitu)

WMF World Monument Fund (Mfuko wa Uhifadhi wa Majengo ya Kihistoria)

86 Marejeo: 1. Alison Redmayne, Mkwawa and Hehe Wars, The Jounal of African History 9 (3) 409-436 1968 cambridge.org 2. Erick Jordan, taarifa ya Julai hadi Desemba 2018 Kituo cha Chifu Mkwawa 3. Hamo Sasoon, Guide to the Mbozi Meteorite, 1967.,” Tanzania National Culture and Antiquities Division Ministry of community Development Dar es Salaam 4. Hamo Sasoon, Guide to the ruins at Kunduchi, 1966.,” Tanzania National Culture and Antiquities Division Ministry of community Development, Dar es Salaam 5. Hamo.Sassoon, Maelezo ya magofu yaliyo Kunduchi. 1966.,” African Pamphlet Collection; Idara ya Utamaduni na Mambo za Kale, Wizara ya Maendeleo na Utamaduni, 1966 Dar es Salaam Tanzania. http://www. indiana.edu/ Kalenga; 6. Jumanne Maburi, taarifa ya Julai hadi Desemba 2018.Kituo cha Amboni Tanga: 7. John Pareso, taarifa ya Julai hadi Desemba 2018; Kituo cha Engaruka 8. Kim Ann Zimmermann, 2013: Louis and Mary Leakey, olduvai Gorge oldest Evidence of Mankind’s Evolution; http://www.livescience.com 2013 9. Maadhimisho na historia ya miaka 150 ya ukristo Bagamoyo http:// sw.radiovaticana.va 10. Pamela W., The rock act of Iringa Region, Southern Tanzania 2013. 11. Paul Ndahani. taarifa ya Julai hadi Desemba 2018 Kituo cha Mji Mkongwe Mikindani 12. Paul Nyelo. taarifa ya Julai hadi Desemba 2018 Kituo cha Kimondo cha Mbozi Songwe 13. William Mwita, taarifa ya Maadhimisho ya Majimaji Songea Ruvuma 14. Wolf-dieter Heinrich, Robert Bussert and Martin Aberh Ablst from the past:the lost world of dinosaurs at Tendaguru, East Africa. (2011). 15. Zuberi Mobie, taarifa ya Julai hadi Desemba 2018.Kituo cha Michoro ya Miambani Kolo Kondoa

87 Picha za Matukio Mbalimbali.

Makabidhiano ya Vituo vya mambo ya Kale kwenye Taasisi. Picha hii inaonesha kikundi kazi cha Wizara Kikikasimisha vituo vya mambo ya kale vya Kwihara, Tabora na Ujiji Kigoma kwenye Taasisi za TFS na TANAPA.

Michoro hii ya Igeleke ipo Mkoa wa Iringa Kihesa Kilolo na inahifadhiwa na Taasisi binafsi ambayo ni kikundi cha KIUMAKI cha Kihesa Kilolo.

Jengo jipya la Makumbusho la Olduvai lililojengwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya (EU) na kwa kushirikiana na Wizara na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro iliyofunguliwa.

88 89 Kimondo hiki kilianguka katika Kijiji cha Ndolezi, Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Songwe.

90